Previous Lesson -- Next Lesson
g) Kristo yupo na alikuwepo kabla ya Ibrahimu (Yohana 8:48-59)
YOHANA 8:48-50
“Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je, sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo? Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu. Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kuutafuta na kuhukumu.”
Yesu aliondoa kifuniko cha nyuso za hao Wayahudi, akiwaonyesha upatano wao na roho ya Shetani kwa kutokujali ukweli.
Baada ya shambulio hili, roho mbaya alichokozwa atokee nje penye uwazi. Lakini kinyume cha kuungama na kuhuzunikia dhambi zao, walionyesha ushirikiano wao na ibilisi; walilkiri kwamba walitukana habari ya Yesu kuzaliwa na Roho Mtakatifu. Walimwita Msamaria, mtu wa kabila la mchanganyiko. Hivyo habari ya mwamko wa ki-samaria ilifika hadi Yerusalamu, na Wayahudi wenye ubaguzi wakawa wameudhika.
Sehemu fulani ya watu walifahamu mizizi ya Yesu kuwa ni ya kiyahudi, wakasisitiza kwamba yeye kweli ni Myahudi. Wengine lakini walisisitiza namna ya miujiza yake ni pamoja na msaada wa Shetani. Basi, waliopagawa na roho ya Shetani, hawakufahamu hali yao ya kweli, lakini walitangaza kwamba Mtakatifu wa Mungu amepagawa na Shetani. Hivyo, baba wa uongo aligeuza mawazo yao waseme: nyeupe ni nyeusi na nyeusi ni nyeupe.
Kwa taratibu na upole Yesu aliwajibu hao watu waliokuwa vipofu kiroho akisema, “Hakuna Shetani ndani yangu; nimejaa nguvu ya Roho Mtakatifu. Hakuna hata doa ovu inanikabili upande wa tamaa za dunia. Kweli na upendo kwangu zafurika; wala siishi kwa ajili yangu; najikana mwenyewe na kumheshimu Baba yangu; hii ndiyo kuabudu na kutukuza kwangu kwake.
Natangaza jina la Mungu kwenu na kumtukuza Baba kwa maisha yangu. Ndiyo, mimi nafunua kweli za Mungu kwenu, lakini ninyi mnanichukia, kwa sababu namweleza Mungu kuwa ni Baba yangu. Roho mbaya ndani yenu hapendi kuwatoka, ili kumwachia Roho wa Mungu nafasi hiyo. Hampendi kuwa watoto wa Huyu Mtakatifu, kwa hiyo mnanitukana na mnakusudia kufa kwangu. Sitafuti utukufu wangu, kwa vile nadumu daima ndani ya Baba. Yeye ananipigania, ananitunza, ananiheshimu na kunitukuza. Ndiye yeye atakayewahukumu, kwa sababu mnanikataa. Yeyote atakayemkataa Yule aliyezaliwa na Roho, atakuwa chini ya hukumu ya Mungu. Hii ni kwa sababu roho mwovu ni juu ya wale wanaokataa, akiwakataza wasimpokee Mwokozi.”
YOHANA 8:51-53
“Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo, Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?“
Yesu sasa atoa jumlisho la Injili yake akisema, - wote wasikiao neno lake wakilishika na kulitunza mioyoni mwao, watatambua kwamba maneno hayo yatakuwa na nguvu maishani mwao. Watapokea uhai wa milele, wasipotee daima. Kifo kwao itakuwa mlango kwenda kwa Mungu Baba yao; si kwa sababu ya wema wao, lakini kwa sababu maneno ya Kristo yanadumu ndani yao. - Je, wewe umeshika taratibu hiyo ya Ufalme wa Mungu? Wote wasioshika maneno ya Yesu mioyoni mwao wataanguka dhambini na ndani ya utawala wa Shetani. Wale washikao Injili na neno lake wataishi milele.
Wayahudi wakavurugwa kwa hasira, wakilia: “Wewe u Shetani, unasema uongo. Babu zetu wote wa imani wamekufa. Unaweza kusemaje basi, maneno yako yatawapatia uzima wa milele wale wanaokuamini? Wewe u bora kuliko Mwumbaji, kwa sababu unaahidi maisha yasiyokoma kwa kifo? Wewe u mkuu kuliko Ibrahimu, Musa na Daudi? Umejifanya mwenyewe kuwa Mungu.”
YOHANA 8:54-55
“Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neon lake nalishika.”
Kwa utaratibu Yesu akajibu na kufunua nafsi yake kwa karibu zaidi. Yeye Kristo hatafuti utukufu kwa ajili yake mwenyewe. Nafsi yake ni tukufu daima. Mungu anathibitisha heshima ya Mwanawe kwa vile Baba ni ndani ya Mwana, na kwa njia yake Ubaba wa Mungu unafunuliwa. Kwa kweli, Wayahudi walidai kwamba, yule Mmoja mwenye enzi ni Mungu wao, ila hawakumfahamu kwa kweli. Baba yao alikuwa ni Shetani akijificha ndani ya “jina la Mungu”, akitumia jina hilo kwa kudanganya. Wao walidai kuwa ni wacha Mungu, lakini walipungukiwa na roho ya upendo. Yeyote amjuaye Mungu, huyu anapenda jinsi Mungu anavyompenda. Kwa sababu hii dini yoyote inayotaja tu kushika jina la Mungu inatosha, basi haithibitishi thamani ya njia hiyo ya maisha; hivyo kanuni za imani hiyo ina makosa. Mungu ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Namna zote na majina ya kiini tukufu zinazotajwa na dini zingine hazina thamani, maana ni mawazo ya asili ya kibinadamu tu. Ukweli wa Mungu umo ndani ya umoja wa Utatu. Hivyo Yesu aliwakemea Wayahudi akisema, “Hammjui Yeye kweli. Maisha na mawazo yenu yanayo msingi wa uongo. Mmekuwa vipofu kwa ajili ya ukweli.” Hata hivyo Yesu alisisitiza kwamba yeye amjua huyu wa Milele. Kama sivyo, ushuhuda wake juu ya Ubaba ungekuwa ni uongo. Lakini Yesu alitangaza nafsi ya kweli ya Mungu mbele ya Wayahudi.
YOHANA 8:56-59
“Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.”
Baada ya Yesu kuwaambia Wayahudi kwamba hawamjui Mungu wa kweli, na ya kwamba nguvu ndani ya uchaji wao ni Shetani, akamalizia kwa kufunua umilele wake, ili wamkubali au wamkataa. Na pia akafunua uungu wake kwa mfano kutoka kwa Ibrahimu, huyu mtangulizi wa imani. Kwa njia hiyo, Yesu anatujulisha hata sisi kwamba, Ibrahimu aliishi na Mungu, na ya kwamba alifurahia kutambua kuingia kwake Kristo mwilini; maana kwa jambo hilo, ahadi iliyofanywa kwa Ibrahimu ikatimizwa, kwamba uzao wake siku moja utakuwa ni baraka kwa mataifa yote.
Kwa tamko hilo, Wayahudi wakashangazwa wakisema, “Wewe ni kijana na hata hivyo unasema kwamba umemwona Ibrahimu, aliyeishi miaka elfu mbila kabla ya sasa? Lazima akili yako ni ngonjwa.”
Yesu akaitika kwa maneno ya kifalme, “Kabla ya Ibrahimu, mimi niko.” Akaimarisha tamko hilo kwa kutanguliza, “Kweli, kweli, nawaambieni”; ili waweze kutambua kwamba yeye ndiye Mungu wa milele, sawasawa na Baba yake. Mapema kabla ya hapo Mbatizaji alikuwa ametangaza umilele wa Kristo. Makutano walikosa kufahamu ukweli huo, wala hawakuamini kwamba mtu angeweza kuwa Mungu wa milele.
Walichukua ushuhuda wa Kristo kuwa kama matukano, yakimshambulia Mungu; pia kama jambo lisilowezekana; ikawa kiasi cha kutokuweza kungojea tamko la hukumu, bali wakaokota mawe ya kumtupia. Walipokuwa tayari kumpiga kwa mawe, yeye akatoweka kati yao. Hatujui jinsi gani. Saa yake ilikuwa haijaja bado. Akaondokea kwenye lango la hekalu.
SALA: Bwana Yesu, tunakuabudu; wewe ndiwe Mungu wa milele, mwenye uaminifu na kweli, ukijaa upendo. Hutafuti utukufu kwa ajili yako, lakini unamheshimu Baba pekee. Utuweke huru na kiburi chochote, ili tusiangukie kwenye dhambi ya Shetani. Daima utusaidie, ili tuweze kutukuza jina la Baba wa mbinguni, na tuweze kupokea kwa kuamini ndani yako maisha ya milele.
Swali:
- Kwa nini Wayahudi walitaka kumpiga kwa mawe Yesu?