Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 008 (The fullness of God in Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

3. Ukamilifu wa Mungu ulitokea katika kuzaliwa kwa Kristo mwilini (Yohana 1:14-18)


YOHANA 1:14
14 „Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.“

Kristo Yesu ni nani? Yeye ni Mungu kweli na mwanadamu kweli. Mwijilisti Yohana atuonyesha siri hii kuu kama msingi wa injili yake. Wakati alipotaja kuzaliwa kwa Kristo kupitia Neno la Mungu, anatuonyesha msingi wa ujumbe wake. Aya hii ya 14 ndiyo maneno ya ufunguo wa ujumbe wote unaofuata. Ikiwa umeelewa uthamani huu wa kiroho kwa maana yake kamili, ndipo utapata kutambua kina cha maana ya sura hizi zote zinazofuata.

Kuzaliwa kwa Kristo mwilini kimsingi ni tofauti kabisa na kufanywa upya kwa roho zetu. Sisi zote tuna mwili na tumezaliwa na Baba na Mama. Baadaye, neno la injili likatufikia na kuanzisha uzima wa milele ndani yetu. Kristo hakuzaliwa na Baba wa duniani, bali Neno la Mungu lilimjia Mariamu kwa malaika Gabrieli akamwambia: „Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye Juu zitakufunika kama kivuli; hivyo, hicho kitakachozaliwa nawe kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu“.(Luka 1:35) Bikira alipokubali ujumbe huu wa ajabu kwa imani, alitambua mtoto ameumbwa ndani ya tumbo lake, ambaye Roho Mtakatifu aliunganika na damu ya mwanadamu.Hivyo ndivyo Mungu alivyopata kuwa mtu.

Mafikiria yetu yanafikia mwisho mbele ya ukweli huu. Biologia haiwezi kufafanua siri hii. Ujuzi wa mwanadamu hauwezi kuelewa mwujiza huu. Baadhi ya wasomi wa theologia wanajaribu kurahisisha mwujiza huu usiowezekana kiakili kwa Kristo kuzaliwa hivyo, wakisema kwamba, Yesu alitokea tu ndani ya mwili wa kibinadamu bila kuwa mwanadamu kweli asikiaye maumivu na huzuni. Sisi lakini, tunakiri kwamba, Kristo alikuwa mwanadamu kamili na pia Mungu kamili kwa wakati moja.

Kuingia mwilini, au ndani ya nyama yetu kwa Kristo ndio maelezo kamili na bora kwa kuzaliwa kwake kwa ajabu. Mwana wa milele wa Mungu aliyetokana na Baba kabla ya ulimwengu kuwepo, akachukua umbo na maisha yetu bila kufanya dhambi, kwa sababu Roho Mtakatifu ndani yake alishinda tamaa zote za dhambi za kila aina. Hivyo Kristo alikuwa mtu pekee aliyeishi maisha matakatifu, masafi, bila lawama.

Mwana wa Mungu aliungana na waasi, wasiojali na watu wabaya ambao wote walikufa. Ila yeye ni wa milele, hawezi kufa, kwa sababu yeye ni Mungu. Hata ingawa ameinuliwa sana, alifanya yote kutupenda, akaacha utukufu wake na kuishi pamoja nasi wanadamu kwa unyenyekevu. Akawa mmoja wetu na kuelewa hali yetu vizuri kwa kila namna. Katika uchungu wake alijifunza kuwa mtiifu kabisa. Katika njia hii alipata kuwa mwenye huruma kwelikweli. Hakutukataa sisi tulio wabaya. Kristo alifanyika mwanadamu, ili kutukaribia kabisa na kutuvuta karibu na Mungu.

Mwili wa Kristo, yaani kanisa lake, sasa limewekwa badala ya hema ya kuabudia katika Agano la Kale ambapo Mungu alikuwa anakutana na watu wake. Ndipo Mungu akawa ndani ya Kristo na kujieleza mwenyewe kwa watu akiwa mmojawao. Uungu wote ulikuwa ndani ya Kristo akiwa mwilini na kuweza kuguswa na kushikwa na mikono yetu. Kufuatana na maandishi ya kigireki, Yohana alisisitiza kusema kwamba, „ amepiga hema katikati yetu“. Hii ina maana, hakujenga makao ya kudumu, ili akae nasi hapa duniani daima, bali aishi nasi katika hema kwa muda, kama kabila ya Bedouins jangwani kwa muda mfupi ndipo kuendelea mbele. Hivyo wanashusha hema zao chini na kuhamia mahali pengine. Kwa njia hiyo Kristo alikuwa kati yetu kwa muda mfupi kabla ya kurundi mbinguni kwa Baba yake.

Mitume wanashuhudia kwa pamoja kwamba waliona utukufu wa Kristo.Ushuhuda wao ulikuwa ni tangazo lenye vigelegele vya furaha. Wao ni wa ushuhuda, ambao waliona kuwepo kwake Mwana wa Adamu aliye Mwana wa Mungu akiwa na nyama yetu. Imani yao ilifungua macho yao, ili waelewe upendo, uvumilivu, unyenyekevu, utii na utukufu waYesu. Katika utakatifu wake walimona Mungu mwenyewe. Usemi „UTUKUFU WAKE“ katika Agano la Kale inaonyesha jumla ya sifa zake zote za Uungu. Mtume Yohana anathubutu kuthibitisha sifa hizo zote za Yesu wazi katika ushuhuda wake juu yake. Alipata kuelewa enzi yake iliyofichwa ndani yake akiwa mwilini, na pia uzuri wake na ukumbwa.

Akifundishwa na Roho Mtakatifu, Yohana alimwita Mungu „Baba“ na Yesu „Mwana“.Hakuna njia ya kuepuka kwa majina haya. Julisho la Roho inaondoa kitambaa ambacho kinaficha jina la Mungu, likitudhihirishia kwamba, Mtakatifu wa milele, Mwumbaji mwenye enzi ndiye Baba, tena anaye Mwana aliye mtakatifu sawa na yeye, Mtukufu na wa milele naye amejaa upendo. Mungu si hakimu wa kutisha au kulipiza kisasi kwa nguvu. Yeye ndiye Baba wa huruma, mpole na mvumilivu, naye Mwana wake yuko vilevile. Mwenye kumfahamu Baba na Mwana, anafikia kiini cha Agano Jipya. Mwenye kumwona Mwana naye amwona Baba. Ufunuo huu umebadilisha kabisa ufahamu juu ya Mungu unavyoonekana katika dini zingine na kutufungulia macho kwa nyakati na uongozi wa UPENDO.

Unataka kumjua Mungu? Basi endelea kusoma maisha ya Kristo! Ni nini wanafunzi wake walichoona kwake Yesu? Ushuhuda wao kwa ufupi unasema nini? Waliona upendo wa Mungu ukiwa umeunganishwa na neema na kweli. Fikiria maana hizi tatu wakati unapoendelea kuomba na utasikia ujazo wa utukufu wa Mungu ndani ya Kristo. Alikuja kwa rehema ya uponyanyi kwetu tusiostahili. Sisi zote tumekuwa na hatia, hakuna mmoja wetu anayekamilika. Kuja kwake kwetu sisi tulio wafanya rushwa, kunatamka rehema juu yetu. Yesu hasikii aibu kutuita „ndugu“, ametuosha dhambi, kututakasa na kutufanya upya, na ametujalia Roho yake. Matendo hayo ya ajabu je, si majilio ya „Neema juu ya neema“? Na zaidi ya hayo yote: Tumejaliwa, bila kustahili, haki mpya. Kwa sababu Kristo alitupanda ndani ya neema yake, ili tuwe na haki kuitwa „Watoto wa Mungu“.

Ujumbe wa neema sio udanganyifu au ndoto tu, bali ni haki mpya. Kristo kufanyika mwili ndiyo thibitisho la kazi ya Mungu, linalotukamilisha ndani ya wokovu wake. N e e m a ndiyo msingi wa imani yetu.

SALA: Tunainama mbele zako mtoto wa horini kama vile walivyofanya wachungaji na mamajusi kule Bethlemu. Wewe ni Mungu ambaye kwa mwili wa binadamu ulikuja kwetu bila kuona haya kutuita ndugu zako. Nuru yako inang’aa gizani. Takasa mioyo yetu, ili kwamba ifae kuwa hori ya milele kwa ajili yako. Pamoja na waumini wote tunakutukuza, kwa sababu utukufu wako ukakubali kuwa mwili mnyenyekevu Twakusihi kwa ajili ya watu wengi wa eneo letu walio na hali mbaya waweze kutambua haki yao mpya na wakupokee wakikuamini wewe. Amina

SWALI:

  1. Maana ya kufanyika mwili kwa Kristo ni nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)