Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 007 (The Baptist prepares the way of Christ)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

2. Mbatizaji anatengeneza njia ya Kristo (Yohana 1:6-13)


Yohana 1: 11-13
11 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu; ndio wale waliaminio jina lake. 13 Waliozaliwa, si kwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

Watu wa Agano la Kale walikuwa watu wa Mungu kwa sababu mwenyewe alijifunga na watu hao wenye dhambi kwa njia ya agano baada ya kuwatakasa. Aliwaongoza kwa mamia ya miaka. Alilima roho zao kwa jembe la sheria na kuwaandaa wawe wapanzi wa injili. Kwa njia hiyo, historia ya ukoo wa Ibrahimu iliongozwa kutazamia kuja kwake Kristo. Kutokea kwake ilikuwa shabaha na maana ya Agano la Kale.

Ni jambo la kushangaza kwamba, wale walioteuliwa kumkaribisha Bwana Yesu walimkataa wala hawakupokea mwangaza wake. Walipendelea kukaa katika giza la sheria, wakielelekea hukumu. Hivyo walikosa neema kabisa na kupenda shughuli zao kuliko wokovu katika Kristo. Hawakutubu bali walijifanya wagumu dhidi ya roho wa kweli.

Si watu wa Agano la Kale tu waliokuwa mali ya Mungu, ila wanadamu wote pia kwa kuwa Mwenyezi aliumba kila kitu: mawe, mimea, wanyama na pia binadamu wote. Kwa sababu hii, watu wote duniani wanabeba jukumu sawa kama vile watu wa Agano la Kale. Mwumba wetu na mwenye vyote anataka kuingia ndani ya mioyo yetu na nyumba zetu, - hivyo ni nani atakayemkaribisha? Wewe ni mali ya Mungu. Je, wewe umejiweka chini ya madaraka ya Bwana? Bahati mbaya, siku hizi watu wa nchi nyingi hawako tayari kujifungua kwa nuru ya Kristo.Hawataki mwanga wa upendo wake, ili waweze kushinda ugumu wa giza lao. Kwa njia hiyo, wanamkataa Mwana wa Mungu mara nyingine wakati wetu. Mwanadamu yeyote wa ukoo wa Ibrahimu au wa wanadamu wengine wakifungua mioyo yao kwa Kristo na kujikabidhi mikononi mwa Mwokozi mkuu, huyo mtu atapokea mwujiza wa ajabu. Kwa sababu nuru ya mbinguni itamwangazia kwa nuru ya kufurahisha na kushinda giza, ambayo inakaa ndani ya roho yake. Pia nguvu ya Mungu itaingia moyoni mwake na kubadilisha utu wake wa ndani.

Kristo atakuokoa kutoka kwa utumwa wa dhambi. Atakupeleka kwenye uhuru wa watoto wa Mungu. Kama unampenda Kristo, Roho Mtakatifu atakaa ndani yako na kuanza kazi ya wokovu wake maishani mwako.

Mwinjilisti Yohana hasemi kwamba tutakuwa au tumekwisha kuwa watoto wa Mungu, lakini tutakuwa watoto wake tunapoendelea kukua kiroho. Tunaona tofauti kubwa sana ndani ya maneno hayo, maana yule amwaminiye Kristo ataingia katika hali mpya ya kuishi. Wakati huo pia atakuwa katika hali ya maendeleo kiroho kwa kuelekea ukamilifu katika maisha yake ya kiroho. Uweza wa Bwana ulituumba kuwa kiumbe kipya na nguvu yake hiyo itatutakasa na kutukamilisha.

Hatukuweza kuwa watoto wa Mungu kwa hali ya kuchaguliwa kuwa mtoto, ila tumekuwa watoto kwa kuzaliwa kwa upya kiroho.Kushuka kwa uwezo wa Roho ya Kristo ndani ya mioyo yetu inamaanisha kuwa tumejazwa nguvu ya Bwana. Kumiminiwa enzi hii tukufu ndani ya waumini inathibitisha jambo hili kwamba, hakuna nguvu katika ulimwengu huu hadi mwisho wa maisha yao itakayoweza kuzuia kukamilika kwa maisha ya kumtukuza Mungu kwa matendo mema. Kristo ndiye mwanzilishi wa imani na atakayeikamilisha.

Watoto wa Mungu na watoto wa dunia hii hawawezi kulinganishwa wao kwa wao.Tulizaliwa na wazazi wawili ambao walitupata kufuatana na mpango wao au kwa makusudi yao. Labda waliomba pamoja wakitafuta mwongozo wa roho. Lakini uroho wote, mawazo yetu au tabia ambazo tulirithi kutoka kwa wazazi wetu hazina ushirika na kuzaliwa kwa upya katika roho kutoka kwa Mungu. Kwa vile kufanywa upya kiroho ni jambo takatifu tangu mwanzo na inatoka kwa Mungu, ambaye toka kwake kila Mkristo amezaliwa moja kwa moja. Maana ndiye Baba yetu kiroho kweli kabisa.

Hakuna mtoto awezaye kujizaa mwenyewe. Anazaliwa na mtu mwingine, mama yake. Hivyo hata kuzaliwa kwetu kiroho ni neema tupu. Kristo mwenyewe huweka mbegu ya injili yake ndani ya mioyo yetu. Yeyote apendaye mbegu hii, ndiye atakayeipokea na kuitunza na kuikuza. Ndani yake uhai wa milele toka kwa Mungu itaota na kukua. Biblia inasema. “abarikiwe yeye asikiaye Neno la Mungu na kulitunza moyoni” (Luk.11:28)

Kuzaliwa ndani ya jamii ya kikristo na kushirikishwa na wakristo wengine haitufanyi kuwa watoto wa Mungu, ila ni kwa imani katika jina la Kristo tu. Imani hii inamaanisha kuja karibu naye, kujizamisha ndani ya sifa zake, kutambua utulivu wake na kukua katika nguvu zake. Ukuaji huu wa kiroho unaendelea wakati tunapojikabidhi mikononi mwake, kuamini kwamba ametuokoa na kutubadilisha tulingane na sifa zake. Imani katika Kristo ni ushirikiano kati yetu ya yeye, unaosikika moyoni, na pia ni Agano la milele naye. Kuzaliwa kiroho hivyo haitakamilika peke yake ndani yetu, ila kwa imani tu. Tutaweza kusema: Kuzaliwa upya si zaidi au ngumu kuliko imani, kama vile imani haipungui au kuwa rahisi kuliko kubalishwa maisha kuwa mapya. Yote hayo yanalingana.

Mwinjilisti Yohana hakutaja katika injili yake jina “Yesu Kristo” kabla ya kufikia kwa andiko hili. (Mstari wa 14) Badala yake alieleza tabia za Yesu kwa waumini wasio wayahudi, akitumia maneno yaliyokaribia vile walivyowaza kwa mazingira yao. Wewe je, umeelewa hizo maana sita hayo yatokayo na tabia za Kristo, ambayo mwinjilisti aliyaleta mbele ya kanisa lake aliyeliandikia? Umefungua moyo wako kwa uwezo huo wa sifa zake Kristo na kuinama kwa unyenyekevu mbele zao? Kama ni hivyo, basi utakuwa mtoto wa Mungu kweli.

SALA: Ee Bwana Yesu Kristo, ninainama mbele zako na kukupenda na kufungua roho yangu kwako. Unakuja kwangu iwapo mimi ni mwenye dhambi. Unanitakatasa maovu yangu yote, na unakubali kukaa nami kupitia kwa Roho Mtakatifu. Ee Bwana, nimefungua wazi milango ya roho yangu kwako.

SWALI:

  1. Ni yapi yanayowapata wale wanaomkubali Yesu Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)