Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 009 (The fullness of God in Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

3. Ukamilifu wa Mungu ulitokea katika kuzaliwa kwa Kristo mwilini (Yohana 1:14-18)


YOHANA 1:15-16
15 „Yohana alimshudia, akapaza sauti yake akasema: Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba: Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu, kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tumepokea neema juu ya neema“.

Mbatizaji alitangaza kwa sauti kwamba Kristo, ambaye atakuja nyuma yake, alikuwepo akiishi kabla yake, na hivyo kushinda mbali uzazi wowote wa muda. Kwa kuleta ujumbe huu Mbatizaji alitetea umilele wake Kristo. Alitoa ushuhuda kwa ukweli kwamba, yeye yuko juu ya anga, juu ya wakati na jehanamu, tena yu bila mwisho na Mungu asiyeweza kupokea rushwa.

Jangwani mbatizaji alihuzunika kwa vile watu wamejaa dhambi nyingi. Aliwafundisha juu ya toba iletayo ondoleo la dhambi. Bali alipomwona Kristo moyo wake uliruka kwa furaha, kwa sababu alizaliwa kuwa mtu asiyeweza kufa, aliyejaa ukweli, hata kifo asiwe na uwezo juu yake. Furaha ya kuzaliwa kwa Kristo na kusherekea sikukuu hii ina chanzo chake katika ujio wa Mungu na maisha ya milele ndani ya mwili wa binanadamu. Haya yalianzisha ushindi wa uhai juu ya kifo, kwa sababu ndani ya kifo chake dhambi ilifutwa kabisa, ambayo ndio sababu ya kifo.

Alipogundua kina cha neema hii, Mbatizaji alimwinua Mungu na kumtukuza kwa ukamilifu aliokuwa akiionna ndani ya Kristo. Paulo baadaye alikiri: „Ndani yake yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa“ (Wakol. 2:9).

Yohana alijumlisha ujumbe huu wa kweli katika tamko lake kuu. „Katika utimilifu wake sisi sote tumepokea neema juu ya neema.“ Utimilifu huu wa Kristo ni nini, na jambo gani tumepata toka kwake? Ukikumbuka maelezo yaYohana juu ya utu wa Kristo katika vifungu 14 tuliosoma, utajua ukuu wa utu wake na kuelewa jinsi ziwa la neema yake linavyotufikia siku hadi siku.

Kristo ndiye Neno la Mungu kutokana na Baba, kama vile maneno yanatoka katika vinywa vya wanadamu. Yeye ndiye kilindi cha ndani cha moyo wa Mungu na mapenzi yake, shabaha na kufurahisha kwetu. Neno la injili linavyotufikia, kutuingilia akili zetu na kubadilisha makusudi yetu, Kristo naye anaingilia mioyo yetu na kutubadilisha tufanane na utukufu wake. Je, hii si neema ya kushinda kupita kiasi?

Kristo ndiye Uhai wa Mungu tunaoweza kutambua. Wataalamu waweza kujenga nyumba, madaraja, pia na bomu ya kuharibu kubwa sana, lakini hakuna awezaye kuumba uhai. Sisi wazazi tumekabidhiwa kuendeleza kwa watoto wetu uhai ambao Mungu alitupa. Hii si neema ya kupendeza? Na kwa sababu uhai wa duniani ni ya muda tu, Kristo anawavisha waumini wake Roho yake mwenye uhai wa milele. Wakristo wote hushiriki uhai wa Mungu na hawatakufa na kuishi daima. Je, hii si neema ya kushangaza?

Kristo ndiye nuru ya ulimwengu. Yeye ni mshindi juu ya giza na mwumbaji wa nuru katika usiku wenye giza nene. Anatoa tumaini kwa ulimwengu ambao umejaa huzuni, anatuma nguvu kwa ulimwengu ambao unahenya katika kulemewa. Nuru ya Kristo ina uwezo wa kufurisha uchafu wa dunia yetu kwa mwangaza wake. Yeye anatoa ukweli na uadhilifu kwenye siasa na makampuni, katika familia na makanisa, iwapo watu wamwamini. Eti, hii si neema juu ya neema?

Kristo ndiye aliyeumba mbingu nchi. Ndani yake kunakaa utimilifu wa nguvu za Mungu. Miujiza yake ni dhihirisho ya mamlaka yake. Kufufuka kwake kutoka kwa wafu inathibitisha nguvu za uhai ya kushinda kifo. Mwilini mwake alishinda nguvu ya mvuto wa ardhi alipotembelea juu ya maji ya ziwa Galilaya. Alimega mkate mdogo na kuwalisha watu elfu tano wanaume hadi wote wakatosheka. Pia anazijua hesabu za nywele za kichwa chako. Ni wakati gani ambapo utainama mbele ya neema yake inayotujalia?.

Unahitaji kujua zaidi juu ya utimilifu wa Kristo? Yeye ndiye mwenye dunia yote. Vitu vyote vizuri na vya utajiri, dakika zote za maisha yako na hata nafsi yako ni mali yake. Alikuumba na ni yeye anayekulinda. Kristo anamiliki yote. Alikukabidhi utajiri wake mkononi mwako, ili upate kuyatunza kwa niaba yake. Misuli yako, uwezo wa akili yako na pia wazazi wako ni kipawa cha Mungu wako ambayo amekujalia. Lini utamshukuru kwa neema zake hizo zote?.

Jambo la kushangaza kuhusu kuingia kwake mwilini na kuzaliwa kwake Bethlehemu ni kwamba utimilifu na ukuu wa Uungu ulifanyika nyama ndani ya mtoto mchanga. Nabii Isaya alitabiri juu ya mwujiza huu miaka mia saba kabla ya kutimia, alipojaliwa na nguvu za Roho Mtakatifu akisema: “Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume. Na uwezo wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani” (Isaya 9:6). Kwa huzuni tunasema, mawazo ya wanadamu yanasita kupokea haraka kwamba, Mungu katika Kristo amerudisha kwa mwanadamu mfano wake safi, ule aliyokuwa nayo wakati wa mwanzo alipoumbwa. Yesu ndiye mwenye utukufu na mwenye hekima, ndiye anayetupa mashauri ya kutumulikia juu ya Mungu mwenye enzi za milele. Vipawa na uwezo wote wa Mungu zilikuwemo ndani ya mtoto horini. Umepata kutambua rehema ya ajabu kwamba Mungu alikuja kwetu kwa njia ya Yesu? Sasa tunaweza kusema: Mungu yu pamoja nasi.

Kristo hahitaji kushika uwezo wake kwa ajili yake binafsi, maana kama si hivyo angekaa mbinguni. Baali amekuja duniani mwetu akauvaa mwili wetu wa nyama na pia kuchukua maumbile yetu madhaifu ili atufungulie njia ya kwenda mbinguni, kutupatanisha na Baba yake na kutujaza na utimilifu wake. Vilevile Paulo anashuhudia kwamba, shabaha ya Mungu ni kuwepo kwa ukamilifu wake ndani ya Kanisa. Soma Waefeso 1:23; 4:10 na Wakolosai 2:10 ndipo utachukuliwa ndani ya mvuto wa sifa za Mungu na kuelekezwa kutukuza neema ya Bwana wako. Usikae katika hali ya huzuni katika dhambi zako, lakini fungua moyo wako kwa ukamilifu wa Kristo. Njoo kwake mtoto wa hori na baraka mbalimbali zitamiminika juu yako. Atakufanya kuwa chemchemi ya neema kwa wale unaoishi nao.

SALA: Bwana Yesu Kristo, wewe u Mwana wa Mungu. Upendo wote, nguvu na ukweli ziko ndani yako. Tunainama mbele zako na kufurahi kwa sababu wewe hukai mbali nasi lakini umeishi kati yetu. Wewe unatupenda sana. Ulifanyika mtu na kutuokoa. Tunakushukuru kwa kutujalia neema juu ya neema.

SWALI:

  1. Ni nini maana ya ukamilifu wa Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)