Previous Lesson -- Next Lesson
a. Shtaki dhidi ya dai ya Kristo kuwa mfalme (Yohana 18 : 28-38)
Yohana 18:28-32
„Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka. Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyo? Wakajibu wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa.“
Baadhi ya Wayahudi walifikiri kumwua Yesu mapema wakati alipomponya yule mlemavu kwenye birika la Bethzatha (Yoh.5:18), ingawa wengi wa viongozi wa Wayahudi waliamua kisiri kwamba, lazima afe baada ya kumfufua Lazaro (Yoh.11:46)
Kwenye Alhamisi usiku vikao viwili muhimu vya baraza lao viliendeshwa, ambavyo Yohana hakuvitaja (Mathayo 26:57-67 na 27:1). Mambo hayo madogo ya kiyahudi hayakuwa na maana zaidi kwa wasomaji Wayunani, lakini Yohana akakazia tamko lisilokuwa haki dhidi ya Yesu, iliyotamkwa na msimamizi wa sheria ya Kirumi, yaani Pilato, pale Praitorio, ambayo ni makao makuu ya jeshi lao, ambapo mtu aweza kuangalia eneo lote la hekalu. Yeye peke yake alikuwa na uwezo wa kuamua hukumu au kusamehe.
Wale Wayahudi waliokuwa wamemtambua Yesu kuwa Bwana wao, walirudi nyuma kwa hofu ya fujo, ikiwa wataingia ndani ya nyumba ya kimataifa. Walitaka kulinda usafi wao wa kidini, ili waweze kushiriki katika kula Pasaka pamoja na jamaa zao, lakini kwa kufanya hivyo walimpiga Mwana Kondoo wa Mungu wa kweli.
Kwa muda huo wa ukatili, Yesu alipopata kufungwa, mabadiliko makali yakatukia maishani mwa Pilato. Mmoja wa jamaa zake wa kiutawala, ambaye ni mkuu wa jeshi la Kirumi, alifukuzwa na Kaisari kwa sababu ya kubuni maasi, Yule mkuu alikuwa kinyume cha Wayahudi, na maasi hayo yalifichuliwa na Wayahudi. Tokeo hilo nalo kwa Pilato ilikuwa kutingisha utawala wake; dharau lake kwao na namna ya kuwatendea kwa ukali yalipungua.
Baada ya Wayahudi kumleta Yesu mbele za Pilato, huyu alitoka nje kwa haraka wamwone, na kuwaulizia haja zao. Hakutumia muda zaidi kujadili nao, lakini alielewa maana ya malalamiko yao. Mtazamo wa Pilato kwake Yesu ilijionyesha kwa kicheko cha upande - Mfalme bila silaha wala askari, hali ameingia Yerusalemu kwa kupanda punda, basi hawezi kuwa hatari kwa Rumi. Lakini alikubalia na madai ya Wayahudi, akiruhusu makusudi yao.
Tayari alikuwa ameweka jemadari kwa ajili yao pamoja na kikosi, akisaidia shughuli ya kumkamata Yesu. Makusudi hayo yakafaulu: Sasa mfungwa huyu yupo mbele zake amtendee atakavyo. Hata hivyo Pilato akauliza: „Ametenda nini inayostahili hukumu?“
Wazee wa Wayahudi wakaeleza kinaganaga: Wewe wafahamu yale tuliyoyasema juu yake mapema. Mtu huyu ni mvunja sheria wa kisiasa mwenye shabaha ya ukaidi. Hatuhitaji kuongeza zaidi. Hatukufika kwako kwa kukutembelea tu na kukueleza habari ya watu wayahudi, hapana. Tumekuja kudai kifo chake, ili watu wasipate kuvurugwa.
Pilato alifahamu habari ya nia zao na namna ya kusingizia kwao, pia alielewa kwamba mashitaka yao yalihusika na sheria zao, pia na matazamio yao ya Masihi mwenye enzi. Yesu hakusema wala kutenda lolote la kuvunja sheria ya kirumi. Hivyo basi akamkabidhi Yesu tena kwao, ili wamhukumu kufuata na sheria zao wenyewe.
Wakati huo basi Wayahudi hawakuwa na haki ya kumpiga mtu kwa mawe, aliyekuwa amevunja sheria ya kidini. Walielekea kumdhilisha Yesu kwa kesi ya hadharani mkononi mwa Warumi, waliohesabiwa kuwa wanajisi. Hivyo adhabu kali kabisa zilizotumika kwa watumwa na wakosaji wakubwa zingemwangukia na yeye - kuinuliwa juu ya „mti mlaaniwa“. Hilo basi lingefunua kwamba, Yesu siye Mwana wa Mungu, aliye Mwenye Enzi na Haki, lakini alivyojionyesha kuwa mdhaifu na mnajisi. Kayafa alimkusudia afie msalabani kwa mikono ya Warumi ili kuthibitisha kwamba yeye siye Masihi, bali ni mla riba na mdanganyi.
Yohana 18:33-36
„Basi Pilato akaingia tena ndani ya praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.“
Askari wakampeleka Yesu ndani ya jengo. Pilato alipokuwa amesikia mashitaka ya Wayahudi, alitaka pia kusikia mateteo yake Yesu kwa mdomo wake. Pilato hakuamini yale „blabla“ ya Wayahudi tu, lakini alitaka kuendesha kesi kwa haki na akamwuliza Kristo, „Wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi? Nimewaona wa-masihi wengine wakiwa wenye silaha tupu hadi kwenye meno, wenye ndevu nyeusi na macho ya kukodolea. Wewe sio mpigaji au mwenye fujo. Unaonekana kama mtu mwenye taabu, mdhaifu na mnyenyekevu, unawezaje kutamani mambo ya kifalme? Mfalme anatakiwa kuwa na amri, nguvu na ujeuri.”
Yesu alisikia kwamba Pilato alikuwa na mashaka juu ya dai lake kuwa na ufalme akamwuliza, “Je, askari zako walikueleza kwamba wanafunzi wangu walipigana nao kwa usiku, au wachongezi wako walinisikia nikitamka hotuba za kisiasa, au swali lako linategemea tu uongo za Wayahudi? Mtawala hatakiwi kusikiliza tu mashitaka ya uongo.”
Kwa kuchokozwa Pilato akamwitikia, “Je,mimi ni Myahudi?” Kana kwamba kusema, „Mimi sitajishusha kwenye daraja la hao washupavu watundu, wakihoji habari ya vipengele vya kidini usiku na mchana“.
Basi Pilato akakiri kwamba sio yeye aliyemfunga Yesu, lakini watu wa kiyahudi, viongozi wao na wenye kutetea taifa lao. Ndipo akauliza kifupi, „Umefanya nini? Nahitaji jibu toka kwako ili kuwakabili wanaokushitaki. Sema, au utapigwa; sema kweli yote.“
Hapo Yesu alikiri ukweli wote kwa namna ambayo hakutumia hata kwa wanafunzi wake. Akasema, „Ufalme wa Mungu ni wake mwenyewe, haikujengwa juu ya ushuru au silaha au shughuli za kuwanyonya wengine.“ Ufalma wa Kristo haitapotea kama zingine. Yesu hakuwafundisha wafuasi wake kutumia upanga, au silaha za moto au kutupia ma-bomu. Ufalme wake ni tofauti kabisa na falme zote za kidunia.
Yohana 18:37-38
„Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. Pilato akamwambia , Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake.”
Pilato hakutambua maana ya madai ya Yesu, lakini alielewa kwamba mstakiwa alikiri kwamba ni Mfalme bila kueleza zaidi maana ya ufalme ule. Yesu akaitika, “Wewe umetambua siri yangu na kuelewa maneno yangu. Mfalme ni mwenye ufalme akiitawala; Lakini ufalme wangu sio wa ulimwengu huu uliojaa uongo na hila; maana mimi ni Mfalme wa Kweli.”
Ndipo Yesu alishuhudia kwamba kuzaliwa kwake na Bikira Mariamu haikuwa mwanzo wa kuwepo kwake, bali alikuja ndani ya ulimwengu wetu kutoka kwenye ulimwengu mwingine. Kwamba alitokana na Baba kabla ya millennium zetu. Afahamu kweli tukufu. Yesu akashuhudia ukweli wa Mungu. Akiwa mwenye kutokana na Mungu, yeye ndiye shahidi mwaminifu. Lakini Pilato akacheka na kuuliza, „Ukweli ni nini?“ Mtwala huyu aliwahi kuona unafiki na udanganyifu nyingi mno, hata akapoteza imani yake ndani ya ukweli. Lakini Yesu akiwa shahidi mwaminifu wa kweli za mbinguni akasimama imara na kulifunulia jina la Baba yake.
Sala: Bwana Yesu, wewe ndiwe Mfalme wangu; mimi ni mali yako. Unifanye kabisa niwe mtumwa wa utulivu wako; unitunze imara ndani ya kweli yako.
Swali 112: Jinsi gani Yesu ni Mfalme na kwa maana gani ?