Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 024 (The cross)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
C - Kristo kutembelea mara ya kwanza mji wa Yerusalemu (Yohana 2:13 - 4:54) -- Neno Kuu: Kuabudu kwa kweli ni nini?
2. Yesu anaongea na Nikodemo (Yohana 2:23 – 3:21)

c) Msalaba, njia ya kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:14–16)


YOHANA 3:14-16
14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa. 15 Ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Yesu aliendelea kumfundisha Nikodemo na kumhakikishia kwamba, kuzaliwa mara ya mpili hakamiliki bila kuungama kwa ukweli, kubadilika kimawazo na imani katika kifo cha Kristo kwa niaba ya mwanadamu. Mambo hayo ya msingi Yesu alieleza wazi kwa Nikodemo kwa kumkumbusha jambo lililotendeka katika historia ya Waisraeli:

Wale waliposafiri katika jangwa la Sinai walimnug’unukia Mungu na kuasi mwongozo wake (Hesabu 21:4-9) Mungu alituma nyoka za moto ili kuwauma na hivyo kuadhibu kutomwamini kwao; basi nambari kubwa wakafa kwa njia hiyo.

Wakati ule baadhi ya watu walitambua dhambi zao. wakamsihi Musa awaombee kwa Mungu ili awaondolee ghadhabu yake. Mungu akamwagiza Musa atengeneze nyoka ya shaba kama ishara ya hukumu ya Mungu. Alama hii aliinua juu ya watu, ili kuwaonyesha kwamba ghadhabu ya Mungu imefikia mwisho. Matokeo yake yakawa hivi: Yeyote aliyetazama alama ile na kutambua huo mwisho wa hukumu kwa kuamini neema ya Mungu, akaponywa na sumu ya nyoka za moto.

Tangu wakati wa kujaribiwa kwa Hawa, nyoka amekuwa mfano wa maovu. Yesu alipokuja alichukua dhambi za binadamu. Hivyo Yeye aliyekuwa bila dhambi, akawa dhambi kwa ajili yetu. Yesu ni kama yule nyoka ya shaba jangwani, ambayo ilikuwa bila sumu, na hivyo Yesu hakuwa na dhambi kabisa, wakati akijitwisha dhambi zetu.

Mwana wa Mungu hakutokea duniani katika hali ya kung’aa, lakini katika unyenyekevu kama mwanadamu wa kawaida, akiwa na majeraha na uchungu na kujitwisha laana ya sheria. Akiwa kama sisi aliweza kufa kwa niaba yetu. Jina la “Mwana wa Adamu” alijiita mwenyewe. Kama vile kuinuliwa kwa nyoka, ikadhihirisha kuondolewa kwa ghadhabu ya Mungu, hivyo kusulibiwa kwa Kristo kulikuwa mfano wa kutuondolea ghadhabu tuliostahili. Dhambi zetu zote ziliwekwa juu ya huyu Mwana, ili kutuweka huru kupitia mateso yake.

Wakati ule jangwani yeyote aliyeangalia nyoka iliyoinuliwa na kuamini ahadi za Mungu alikuwa ameponywa kutokana na kuumwa na nyoka. Tumaini katika alama ile ya rehema iliwahakikishia uzima na kushinda walioamini. Hivyo yeyote anayetazama Msalaba na kumshika yule aliyesulibiwa hupokea uzima wa milele. Paulo aliandika: “Nimesulibiwa pamoja na Kristo, lakini niko hai, wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu”. Kifo chake ni changu, kwa hiyo na uhai wake pia. Yeyote anayekubali kifo cha ushindi cha Kristo akimwamini ndiye anayehesabiwa haki na kuishi naye milele. Kifungo hicho nacho chatupatia ushirikiano katika ufufuo wake.

Wabovu, hata kutofaa tena, kumtazama Yesu tutakuwa tumeokoka. Yeye anaumba ndani yetu kuzaliwa kwa upya. Hakuna njia nyingine kuja kwa Mungu salama, ila kupitia kwa Msulibiwa. Ndiyo maana Shetani anapigania kwa ukali usiku na mchana mambo haya mawili ya wokovu: Umwana tukufu wa Yesu na kusulibiwa kwake Kristo. Maana katika hayo mawili wokovu wa ulimwengu unasimama.

Mungu ni upendo, neema yake ni kama bahari isiyo na mwisho. Kwa upendo wake hakutupa ulimwengu uliyokufuru, bali anaendelea kutupenda. Hakatai waasi wenye dhambi, lakini amejaa rehema. Sadaka ya Mwanaye imetimiza kamili madai yote ya haki yake kwa ajili ya wokovu wetu. Hakuna wokovu mbali na Mwana!

Ndugu, unaweza toa paundi mia moja hela ya kiingereza, kwa ajili ya rafiki? Unaweza kuwa tayari kwenda gerezani kwa niaba yake? Au hata kufa kwa ajili yake? Labda kama kweli unampenda. Lakini huwezi kama yeye ni adui yako. Hii inadhihirisha upendo mwingi ambao Mungu anao kwetu, katika kumtoa Yesu awe sadaka kwa wakatili kama sisi, ili atuokoe.

Kristo alitimiza wokovu wa ulimwengu msalabani. Sisi sote twahitaji dhabihu ya Yesu. Kabila zote za watu, walio matajiri au maskini, wazuri au wabovu, walioendelea au wasio na elimu, hakuna yeyote ambaye ni mwenye haki ndani yake. Bali Kristo alirejesha ulimwengu kwa Baba yake.

Kiajabu, ukweli huu haupatikani na elimu au akili safi ya mwanadamu, ila wale wanaoamini katika Msulibiwa. Uhusiano wako wa tumaini ndani ya Mwokozi unathibithisha wokovu wako. Bila imani utaendelea kuwa chini ya ghadhabu ya Mungu. Kazi zako zitahesabiwa kuwa bure na chafu katika mwanga wa utakatifu wa Mungu. Nikodemo, mwenye kutii sheria na mwalimu mwema, alipaswa kusikia maneno haya, matamshi yaliyomstusha sana.

Yeyote anayekubali wokovu wa msalaba na kuamini Mwana aliyetundikwa kwenye mti wa aibu atapata kuishi na hatakuwa na kizuizi kati yake na Mungu. Unamshukuru Yesu kwa msamaha huu? Umejitoa maisha yako kwake? Yeyote anayeamini ataishi. Anayedumu ndani ya Kristo amepokea uzima wa milele, hatakufa kabisa. Anayeendelea kumtazama Kristo, atapokea tumaini la uzima wa milele. Imani inatuhakikishia uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Ukipata kutambua undani wa maana yake katika aya ya 14 hadi 16 utagundua kiini cha injili ikijumlishwa pamoja.

SALA: Mungu wa mbinguni, tunakuabudu kwa ajili ya upendo wako usio na kikomo. Ulimtoa Mwana wako wa pekee, ili afe kwa niaba yetu. Alibeba dhambi na hukumu zetu na kutukinga na ghadhabu yako. Tunangalia msalaba, tukitumaminina kuabudu na shukrani jina lako. Ulifuta makosa yetu na kupatanisha ulimwengu na wewe mwenyewe. Utusaidie ili tuwambie wengine kuhusu ujumbe huu, ili nao wapate uzima wa milele kupitia kwa ushuhuda wetu.

SWALI:

  1. Ni jinsi gani Kristo anafanana na nyoka ile ya shaba jangwani?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:55 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)