Previous Lesson -- Next Lesson
d) Kumkataa Kristo kunaleta hukumu (Yohana 3:17-21)
YOHANA 3:17-21
17 „Maana Mungu hakumtuma Mwanawe ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndio hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru, kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. 21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu“
Mbatizaji alihubiri kuhusu Masihi ambaye atahukumu wanadamu, akikata miti iliyo migonjwa ndani ya taifa lake. LakiniYesu alimwambia Nikodemo kwamba yeye hatachoma kwa moto, lakini amekuja kuokoa. Mwokozi wetu ni mwenye huruma. Wakati Mbatizaji alipogundua siri ya malipo ya ushindi kwa ajili ya dhambi, alimwita Yesu Mwana Kondoo wa Mungu.
Katika upendo wake Mungu akamtuma mwanawe si kwa Wayahudi pekee bali kwa dunia yote. Tamko „dunia“ limepatikana mara tatu katika aya ya 17. Hii ilikuwa ni mshangao kwa Wayahudi, ambao waliwachukua wasiotahiriwa kuwa kama maumbwa. Lakini Mungu anawapenda wote wa mataifa nao, sawasawa kama watu wa mbegu za Ibrahimu. Wote wanastahili hukumu, lakini Yesu hakuja kuhukumu, bali kuokoa. Tangu mwanzo alitimiza mfano wa nyoka jangwani, alipoinuliwa msalabani mwenyewe, ili kuchukua hukumu ya Mungu badala ya binadamu. Upendo wa Mungu si wa ubaguzi wowote, lakini unajumlisha wanadamu wote.
Ndipo Kristo alitumia msemo wa kushitusha akisema: „Yeyote atakayeamini katika Mwana hatahukumiwa“. Hivyo hofu yoyote kuhusu siku ya hukumu imetupwa mbali. Na imani katika Kristo yatuweka huru kutoka kifoni, ambacho penginepo tungestahili kuipata. Wewe je, umewekwa huru kutoka kwa hukumu ukiwa unamtegemea Yesu tu.
Wale ambao wanakataa wokovu wa Kristo, wakifikiri kwamba hawana haja nayo, wako vipofu, wajinga, na kutengwa na neema ambayo yu tayari kuwapatia. Wale ambao hawakaribishi nguvu ya Kristo, wamebaki nje ya miale ya nuru ya Roho Mtakatifu. Yeye anayedharau kifo cha Kristo au kuikataa, anamwasi Mungu na kuchagua namna ya kujipatia haki mwenyewe. Lakini kazi zetu zote hazifai na tutapungikiwa na utukufu wa Mungu tunapojitegemea wenyewe.
Yesu anaeleza, kwa nini watu fulani wanakataa wokovu: Wanapenda dhambi kuliko haki ya Mungu yenye rehema, na wanajitenga na Kristo aliye nuru ya ulimwengu. Hivyo wanaendelea kushikamana na dhambi zao. Kristo ajua mioyo yetu na mizizi ya mawazo yetu ya kijahili. Matendo ya watu huwa hayafai kitu. Hakuna aliye mwema kwa uwezo wake. Mawazo yetu, maneno na matendo ni maovu tangu ujana wetu. Maelezo haya yalimstua Nikodemo, hasa wakati Kristo alivyotanguliza kwake hayo na mvuto wa upendo wake, ili kuvunja kiburi chake na kumvuta akubali kuungama.
Yesu akaongeza kwamba, yeyote asiyemtumaini Kristo, basi anapenda uovu na kuchukia mema, na hivyo kuendelea kushikamana na dhambi zake. Wingi wa watu ni wanafiki, wakificha makosa yao kwa kicheko kitakatifu. Wanamchukia Kristo kwa kutokuelewa au hata kwa makusudi. - Je, wewe umeungama dhambi zako kwake Yesu? Usipoungama ukatili wako kwake huwezi kuzaliwa kwa upya. Fungua moyo wako kwa nuru ya Mungu na uoshwe. Ndipo imani ndani ya Mwana Kondoo wa Mungu inakutakasa. Kwa hiyo nyenyekea na upate kuungama ongo wako, ukamtumaini Kristo tu, na kwa njia hii utapata kuishi milele.
Kuwa mwenye imani yenye matendo, inamaanisha kufanya mema. Utayari wa kukubali ukweli wa Mungu ndio hali ya kufanyika upya. Atakayepokea ukweli wa Kristo si kiakili tu, lakini kwa nafsi yake yote, atabadilishwa katika tabia yake. Waongo watakuwa wenye kuongea kweli. Walio kombo wanafanyika wanyoofu, wabaya wanabadilika kuwa wenye kuaminika. Wale ambao wamezaliwa mara ya pili hawakuwa wazuri kabla ya hapo, lakini waliungama dhambi zao na Mungu aliye mwaminifu akawasamehe. Utakaso umeanza kwao, ndipo Yesu huwapa nguvu za upendo, ili wafanye kazi za Roho yake.
Hatukatai matendo mema, lakini hayo hayatoki kwetu, bali ni toka kwa Mungu. Sifa si zetu, ni kwa neema yake tu yanatendeka. Inamaanisha kwamba tunaachana na kujidai haki za binafsi yenye msingi wa bidii ya kujisifu mwenyewe. Tanafungua utu wetu kwa haki ya neema inayotegemea damu ya Kristo tu. Wote waliozaliwa mara yapili na kudumu ndani ya Kristo wanampendeza na Mungu. Maisha yao yamekuwa ya shukrani kwa neema yake. Kuzaliwa kwa upya na maisha ya utakaso yanakuwa ibada ya kumpendeza Mungu sana.
SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa kubeba hukumu yetu na kwa ajili ya ulimwengu. Tunakwinamia kwa sababu hatutapata hukumu, kwa vile tumeunganika nawe katika imani. Umetuweka huru na ghadhabu ya Mungu. Tunaungama dhambi zetu mbele zako. Utuoshe na tamaa za kutaka kufanya dhambi, bali tuishi na furaha bila hofu. Tuumbie ndani yetu matunda ya Roho, ili maisha yetu yaonyeshe kukutukuza wewe na shukrani kwa Mungu, Baba wa mbinguni.
SWALI:
- Kwa nini waumini wa Kristo hawatapita kwenye hukumu?