Previous Lesson -- Next Lesson
b) Haja ya kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:1-13)
YOHANA 3:6-8
6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa na Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho”.
Yesu alimwonyesha Nikodemo umuhimu kwa yeyote abadilishwe kabisa kabisa. Ugeuzi huu ni kuu jinsi ilivyo tofauti kati ya mwili na Roho. Neno “mwili” katika Agano Jipya inamaanisha utu wa asili ulioanguka dhambini na kutengwa na Mungu, mwendo mwovu wa kuelekea kifoni. Neno hili halimaanishi mwili wa kawaida tu, bali mawazo na roho za waasi. Hii ndio hali ya ubovu kamili, kama vile Yesu alivyosema ”Katika moyo kunatoka mawazo maovu.” Hakuna mtu anayestahili kuingia Ufalme wa Mungu. Mtu ni mbaya tangu kuzaliwa na anakuwa chanzo cha uchafu.
Neno “Roho” inasimamia Roho Mtakatifu wa Mungu mwenyewe, aliyejaa ukweli, usafi, nguvu na upendo. Mungu hamdharau mwenye dhambi, lakini ameshinda namna ya mwili kwa njia ya Kristo.Hii inaonyesha shabaha ya kuzaliwa mara ya pili. Roho akiwa ndani yetu inakomesha tamaa za mwili, ili tuishi inavyostahili kwa wito tulioitiwa. - Je, umezaliwa mara ya pili na kuwekwa huru kutokana na kulemewa na nguvu za giza katika mwili?
Kwa mara ya tatu Yesu aliongea na Nikodemo kwa upole na kumwambia, “Wewe na wajumbe wote wa baraza, nyote mlio mbegu ya Ibrahimu mnahitaji kuzaliwa kwa upya”. Hii ni jambo la lazima, ni wajibu takatifu. - Tunakushuhudia, ndugu, kwamba neno hili lililosisitizwa na Kristo “ni lazima”, basi inakuagiza ufanye! Bila kufanyika upya kabisa huwezi kumjua Mungu wala hutaingia katika ufalme wake.
Umesikia mwendo wa upepo? Waliozaliwa mara ya pili ni kama upepo unapoanza kuvuma. Inaonekana kwamba upepo unatokea mahali pasipojulikana na kurudi huko huko. Ni hivyo pia kwa watoto wa Mungu, wamezaliwa kutoka juu na kurudi kwa Baba yao. Sauti ya upepo inadhihirisha kuwepo kwa upepo. Alama ya wazi kwa watu waliozaliwa upya ndio sauti ya Roho Mtakatifu ikisema kupitia kwao. Hatuongei tu kwa sauti za watu wa kawaida ambazo zinatoka katika mawazo yao. Roho Mtakatifu anakuja kwetu toka nje ya dunia hii kama sauti ya nguvu za Mungu kwa mwumini. Je, amekushukia moyoni mwako?
YOHANA 3:9-13
9 “Nikodemo akajibu, akamwambia, yawezaje kuwa mambo haya? 10 Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli na mambo haya huyafahamu? 11 Amin,amin nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. 12 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa Adamu.”
Katika maelezo ya Kristo, Nikodemo alisikia sauti ya Roho Mtakatifu. Moyo wake uliitikia mvuto wa huyu Mtukufu. Lakini mawazo yake hayakuelewa, wala hakutambua ukweli kwa kina chake.Akanong’oneza, “Sijui jinsi gani kuzaliwa hivyo inawezekanaje.” Kukiri hivyo ilikuwa ni kukubali wazi kushindwa kwake. Ndipo Yesu aliendelea kumpatia uongozi: “Ndiyo, wewe ni mwalimu anayeheshimiwa, umekuja kwangu, wakati wengine walijisikia kuwa wenye akili na juu zaidi, wasio na sababu ya kuongea nami. Wewe unawazidi, hata hivyo na wewe hujui sana kusudi la Roho Mtakatifu. Kuomba kwako na sadaka na juhudi zako za kutimiza sheria ni bure. Hujaelewa miongozo ya msingi ya Ufalme wa Mungu.”
Mara ya tatu Yesu alitumia maneno muhimu sana. “Amin, amin nakuambia”. kwa kila mara kwa maneno haya Yesu alikuwa anatangaza mafunuo mapya. Anayatumia hivyo kwa sababu mawazo yetu ya kibinanadamu hayashiki kwa urahisi.
Ni nini hatua mpya ambalo Nikodemo alijifunza? Kristo aliendelea kutumia badala ya neno la “Mimi”, sasa akatumia “Sisi”, na kwa njia hii kujiunga na sauti ya Roho na hivyo kuwa wawili. Hata hivyo Kristo ni mmoja pamoja na Mungu kama Neno lake lililoingia mwilini. Yesu alifundisha ukweli huu, ambao si wote wanaolitambua. Alishuhudia mambo ambayo alifunuliwa kwa kushirikiana na Roho. Nasi tunatakiwa kukubali ushuhuda huu tukiishika kabisa na kuiamini.
Ni nini ambalo Yesu alilijua kuliko watu wote? Alimjua Mungu na kumwita “Baba”. Maajabu haya hayakuweza kuwaingia hao viongozi, ambao walijiamini kuelewa bora, tena bila kujazwa Roho. Kristo alitoka kwa Baba na kurudi kwake tena - alishuka toka mbinguni na kupaa tena. Kutengana kwa Mungu na mwanadamu ilifikia mwisho wakati Roho wa Mungu alifanyika mwili ndani ya Yesu; hivyo matengano hayo yakaisha. Mwenye Umilele hayuko mbali tena, wala si wa kutisha, bali yu karibu naye yu mpole. Kiajabu, watu hawakuelewa ushuhuda huu kuhusu ukweli wa Mungu. Hawakutambua ule umoja kati ya yule aliyezaliwa kwa Roho na Baba yake. Kwa sababu walikataa kuamini, wala kukiri makosa yao. Walishindwa kutambua haja ya kuzaliwa mara ya pili, bali walijidanganya kwamba wao ni wazuri na waerevu sana. Wangetambua kwamba kujitosheleza haiwezi kuwafanya waelewe ule umoja wa Utatu Utakatifu.
SALA: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tunakuabudu; katika uhakika wa upendo wako umetufanya kuwa wapya na kutufanya tuwe watoto wa ukweli wako. Twaomba, Roho wako wa ukweli uvume juu ya taifa letu, ili wengi wapate kuokolewa, na ushuhuda kuhusu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu uenee kwa umbali na upana, tena upate kuwa wazi katika lugha zetu za asili, ili wengi wapate kuokolewa.
SWALI:
- Ni nini dalili za kuzaliwa mara ya pili ndani ya waumini?