Previous Lesson -- Next Lesson
3. Wanafunzi sita wa kwanza (Yohana 1:35-51)
YOHANA 1:35-39
35 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama na wanafunzi wake wawili. 36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema “Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka akawaona wakimfuata, akawambia “Mnatafuta nini?” Wakamwambia, “Rabbi”(maana yake, mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.”
Kristo ni Neno la Mungu katika mwili, uungu kamili, ndio chanzo cha uhai na asili ya nuru. Hivi ndivyo mwinjilisti amemweleza Kristo kwa asili yake. Pia ameeleza huduma ya Yesu na kazi zake. Yeye ndiye Muumba na Mhifadhi wa vyote. Naye ametupatia ufahamu mpya wa Mungu, akiwa Baba mwenye rehema anayetujali. Hivyo anarudia “Tazama, MwanaKondoo wa Mungu”, ili kujumlisha yote yanayohusiana na Yesu na shabaha yake. Katika kifungu cha 14 alielezea kiini cha Kristo na asili yake, ndipo kifungu cha 29 na 33 inaeleza lengo la kuja kwake Yesu na huduma yake.
Kristo akawa mwanadamu, ili aangamizwe na mauti kuwa kafara kwa Mungu, aliyemtoa mwanae ili abebe dhambi zetu na atuokoe kutoka kwa hukumu. Mungu alitamani dhabiu hii akaitoa kuwa baraka na pia kibali mbele zake. Kufuatana na maneno ya mtume Paulo “Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiipatanisha dunia na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.”
Sio rahisi kwa kizazi chetu kuelewa tamko hili “Mwana-Kondoo wa Mungu”, kwa vile hatuchinji wanyama kwa kuondolewa dhambi zetu. Mtaalamu fulani wa mfumo wa utoaji wa sadaka za kuchinja wa Agano la Kale anatambua huu msemo ya kwamba hakuna ondoleo la dhambi bila umwagaji wa damu. Tunashangaa kwamba, Mungu hakutuadhibu kwa ajili ya dhambi zetu kwa kumwaga damu yetu, ila akamtoa Mwana wake kwa ajili ya kusudihili. Mtakatifu alikufa kwa ajili ya waasi kama sisi. Mwana wa Mungu alifia dhambi za wenye hatia, ili wafanywe wana wenye haki wa Baba wa mbinguni. Haya, tumtukuze YEYE na tumwinue pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu, YEYE aliyetukomboa.
Wanafunzi wale wawili nao hawakutambua kwa haraka kina na maana ya tamko hili “Mwana-Kondoo wa Mungu”. Lakini walipoona namna ambavyo Mbatizaji alimtazama Mwana-Kondoo wa Mungu, wao nao walitamani kumfahamu Yesu, aliyetazamiwa kuwa Bwana, hakimu wa dunia na vile vile dhabiu kwa ajili ya binadamu. Mawazo kama haya yalitawala akili ya hao wawili walipokuwa wakisikiliza kwa makini. Yesu hakuwachukua wanafunzi wa Yohana, ila mwenyewe aliwaelekeza kwa Yesu. Ndipo hao wanafunzi walikubaliana na ufuasi huu mpya.
Yesu alitambua kutamani kwao, pia akaelewa lengo lao. Waliona ndani ya Yesu upendo na neema na wakasikia matamshi ya kwanza ya Yesu yalivyo katika injili hii, “Mnatafuta nini?”Bwana hakuwamwagia maneno magumu, bali aliwapa nafasi ya kusema mafikira yao.Kwa hiyo, unatafuta nini, ndugu? Ni nini lengo la maisha yako? Unamhitaji Yesu? Utamfuata Mwana-Kondoo?Jifunza makuu yaliyo kweli, (“the greatest truths”) kwa maisha yako ya kiroho, kuliko kwa ajili ya mitiani yako ya shule tu.
Wanafunzi hawa wawili walimwomba Yesu awakubali waende naye kwake. Maswali ndani ya mioyo yao yalikuwa ya maana kuliko majadiliano barabarani ambapo misukosuko ya umati wa watu ingewasumbua. Hapo Yesu aliwajibu “Njoni mwone”. Hakusema “Mje msome kwangu”, lakini “Funbueni macho yenu na mtaona nafsi yangu ya kweli, matendo na mamlaka yangu, na mtatambua sura mpya ya Mungu.” - Yeyote atakayemkaribia Yesu atapokea ufunuo mpya wa dunia na atamwona Mungu alivyo. Ufunuo wa Yesu utapinduaufahamu wa akili zetu kuhusu ulimwengu. Yeye atakuwa nuru ya mafikira na shabaha ya matumaini yetu. Kwa hiyo, njoo uone na wewe, jinsi wale wawili walivyofanya na kukiri na mitume kwa wakati wake, “Tumeuona utukufu wake kama Mwana wa pekee wa Mungu aliyejaa neema na kweli”
Wanafunzi hawa walikaa na Yesu siku nzima. Vipi yanavyopendezamasaa kama haya ya neema ya kukaa naye! Mwinjilisti alishuhudia juu ya saa moja ya siku ile yenye baraka ya kukata shauri ya maisha yake. Hii ilikuwa ni saa tatu. Hapo ndipo Yohana mwinjilisti alitambua ukweli wa Yesu kupitia kwa uongozi wa Roho.Maana hapo Bwana alikubali imani yake na akamjalia haki na uhakika ya kwamba Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa. – Je, nuru ya Yesu imeangaza ndani ya giza la roho yako? Unamfuata wakati wowote?.
SALA: Tunakutukuza na kukuinua wewe Mwana-Kondoo wa Mungu uliye takatifu.Umeondoa kabisa dhambi za ulimwengu, ukitupatanisha na Mungu. Usitukatae, bali tukufuate wewe tu. Tusamehe makosa yetu, tufunulie enzi yako,ili tukutumikie kwa kujitoa kabisa.
SWALI:
- Kwa nini wanafunzi wale wawili waliamua kumfuata Yesu?