Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 015 (Testimonies of the Baptist to Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

2. Ushuhuda zingine za Mbatizaji za kuvutia sana, za kumhusu Kristo (Yohana 1:29-34)


YOHANA 1:31-34
31 “Wala mimi sikumjua, lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nilikuja nikibatiza kwa maji. 32 Tena Yohana alishuuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni naye akakaa juu yake. 33 Wala mimi sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka nibatize kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34 Nami nimeona, tena nimeshuuhudia ya kuwa huyo ni Mwana wa Mungu”.

Mungu alimwita Mbatizaji akiwa na umri wa miaka thelathini, ili kutengeneza njia ya Kristo na kumjulisha kwa watu. Haya yalijitokeza wakati wa ubatizo wake na kuwafanya watu wajirudi na kujiweka tayari kumkaribisha Kristo. Mungu alimwambia Mbatizaji akimahidi kwamba, ataona mambo, ambayo hakuona mtu kabla yake – kushuhudia jinsi Roho Mtakatifu alivyoshuka juu ya Kristo. Itambulikane kwamba, Roho alitulia juu ya Yesu. Manabii wa Agano la Kale walijazwa kwa muda fulani kwa huduma ya pekee, lakini Kristo alijazwa moja kwa moja. Kama chemchemi kisichokoma kutoa maji, huyu Roho atawajaza na waumini na nguvu tukufu ya Mungu.

Hao wanaume wawili walisimama kando ya mto Yordani; mbingu ilifunguka polepole, ndipo kwa ghafla Yohana aliona Roho Mtakatifu kama njiwa nyeupe katika anga ya blue, akiwa alama ya amani na upole.

Roho haikumtelemkia mwingine ila Yesu tu na kutulia juu yake, ili kumhakikishia kwamba, kijana huyu Mnazareti ni mkuu kuliko manabii wote na viumbe vyote. Mbatizaji alitambua kwamba, Mungu amesimama mbele zake, yule wa Milele aliyetazamiwa.

Bila shaka mbatizaji alijawa na shukrani na furaha, kama wakati aliporukauka tumboni mwa mama yake, wakati wa kutembelewa na Mariamu, ambaye naye alisisimuka kwa furaha na shukrani (Luka 1:36-45).

Mbatizaji alimtambua Kristo kuwa mgawaji wa Roho, wala hakufisha maono hayo, bali kwa uwazi alidhihirisha akilia: “Bwana amekuja! Yupo pamoja nasi, si kwa kuhukumu, bali kwa kuonyesha upendo na ushirikiano. Yeye si mtu wa kawaida, bali Mwana wa Mungu, aliyejawa na Roho. Yeyote anayeamini kwamba Yesu ni Roho kutoka kwa Mungu, anakiri pia kwamba, yeye ni Mwana wa Mungu”. Hivyo Yohana aliweka wazi shabaha ya kuja kwake Kristo: Kuwabatiza kwa Roho Mtakatifu waliotubu. Mungu ni Roho, Mwanaye ni Roho wa Mungu ambaye amefanyika mwili. Ni furaha yake kuwajaza wafuasi wake na ukweli wake tukufu kwamba: Mungu ni upendo.

Ndugu mpendwa, wewe umejazwa na Roho Mtakatifu? Umewahi kutambua nguvu za Mungu ndani ya maisha yako? Sifa hii bora itakuwa yako wakati utakapoacha dhambi kwa njia ya imani katika Kristo aliyejitoa dhabihu kwa ajili yako. Anayekubali msamaha huu kutokana na Mwana Kondoo wa Mungu atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu. Mwana wa Mungu yu tayari kumgawia kila atakayeamini vipawa vyake vya kiroho.

SALA: Ewe Mwana Mtakatifu wa Mungu, tunakuabudu na kukupa sifa. Ulinyenyekea kwa sababu yetu na kubeba dhambi zetu. Tunakushukuru kwa msamaha wa dhambi zetu kupitia damu yako pale msalabani. Tunakushukuru pia kwa vile tumepewa nguvu za Roho Mtakatifu sisi na wote wanaokupenda. Uwaamshe wengi kutoka usingizi wao wa dhambi na maovu yao. Wafanye kuwa wapya na uwajaze na ukweli wako wenye upole.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu alipata kuwa mwenye kugawa Roho Mtakatifu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)