Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 017 (The first six disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

3. Wanafunzi sita wa kwanza (Yohana 1:35-51)


YOHANA 1:40-42
40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41 Huyu akamwona kwanza Simioni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, “Tumemwona Masihi”(maana yake Kristo). 42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema “Wewe u Simoni, mwana wa Yohana, nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

Andrea nduguye Petro alikuwa mvuvi kutoka Bethsaida, mji wa ufuoni mwa ziwa Tiberia. Alikuja kwa Mbatizaji, ili atubu dhambi zake na angojee kuja kwa Masihi. Anderea alikubali ushuhuda wa Mbatizaji, ndipo akamfuata Yesu. Moyo wake ulijaa na furaha, alishindwa kuhifadhi alichoona ndani yake tu, lakini akamtafuta nduguye kwanza kuliko wageni. Hivyo Andrea, kaka yake, kwa kumpata ndugu yake mwenye shughuli sana, alimtolea haraka habari njema kwa kusema. ”Tumemwona aliyeahidiwa, Kristo na Mwokozi, aliye Bwana na Mwana-Kondoo wa Mungu”. Petro labda alikuwa na shaka, lakini Andrea akamshawishi. Hatimaye Petero akaungana naye na akamwendea Yesu akiwa amechanganyikiwa bado.

Petro alipoingia kwenye nyumba, YEYE alimwita kwa jina. Yesu alihoji mawazo yake kwa kumpatia jina mpya “Mwamba”. Yesu alielewa yote kuhusu mambo ya Petro wa kale, ya wakati huu na ya wakati ujao, huyu aliyekuwa na uzoefu wa kutokujali.Yesu alijua mioyo iliyokuwa wazi kwake. Petro akaelewa na akavutika kimakini na Yesu alivyomwangalia. Yesu alianza polepole kumgeuza mvuvi wa samaki mwenye uhodari kuwa “Mwamba” imara. Ndani ya Kristo baadaye akawa msingi kwa ajili ya kanisa lake. Hivyo kwa namna fulani Andrea akawa mwanafunzi mwanzilishi.

Mwanafunzi mwingine naye akatumika kama chombo kwa kumwongoza nduguye kwa Yesu. Yohana alimwongoza Yakobo nduguye kwake Yesu, ingawa majina hayo mawiliameyaficha ndani ya injili yake, kama ishara ya adabu. Kwa hakika Anderea na Yohana walikuwa wanafunzi wawili wa kwanza kwa mfuatano wa wakati.

Uzuri wa vifungu hivi vya utangulizi uko katika mfano wa jua linapokucha(“the analogy with sunrise”) – kucha kwa muda maalum.Waumini hao hawakuwa na uchoyo, bali walileta ndugu zao kwa Kristo. Kwa wakati huu hawakwenda kwenye njia kuu na sokoni, ili kutangaza Injili,bali walishughulikia jamaa zao na wakawaleta kwa Kristo. Hawakukimbilia kwa wale wenye mashaka au wanasiasa, lakini walitafuta wale waliokuwa na njaa ya neno la Mungu, waliovunjika moyo na waliotamani kutubu.

Kwa hiyo tunajifunza namna ya kupitisha habari njema ya neema sio kwa nguvu za haraka, bali kwa furaha inaotokana na ushirikiano na Yesu. Wanafunzi hawa wa mwanzoni hawakuanzisha shule ya theologia, wala hawakuandika mambo ya kuhusu maisha yao, lakini walishuhudia kwa maneno ya midomo yao na yale waliyoyaona kwake. Walimwona Yesu na kumsikia wakamshika mkono na kumwamini. Ushirikiano huo wa moyoni ilikuwa chanzo cha mamlaka yao. – Je, umewahi kukutana na Yesu kwa njia ya injili yake? Umewahi kuwaleta marafiki zako polepole na ukiwa umewashawishi kuja kwake?

SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa furaha uliotia mioyoni mwetu. Utuendeshe kwa utamu wa ushirikiano wako, ili tulete wengine kwako. Tupe uwezo wa kuwaeleza Injili wengine kwa upendo. Utusamehe woga wetu na kuona haya,tusaidie ili tushuhudie jina lako kwa ujasiri.

SWALI:

  1. Ni kwa njia gani wanafunzi wa kwanza walitangaza jina la Yesu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)