Previous Lesson -- Next Lesson
3. Mungu anadumu kuwa mwenye haki, hata kama sehemu kubwa ya Waisraeli (Warumi 9:6-29)
Paulo alikuwa ni mtume mwenye furaha katika huduma yake kwa ajili ya Bwana Yesu, lakini pamoja na hayo alikuwa amezama ndani ya huzuni kuu na kujisikia anazidi kusongwa. Aliwaona mamia ya watu wa mataifa bila imani waliopata kuwa watu wapya na kuingizwa katika ufalme wa Mungu, wakati ambapo maelfu ya Wayahudi waliochaguliwa walimkataa Yesu na ufalme wake, wakiendelea kwenda mbali naye na bila kutaka kumsikiliza wala kumfuata.
a) Ahadi za Mungu hazihusiki na mbegu za asili za Ibrahimu (Warumi 9:6-13)
WARUMI 9:6-13
"6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. 7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; 8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao. 9 Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. 10 Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, 11 kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye, 12 aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. 13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia“
Paulo, mtaalamu halali, alihitaji kuweka wazi ukweli huu, ambao ulikuwa geni kwa wote wawili, kwa Wayahudi na kwa Wakristo wa asili ya kiyahudi kule Rumi. Aliwaandikia kwamba, neno la Mungu ndiyo ukweli wa pekee unaoweza kuweka wazi maendeleo hayo mageni, nalo linabeba jibu lililo kweli kwa siri hiyo. Jibu hilo lakini lina mambo mawili:
Kwanza: Sio watoto wote wa Ibrahimu ni watoto wa ile ahadi. Mungu hakumchagua Ismaeli kuwa mmoja wa mababu wa Kristo. Ismaeli na uzao wake wote waliendelea nje ya mfululizo wa dini, pia na nje ya chaguo la watoto wa Yakobo. - Tunajifunza kutoka kwa maendeleo hayo kwamba, habari ya mbegu ya asili ya mtu haiamui juu ya hali yake ya kiroho katika maisha yake ya mbeleni. Si kila mmoja aliyezaliwa ndani ya familia ya Kikristo kisiri atapata kuwa Mkristo wa kweli, lakini bado atahitaji yeye binafsi kumrudia Mungu. Mungu anao watoto, wala hana wajukuu. Ukweli huo unatuwekea wazi kwamba, si wote katika Wayahudi waliochaguliwa tangu awali ni watoto wa Mungu, lakini ni wale tu, ambao kwa kutaka kwao wanakuwa wazi kwa Injili ya Kristo. Haki ya Ibrahimu ya kupokea watoto (wa kiroho) imetendeka kwao, lakini tendo hilo linategemea mapenzi ya kila mtu binafsi.
Pili: Twasoma katika Biblia Takatifu kwamba, Bwana alikuwa amemwambia Rebeka, mkewe Isaka kabla hajawazaa mapacha yake kwamba, mkubwa atamtumikia mdogo wake (Mwanzo 25:23). Wote wawili walikuwa ni wana wa baba mmoja. Lakini Mungu alijua kabla ya hapo kwamba, chembechembe na vile vinavyotokeza namna ya mtu, vitakuwa tofauti ndani ya kila mmojawao.
Hivyo basi, Mungu alimchagua Yakobo, yule mdogo, na akamkataa mkubwa, yaani Esau. Ingawa Yakobo hakuwa bora kwa tabia yake kuliko Esau, alifurahia uwezo ule wa kuamini zaidi kuliko Esau, na pia aliungama kwa moyo. Biblia halitaji sifa hizo ndani ya Easu. Hali hiyo inatueleza kwamba, chaguo la mtu, kufuatana na kuamriwa mbele, inategemea uwezo wa Mungu wa kufahamu yote, pia na mapenzi yake.
Hakuna awezaye kumlaumu Mungu kwa ajili ya kumkataa, kwa sababu hatuzifahamu siri zetu za utu wetu, wala yote yaliyomo ndani ya miili yetu (hasa kwenye ubongo wetu). Mungu ni mtakatifu, mwenye haki, na bila lawama katika maamuzi yake.
Baadhi ya wana-theologia wanaona kwamba, uchaguzi wa Mungu hauhusiki na hali ya maisha ya mtu, wala matendo yake, lakini inategemea tu uamuzi wa Mwumbaji. Pia kwamba, mwanadamu hawezi kugundua azimio na makusudi ya Mungu. Si kila mtu anayekubaliana na msimamo huo, maana Mungu wetu ndiye Baba, ambaye si mtakatifu tu, lakini pia ni wa kupenda na mwenye huruma mno.
Wakati wa huduma yake Yesu alitamka maneno hayo yaliyo dhahiri: „Kondoo zangu husikia sauti yangu, nami nawafahamu, nao wananifuata. Nami nawapa uzima wa milele“ (Yohana 10: 27-28). Si kila mtu asikiaye sauti yake, wala si kila mmoja asikiaye sauti yake atamwitikia, au kutenda kufuatana na maagizo yake. Tutakuta watu wa ukoo moja, tena wa taifa moja, hata wa familia moja, wanaosikia injili na hawaielewi, wakati wengine wao wanajazwa na ujumbe huo kwa furaha na amani.
SALA: Ee baba wa mbinguni, tunakushukuru kwa sababu uliwachagua Isaka na Yakobo ukawafanya kuwa mababu wa kizazi cha mwana wako Yesu, ingawa wao kwa kweli hawakuwa watakatifu. Tunaomba, uimarishe imani yetu kwamba, sisi tuweze kushinda, kwa jina lako, magumu yanayotujia, pia na maovu yaliyomo ndani yetu. Utuongoze tuwe wanyenyekevu na wa kujikinahi, ili tusijihesabu kuwa bora kuliko wengine.
SWALI:
- Maana ya kuchaguliwa kwake Isaka ni nini na ya uzazi wake, pia na kuchaguliwa kwake Yakobo na wana wake?
- Je, siri ya uchaguo wa Mungu ni nini?