Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 052 (God Selects whom He has Mercy on)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 2 - HAKI YA MUNGU HAISOGEI HATA BAADA YA WATOTOWA YAKOBO, WATEULE WAKE, KUFANYA MIGUMU MIOYO YAO (Warumi 9:1-11:36)

3. Mungu anadumu kuwa mwenye haki, hata kama sehemu kubwa ya Waisraeli (Warumi 9:6-29)

b) Mungu humchagua yule, ambaye anamrehemu, na mwingine atakavyo anamtia ugumu (Warumi 9:14-18)


WARUMI 9:14-18
"14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! 15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali ni wa yule arehemuye, yaani Mungu. 17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.“

Kutokana na mafunuo ya Bwana kwake Musa katika kitabu cha Mwanzo 33:19 tunakuta kwamba, Mungu anayo mamlaka kuwa na rehema kwa mtu fulani na kuendelea na hiyo rehema, si kitu kama huyu mtu ametenda dhambi au hapana. Kwa hiyo, uchaguzi wa Mungu hautegemei matendo ya mtu, bali kipekee ni rehema ya Mwenye Enzi; na wokovu wa mtu inamaanisha kumjalia haki bila kustahili kwake, kwa sababu ya neema ya Mungu isiyo na mwisho.

Pia tunasoma kwa maana iyo hiyo katika kitabu cha Kutoka 9:16 kwamba, Bwana aliye mtakatifu alimwambia Farao, mwamuzi, aliyekuwa amejaa mapepo ya Misri: „Lakini nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uwezo wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.“ Tangazo hilo tukufu lilimsukumiza Paulo aandike: „Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.“ (Warumi 9 : 18).

Hayo ni halali kwa sababu ya utakatifu wa Mungu. Hata hivyo, Mungu siye mwenye amri ya ushupavu, bali anatamani watu wote wapate kukombolewa na kufikia ufahamu wa ukweli (Warumi 11:32; 1.Timotheo 2:4 na 2.Petro 3:9 ).

Kama fulani amefungua moyo wake kwa roho zilizo kinyume cha Mungu, au yeye amezaliwa katika familia, au ukoo, au watu wengine, wanaojaa na mawazo kinyume cha Yesu, bado inaeleweka kwamba, Mungu aweza kumruhusu kiongozi aletaye shida, aweze kuwa kinyume cha maagizo yake waziwazi; na Mungu pia aweza kuthibitisha uwezo wake wa milele kwa kumjali mtu wa namna hii anayemkataa.

Kwa kujibu ule mstari uiliotajwa hapo juu utokao katika waraka wa Paulo wapo wanaosema kwamba, Uislamu unakubali wazo kwamba Mungu humpotosha mtu anayemtaka, naye humwongoza mtu amtakaye; maana Mungu, kufuatana na utakatifu wake, anaye haki ya ya kupotosha watu wote, kwa vile hakuna mwenye haki. Lakini basi, kawaida yake Mungu si wa namna hiyo, jinsi dini zingine zinavyosema, maana yeye ni mwenye huruma kwa watu wote, na yeyote anayemkubali Kristo basi anashiriki katika chaguo lake mwenyewe, maana Kristo ndiye wa pekee, ambaye hakutenda dhambi wakati wowote.

Lakini yeyote anayejifungamanisha mwenyewe na ibilisi, aliye baba wa maongo yote, na apendaye fedha zaidi ya Mungu, basi asishangae ikiwa yeye Mtakatifu anamruhusu aanguke kabisa, hata asiweze kuelewa tena neno la Mungu, jinsi Yesu asmavyo katika Injili yake kufuatana na mwinjilisti Yohana (8:43-45). Kweli, Mungu anayo uhuru kufanya maamuzi yake, lakini mwanadamu hushiriki katika wajibu, kwa kutegemea kama ameungama kweli au sio.

Ili kuweka wazi kabisa jambo hilo kwako msomaji, twadokeza kwa mkazo kwamba, Paulo alituma mawazo hayo si kwa watu wa mataifa, lakini kwa Wayahudi kule Rumi, ili ikiwezekana kushinda ugumu wa mioyo yao. Aliwawekea wazi kwamba, Mungu angeweza kuwapotosha, ingawa alikuwa amewachagua, ikiwa wao hawafungui mioyo yao kwa uongozi wake ndani ya Injili ya Kristo. Waraka huu wa Paulo hautolei filosofia fulani kwa yeyote yule, bali inatuonyesha jinsi Mungu anavyoenenda na hali ya ugumu wa mioyo ya hao Wayahudi.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakuabudu kwa sababu umetuchagua sisi wenye dhambi katika uchaguzi wa Yesu Kristo, nawe ulitujalia haki ile ya kupata kukwawa watoto wako, ingawa hatustahili uchaguzi wako. Tunakusifu na kukutukuza kwa ajili ya rehema yako isiyo na mwisho na kukushukuru kwa moyo wetu wote, kwa sababu hukufanya mioyo yetu kuwa migumu au kutukataa, ingawa tumetenda makosa, lakini ulituvuta kwako kwa njia ya upendo wako tukufu unaofurika, asante.

SWALI:

  1. Kwa nini hakuna mtu anayestahili kuchaguliwa na Mungu? Jambo gani basi ni sababu ya kuchaguliwa kwetu?
  2. Kwa nini Mungu alimfanya Farao kuwa ngumu? Jinsi gani ugumu wa mioyo ya watu unajionyesha, ikiwa ni ya mtu mmoja, ya ukoo au ya watu kwa jumla?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 04:30 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)