Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 039 (Man without Christ always Fails before Sin)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

5. Mwanadamu bila Kristo kwa vyovyote anakosa mbele ya dhambi (Warumi 7:14-25)


WARUMI 7:14-25
"14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. 15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. 17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda, ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda, ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, 23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. 24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? 25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.“

Paulo anatuonyesha jinsi mtu wa asili anavyoishi bila Kristo chini ya jinamizi ya kutisha ya sheria. Somo hilo, ambalo ni kilele cha kujitambua mwenyewe, haliweki waziwazi kwa njia za mawazo ya kifilosofia au itikadi fulani, bali anamfunua mtu wa asili kwa kutumia ungamo la binafsi la kushtua sana. Roho Mtakatifu alikuwa amelainisha dhamiri yake ya kitume kiasi cha kumfanya atambue kama amesogea hata kwa sehemu ndogo sana kutoka kwenye mapenzi ya Mungu na kwamba ni jambo la kutisha.

Paulo asema: „Mimi ni wa kimwili kila ninapoangalia uwezo wangu tu. Kila mtu ni wa kimwili, kwa sababu amepoteza sura ya utukufu wa Mungu aliyowahi kujaliwa. Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Wote pamoja wamekuwa waasi, na roho wa sheria inawahukumu ndani ya dhamiri zao kwa ajili ya uchoyo wao wa kujisifu.“ Watakatifu hasa ndiyo wale wanaopoteza tumaini la neno la Mungu, kwa sababu wanasikia tamko hilo: „Uwe mtakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu“, au wanavunjika kwa agizo la Yesu: „uwe mkamilifu, jinsi Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu“. Paulo anakiri kwa maumivu ya rohoni kwamba, mtu wa asili hawezi kutimiza mapenzi ya Mungu kwa nguvu yake mwenyewe. - Jinsi ilivyo taabu kabisa mtu akiri hali ya kutokuweza kwa nguvu yake ya kibinadamu!

Mbali na hayo, kuna hamu kubwa sana ndani ya kila mtu atende mema, na aishi safi na takatifu. Hata watu wa chini kabisa wanao hamu hiyo. Na kwa hiyo, haitupasi kuzungumza tu habari ya dhambi na nguvu yake, wala tusiwe wenye kiburi mbele za watu wengine, bali ni lazima kutambua mabaki ya sheria za Mungu zinazobakia ndani ya akili za wote, kwa vile hakuna aliye mbaya mno kiasi cha kutokutaka kuwa mwema. Ni ya kujutika kwamba, hata yeye anayetamani kuitika kwa hamu hiyo, bado anakosa daima na kutenda kinyume cha mapenzi yake mema, na hivyo kuvuka juu ya sauti ya dhamiri yake. Dhambi iliyo ndani yetu ni yenye nguvu kuliko akili zetu; na sheria ya Mungu inatawala juu ya kila mtu mbali na kusudi lake njema.

Je, kwa nini hatuwezi kuishi safi na kuendelea ndani ya upendo wa Mungu? Kwa sababu mwanadamu bila Mungu anatawaliwa na dhambi. Yeyote atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Uwezekano wa kutenda dhambi unaonekana pia kati ya waumini, wasipolindwa naye Kristo. Miilini mwetu hatuna nguvu ya kutimiza mapenzi ya Mungu. Uamuzi huo unafuatwa na ungamo kuu wa ufilisi wa mwanadamu. Paulo mwenyewe alikiri ukweli huo aliposema, „Mimi najua kwamba ndani yangu (maana yake ndani ya mwili wangu) haiishi lolote jema. Maana yale mema nitakalo kutenda, silitendi;bali lile ovu nisilotaka kutenda, ndilo nalitenda.“ Je, wewe unalikiri jambo hilo pamoja na Paulo na kukiri kwamba wewe ni mtu mhalifu? Je, utakabidhi utu wako uliochafuka kwa neema ya Mhukumu wa milele?

Mtume amwita kila mtu mtumwa wa dhambi, kwa sababu nguvu yake iliendelea kukua kufikia aina ya sheria, ambayo anaiita sheria ya dhambi. Utumwa wetu kwa maovu ikawa kama sheria, na kifungu hiki kikatupatia maumivu, kwa sababu ndani ya akili zetu tunafahamu wajibu wetu na tunataka kuyatenda, lakini hatuwezi. Hii inaleta hali ya kukata tamaa, kwa sababu utu wetu unatikisa mapingu ya gereza ambalo limo, wala haliwezi kutoka. Sisi sote tu wafungwa wa uchoyo wetu. Hata hivyo, Kristo akuita wakati huu kwa jambo kuu la ukamilifu wa Mungu. Je, unatambua ujinga ndani ya kila mtu? Anataka kutenda mema, lakini hawezi peke yake.

Basi, hakuna msaada? Paulo anatuongoza ndani ya uchini wa mwisho wa kutambua uchafu wetu, na anafanya hivyo kutuonyesha kwamba, wokovu haupatikani katika mambo kama haki ya ubinafsi, unyofu wako, uwezo wako, au ndani ya sheria yenyewe, hakuna kabisa. - Sasa, ushuhuda wa mtume umekuweka huru na imani yako ya kiakili tu, na pia imekufukuza kutoka kwa hali ya kinahi kuhusu kila aina ya utu wema? Waalimu ni waongo na wana-filosofia ni wajinga, wakipungukiwa na hekima ya Roho Mtakatifu. Hao hawatambui mipaka yao. Abarikiwe yule mwumini anayefahamu mbele za utakatifu wa Mungu kwamba, yeye ndani yake sio mkweli, ni mwenye dhambi na wa kuharibika. Heri mtu yule ambaye ametambua ukali wa hukumu wa sheria juu ya utu wake uliofungwa, naye aliyepata kuwa huru na maelekeo yote ya kudai haki ya kibinadamu, naye asiyeamini katika ubingwa wa ubinadamu, bali anayemtegemea Kristo pekee.

Ashukuriwe Mungu! Maana Yesu Kristo ndiye Mshindi, ambaye pasipo yeye tumepotea na wenye kujidanganya sawa na wengine wote. Yeye alitupatia ukweli na nguvu mpya. Roho yake Mtakatifu hutujalia uhai na kutufariji, akitupatia na tumaini imara ndani ya Mwokozi wa pekee.

SALA: Ee Baba mtakatifu, tunakuabudu na kukutukuza kwa mioyo yetu yote, kwa sababu hukutuacha katika hali ya kukata tamaa, lakini ulimtuma Mwana wako Kristo kwetu, Mwokozi na Mpatanishi kwa wote, na kwa njia ya haki yake Roho yako aliweza kutufikia. Tunamfungulia akili na utu wetu, ili yeye aweze kufungua gereza la dhambi zetu na kutuweka wakfu kwa huduma takatifu, pamoja na waumini wote katika taifa letu na pia ulimwenguni kote.

SWALI:

  1. Mambo gani Paulo alikiri juu ya nafsi yake, na ungamo hilo linamaanisha nini kwa ajili yetu?

Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili
wangu halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka,
bali kutenda lililo jema sipati.

Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi;
bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

(Warumi 7:18-19)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 16, 2022, at 04:00 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)