Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 038 (The Law Prompts the Sinner to Sin)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

4. Sheria humsukuma mtenda dhambi azidi kutenda dhambi (Warumi 7:7-13)


WARUMI 7:8
"7 Tusemeje basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. 8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa“.

Paulo alisikia rohoni mwake upinzani wa maadui yake: „ Kama umetuweka huru na yale mafunuo makuu na matakatifu, je, unaihesabu sheria kuwa si kamili, dhaifu au si ya kweli?“ Mtume alijumlisha hoja zao zote, ndipo akawauliza kwa swali la kukuza: Je, sheria ni dhambi? Ndipo kujibu mara moja: „Msikubali kwa vyovyote, maana haiwezekani kabisa kwamba, maagizo ya Mungu yawe maovu, maana yanatuonyesha njia kwa uzima.

Tamko lililotafsiriwa „kinyume cha hayo“ inamaanisha „bali“, na kwa kutumia neno hilo litaeleza kwa ukamilifu zaidi maana hilo: „Nakataa kwamba amri ni dhambi. Msimamo wangu haunifikishi hapo; wala siwezi kuthibitisha kwamba, amri ni ovu. Mimi kwa nguvu narudisha lile tamko. Lakini bado nathibitisha hilo kwamba, amri zilikuwa na matokeo katika kuchokoza dhambi. Bila sheria niliishi kwa wasiwasi dhambini, kama mtoto aliyekula bila kutambua matunda yaliyokatazwa kutoka kwa bustani ya jirani. Dhambi inaonekana nzuri na kupendeza mwanzoni. Hii ndiyo hali ya upotovu ya dhambi zetu kwamba, tunafikiria kile kitu kilicho potovu na ovu kuwa ni cha kawaida na safi tu, wakati mengine bora yanaonekana kama geni na ya hatari. (Ndiyo udanganyifu wa dhambi)

WARUMI 7:9-11
"9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. 10 Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. 11 Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua.“

Tunapoamuru jambo, tunasababisha kutokutii moyoni mwa mtu; na hamu ya kuvunja ile amri inazidi kukua kila wakati. Paulo hapo anasema habari zake mwenyewe kuanzia mstari wa 7 anapotumia „Mimi“, kwa sababu alitambua ndani yake mwenyewe kwamba, watu wakiwa bila kuelewa amri, wanajifikiria kuwa na hali safi kabisa, salama sana na tegemeo la wema katika hali yake, kana kwamba ni bila dhambi, na maovu yamekwisha mwilini mwake. Lakini wakati amri za Mungu zilipoletwa maishani mwake, alianza kufahamu na kutambua dhambi zake, naye akasikia rohoni mwake ile agizo la kukataa dhambi, na hata kuifia (kuiacha kabisa). Maana amri inamaanisha Mungu anashambulia ule umimi wa kibinadamu ndani yetu, kwa vile utu wetu wa asili ni tamaa tupu na udadisi. Kila mara na neno na agizo la Mungu linamaanisha kufa kwa ule umimi.

Tena mtume anarudia kutueleza kwamba, hakuna kabisa ufumbuzi mwingine kwa ajili ya ubovu wetu, ila kufia kwa utu wetu wa asili. Kufu hivyo kiroho inafunua ile kweli geni kwamba, sheria inatuonyesha njia ya kwenda uzimani, iwapo inatupeleka kwanza kifoni. Zaidi ya hapo, inatuongoza kujikinahi wenyewe na kwa hukumu ya Mungu dhidi yetu ya kufa na kuharibika.

Paulo anaeleza kwamba, dhambi kwanza ilionekana tamu kama sukari, bali ilimwongoza kwa hatua ya kutokutii dhidi ya utakatifu wa Mungu na sheria zake za asili. Hali amevaa nguo safi ilimpeleka moja kwa moja kuzimuni. Hii ndiyo uongo wa Shetani, pia na kukufuru kwake yeye aliyekuwa mwuaji tangu mwanzo. Kwa maneno yaliyopakwa sukari na mitindo ya kudanganya huwa anatukaribisha mautini.

WARUMI 7:12-13
"12 Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Basi je! 13 Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.“

Paulo, mtaalamu wa sheria, tena Mfarisayo hapo zamani, alisimama katika hali ya hofu mbele ya ukweli kwamba, ufunuo takatifu wa Mungu ndani ya agano la awali haikufanya mema kwa watu, badala yake ilifanya mioyo yao kuwa migumu na kuwachokoza watende maovu. Basi yakiwa hivyo kwamba, zuio linaumba katazo, na lile lililokusudiwa kuwa njema na safi linapeleka mautini. Paulo alilia kwa sauti: „Hapana! Maelezo hayo si kweli. Yale mema yanafunua maovu, na inamvuta mtenda maovu kutafuta kupona na kujibidiisha kupata kuokoka. Hivyo Mungu mara kwa mara huwaruhusu watu kutumbukia ndani ya dhambi, wafuate kabisa tabia zao za asili, ili wapate nafasi kujiona wenyewe na kushitushwa na matokeo ya kuvunja sheria.

SALA: Ee Bwana, katika utakatifu na ukamilifu wako uasi na uchafu wangu zinaonekana sana. Nisamehe hali ya juujuu tu katika uaminifu wangu, na utuondolee kwenye nyuso zetu, kwa ukali wa amri zako, kila mwigo tuliotengeneza kwa unafiki wetu, ili tupate kufahamu na kukiri kwamba, hakuna njia nyingine kwa ajili yetu, ila kukubali kifo chako msalabani mwako na kuendelea ndani ya kifo hiki siku zote, kwa sababu sheria yako inatuhukumu na kutokeza ndani yetu hali ya kutokutii kwa ushupavu. Ee Bwana, najitoa kwako kabisa, ili uweze kuniponya; niokoe na kunitunza katika hali ya kufisha utu wangu wa asili, na niwe katika uhai pamoja nawe.

SWALI:

  1. Ingawa inatufaa, mbona sheria inaweza kuwa sababu ya maovu na kifo kwetu?

Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi!
(Luka 18:13)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:55 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)