Previous Lesson -- Next Lesson
6. Ndani ya Kristo mtu huondolewa dhambi, mauti na hukumu (Warumi 8:1-11)
WARUMI 8:1
"1 Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.“
Katika sura za 5 – 7 mtume Paulo anatuhakikishia hali yetu ya kutokuweza kujiokoa wenyewe kutoka kwa utu wetu wa asili ulio ovu kwa njia ya nguvu zetu sisi wenyewe. Anatuwekea wazi kabisa kwamba, sheria haitusaidii, lakini inachochea ndani yetu ile hamu ya kutenda dhambi, na mwishowe inatuhukumu adhabu. Roho wa mauti inatawala ndani ya miili yetu, na dhambi inakuwa na nguvu juu ya mapenzi yetu mema. Kwa mathibitisho hayo mtume amemvua mtu na uwezo wote wa kujiokoa mwenyewe kwa nguvu zake, pia na kupoteza tumaini lake lisilofaa la kuishi kwa usafi kwa njia ya nguvu zake mwenyewe za kibinadamu, wala si kwa makusudi yake mema ya adabu.
Baada ya thibitisho hilo linalokubalika na wote, mtune atuonyesha njia ya pekee ya maisha na Mungu, kwa mambo anayoyataja katika sura ya 8 kuhusu miongozo ya hayo maisha mapya anapoeleza hali ya kuwa „ndani ya Kristo“.
Mtu ambaye ameunganika na Kristo, sasa anaingia ndani ya mapana ya Mwokozi. Hatembei tena peke yake, au aliyeachwa, mdhaifu, au mwenye makosa, kwa sababu Bwana wake anasindikizana naye, anamlinda, naye anamtunza. Bwana hufanya hivyo, si kwa sababu huyu mwumini ni bora ndani yake, lakini kwa sababu alijikabidhi mwenyewe kwa Mwokozi wake mwenye huruma, aliyemjalia haki na kumtakasa; alimjalia fahari ya upendo na kumtunza daima. Kristo mwenyewe huishi ndani ya mwumini, naye anambadilisha na kumwendeleza kwa ukamilifu wake katika hali yake ya kiroho, ambayo mtume anaiita „kuwa ndani ya Kristo“. Hasemi habari ya kuendelea kanisani daima, lakini anatutaka kuunganika na Kristo na kujizamisha kabisa ndani ya upendo wake.
Imani yetu sio kwamba ina msingi wa kimawazo tu, lakini inaonekana katika matendo matakatifu, kwa sababu Kristo alifanya kiburi chetu kife msalabani, ndipo alitufufua kwa njia ya ufufuo wake tuwe na maisha mapya. Yeyote amwaminiye anaambatana na Bwana wake na anapokea kwake nguvu ya mbinguni. - Maneno hayo siyo filosofia tupu, lakini mamilioni ya waumini wanapata kujua hayo wenyewe, wakimtambua Roho Mtakatifu kwamba anaishi ndani yao. Mungu mwenyewe anakuja, naye anaishi au anakaa ndani yake yule ampokeaye Kristo na ukombozi wake.
Roho Mtakatifu, akiwa mtetezi mtakatifu na wa pekee, hufariji dhamiri yako iliyochanganyikiwa dhidi ya mashitaka ya shetani. Anakuthibitishia, tena katika jina la Mungu mtakatifu kwamba, wewe umepata kuwa na haki ndani ya Kristo, pia umejaliwa kupokea nguvu za mbinguni, ili upate uwezo wa kuishi kwa usafi katikati ya dunia hii ya uchafu. Utawala wa Roho Mtakatifu unabadilisha hali ya mtu, jinsi Paulo anavyoeleza kwenye sura ya 7. Mtu wa namna hii hatabakia katika hali ya kiasili, ya kimwili na mdhaifu, lakini anapata na nguvu, katika uwezo wa Roho Mtakatifu, ya kutenda yale yaliyo mapenzi ya Mungu. Sasa baada ya kutambua wokovu mkuu ndani ya enzi ya Roho, ungamo ule wa Paulo kwamba, yale aliyoyataka kutenda, hakuyatenda, lakini yale aliyoyachukia ndiyo yale ambayo alitenda. Kwa sasa anatenda yale ambayo Mungu anayataka, na moyo wake unafurahia nguvu yake.
Roho huyu anakuhakikishia kwamba, Kristo aliyefufuka na kushangilia pia atakusindikiza kupita katika saa za hukumu. Akubeba pia mikononi mwake katika miali ya moto ya ghadhabu ya Mungu, na kukulinda na mishale ya nuru ya Mtakatifu, maana haitakuwa na lawama kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu.
Pia atakusaidia leo uongoze maisha ya kikristo katika subira ya upendo, furaha ya unyenyekevu, pia na ukweli wa usafi; si kwa sababu unaweza kuumba hali hiyo ndani yako mwenyewe, lakini kwa sababu unaendelea kudumu ndani ya Kristo kama vile tawi la mzabibu linavyodumu ndani ya shina. Ndiyo maana Bwana wako akuambia: „Udumu ndani yangu na mimi ndani yako, ili uweze kubeba matunda mengi“. Loo, jinsi tumaini lako lilivyo la ajabu!
SALA: Ee Mungu mtakatifu, tunakuabudu na kushangilia, kwa sababu umetuokoa kutoka kwa kiburi chetu, ulitukomboa toka kwa mwenendo wetu mchafu, ukatuweka huru na dhambi zetu zote na ukatutakasa na machukizo yetu. Twakusifu kwa sababu ulitubeba hadi kwenye uzima wako na kutuokoa na upendo wako, ili tuweze kutembea kwa utakatifu na kuendelea ndani ya ushirikiano wako daima pamoja na wote walioitwa katika ulimwengu huu.
SWALI:
- Maana ya sentenso ya kwanza katika sura ya 8 ni nini?