Previous Lesson -- Next Lesson
c) Uadilifu (haki) ya Mungu unaimarishwa na kutendeka ndani yetu kwa njia ya imani inayodumu (Warumi 1:16-17)
WARUMI 1:17
"17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.“
Kuna mashaka makubwa katika usomi wa theologia kwamba, ipi ni haki (au uadilifu) wa Mungu. Kama dini yetu ingekuwa kijuujuu, mashaka kama haya yasingetokea. Hata hivyo, tunapojifunza kwamba, utakatifu wa Mungu unadai kwamba, kila mtenda dhambi auawe, na kwamba hakuna aliye mwenye haki mbele za Mungu. Tunapata huzuni, maana binadamu wote tunastahili kufa mara moja. Basi, Mungu ndani yake siye takatifu tu na hakimu atendaye haki, lakini naye ni Baba mwenye huruma, hali amejaa upendo, ufadhili na uvumilivu sana. Asingemharibu mtenda dhambi, bali angependa kumwokoa.
Kutokana na utakatifu wake, Mungu asingeweza kumsamehe yeyote na wakati wowote apendavyo, ingawa anatafuta namna ya kumsamehe kila mtu bure, kwa sababu enzi ya Mungu inaweka mpaka wa hali ya kuwepo kwake.
Kwa suluhu wa tatizo hilo yeye mwenyewe aligundua badilisho la kufaa ndani ya sadaka (au kafara), ambayo inakufa kama badilisho kwa ajili ya (au badala ya) mtenda dhambi. Kwa vile haikupatikana mnyama au sadaka ya kibinadamu iliyoweza kumudu matakwa ya utakatifu wa Mungu, basi alichagua kumtumia Mwanawe hata kabla ya wakati wote kwamba, apate kuingia mwilini katika ukamilifu wa wakati, ndipo afe badala yetu, alipie kwa dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki. Hata hivyo, neno kuu la barua kwa Warumi sio thibitisho kuwa haki sisi wenyewe, lakini haki au uadilifu wa Mungu mwenyewe: Jinsi gani Mwenye Utakatifu ataweza kuwa mwenye haki, mbali na hatua ya kutuweka haki sisi tulio wenye dhambi? Kristo ndiye jibu la pekee kwa swali hilo.
Watu wa sheria ya Agano la Kale walikufuru dhidi ya Msalaba, wakisema: „Ikiwa kila mtu anaweza kupewa haki kwa njia ya imani ndani ya Kristo, basi tuendelee kutenda dhambi zaidi, maana neema ya Msulibiwa inatupatia haki kwa kujienda.“ Paulo aliwalaani hao, na aliwashuhudia kwamba, imani ya kikristo sio namna ya kusadiki tu, lakini ni kuishi pamoja na Kristo, ambapo nguvu yake inatenda kazi katika udhaifu wetu, naye anaumba matunda yake ndani yetu. Kumfuata Yesu inaunganisha mnyororo, ambayo viungo vyake ni vipimo vya imani vinavyojaa shukrani mna upendo kwake Kristo anayetujalia haki, kututakasa na kutukamilisha. Sisi hatuwi wakombozi wenyewe, bali tunafungua mioyo yetu kwa neema ya Mungu. Wale waliowekwa haki wanaishi na imani pekee. Wanaendelea toka imani hadi imani, wala hawajisikii wenyewe kuwa na haki ndani yao. Kristo aliwajalia haki hiyo, naye anawatunza na kuwatakasa siku hadi siku kwa kutenda kazi kwa Roho yake. Kwa njia hiyo Mungu anaendelea kuwa mwenye haki, kwa sababu anatusamehe kila siku na kututakasa kila dakika. Sisi tu mali yake, nasi tu takatifu kwake.
Swali lingine likainuliwa kuhusu watu wa Agano la Kale, waliotia uadilifu wa Mungu kwenye mashaka. Hii ndiyo namna ya Wayahudi ya kukataa neema. Wayahudi walimsulibisha Mwana wa Mungu, na hivyo walikosa kutambua historia ya wokovu wao. Zaidi ya hapo, siku zote walikuwa kinyume cha sauti ya Roho Mtakatifu, aliyejaribu kuwarudisha katika hali ya ungamo na imani. Kwa kuangalia ukweli huo usioweza kupingwa, Paulo na mitume wengine walijiuliza: „Jinsi gani Mungu aliweza kuendelea kuwa mwenye haki, kama aliweza kuchagua ukoo wa Imbrahimu na kujifunganisha nao katika agano la milele? Pamoja na hayo tunaona siku hizi kwamba Mungu anawapa mioyo migumu na kuwakataa, kwa sababu hawakuwa wazi kwa Roho yake Mtakatifu. Je, Mungu aliwakosa?“ – „Hapana“, anajibu Paulo katika barua yake, anapoweka wazi jibu kwa ufunuo huo (katika sura za 9 hadi 11 ya Warumi) si kwa kuwasafisha Wayahudi, lakini kwa ajili ya kukazia uadilifu wa Mungu kwao, kwa maana Mtume wa Mataifa alikuwa na shauku kwa ajili ya uungu, utakatifu na haki za Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Yeyote anayepokea imani ya kweli na kujikabidhi kwenye mwelekeo wa Roho Mtakatifu, huyu atapata kufanywa upya ndani ya ufahamu wake, na ataweza kuishi katika utakatifu pamoja na wote waliowekwa kuwa haki katika Agano Jipya. Maadili ya Kikristo hayakomi kwenye elimu ya watu, au kwenye nguvu za kibinadamu, lakini yanaendelea kwa utiifu wa kuchota kutoka kwa upendo wa Mungu na enzi ya ukombozi wake, unaowabeba wote wanaoamini ndani ya Mwana. Adabu ya Wakristo inatakasa jina la Baba. Ufafanuzi wa haki yake ndiyo jambo kuu na kiini cha waraka kwa Warumi.
SALA: Ee Mungu, Utatu Utakatifu, tunakuabudu kwa sababu ulitukabidhi kwenye imani ya kweli na kutuweka haki bure, nawe unatutakasa kila siku na kutuongoza. Wewe tu ni Mwenye Haki, nawe unaendelea kuwa wa haki, hata hivyo hatuelewi hatua nyingi za watu katika historia ya ulimwengu. Twaomba ututakase kikamilifu, na uondoe dhambi zinazosalia katka tabia zetu, ili tupate kuwa sifa na harufu tamu kati ya watu wote.
SWALI:
- Jinsi gani haki ya Mungu inahusika na imani yetu?