Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 008 (The Righteousness of God)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Ufunguzi Wa Barua: Salamu, Shukrani Kwa Mungu, Na Mkazo „Haki Ya Mungu” Kama Neno Kuu La Barua Hii (Warumi 1: 1 – 17 )

c) Uadilifu (haki) ya Mungu unaimarishwa na kutendeka ndani yetu kwa njia ya imani inayodumu (Warumi 1:16-17)


WARUMI 1:16
"16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uwezo wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.“

Paulo alikuwa akitambua sana kwamba, neno „injili“ lilijulikana na pia lilikuwa na maana ya kufurahisha kule Rumi, maana yalikuwepo injili nyingi, kama vile kutangaza wakati wa furaha kwenye daraja la familia ya watawala, ambazo wenyeji wa mji mkuu walitamani kusikia.

Yeye Paulo alinyanyua wakati wa furaha ya wokovu kwenye daraja lile lile la matangazo ya kitawala, kana kwamba alitaka kusema, „Mimi siionei haya barua yangu hii, inayotoka Palestina, ile koloni ndogo. Kwa maana nyingine naitolea katikati ya mji mkuu, maana nawaletea habari ya wakati wa furaha kwamba, Mungu mmoja anaye Mwana wa pekee, aliyetembea mbele zake tangu milele, na wakati huu aliingia mwili awe karibu nasi katika uungu wake, na kwa ajili ya kuokoa wanadamu wote kwa njia ya kifo chake na kufufuka.

Ndani ya waraka wangu sikuandika mtangazo kwamba, mwana mwenye kufa tena amezaliwa, kwa kaisari aliye wa kufa siku moja, lakini kuna mtangazo wa furaha ya kuzaliwa kwa Mwana wa milele kwa Mungu wa milele. Kama injili za kitawala zilipeleka kwenu habari ya wakati wa furaha kuhusu ushindi wa jeshi la kirumi, au ilitangaza kwenu michezo ya kifalme, au habari ya chakula cha kutosha kwa majeshi ya watu, mimi kwenu nawapelekea Habari Njema kwamba, binadamu wote bila kumwacha hata mmoja wamekombolewa na dhambi, kifo, Shetani, ghadhabu ya Mungu na hukumu. Injili yangu ni kuu kuliko injili zote za kirumi, maana inahusu ulimwengu wote, ni ya juu sana, ya milele, yenye enzi kuu na yenye utukufu. Haikujengwa juu ya filosofia ya kibinadamu, vitabu au matumaini matupu, lakini imekuwa na kiini ya nafsi ya mtu mmoja tu.“

Warumi hawakufahamu maana mbalimbali ya neno „Kristo“ lilivyotajwa na Wayahudi. Walifahamu maana yake kama „aliyetiwa mafuta“, ambalo ni sifa aliyepewa pia Kaisari, ambaye kwa nyongeza ya utendaji wa kawaida, alihesabiwa kuwa ndiye kuhani mkuu. Kaisari alijumlisha nafsini mwake kuwa mtendaji wa kisiasa, kijeshi na ya kisheria pamoja na huduma ya upatanisho wa umati wa watu kwa miungu na roho za kitaifa, kana kwamba yeye ni msuluhishi kwa baraka zote na za amani.

Basi, Kristo ndiye Bwana wa mabwana, ambaye kwake enzi zote zimekabidhiwa mbinguni na duniani, maana yeye ndiye Kuhani Mkuu wa kweli na Mpatanishi pekee na Mwombezi kwa Mungu.

Kwa tamko lake hili mwanzoni mwa injili yake, Paulo hakuweka wazi tu uwana wa Kristo kwake Mungu na asili yake ya kimungu, lakini alieleza wazi pia utendaji wake kama Bwana, Hakimu, Mfalme, Mtawala na Mpatanishi, ambaye yeye pekee anastahili sifa au cheo hiki cha „Mwokozi wa ulimwengu“, ambayo kwa wakati ule ilitajwa kipekee kwa Ma-Kaisari.

Wakati huu wa furaha ya Mwana wa Mungu na huduma zake mbalimbali sio wazo tupu tu. Ni enzi ya kuweza kulipuka, ambayo ni kubwa kuliko enzi zote za dunia, maana injili inajumlisha enzi zote za Mungu. Bwana mwenyewe yupo ndani ya injili! Anasema kwa njia za hizo herufi nyeusi zilizochapwa kitabuni, akiumba maisha mapya ndani ya wasomaji na wasikilizaji na kuwafanya wapya walioitwa. Hivyo basi, usiweke hiki Kitabu cha vitabu kwenye usawa na vitabu vingine kwenye rafu yako, lakini ukiinue na kukiweka mahali pa pekee sana, maana kitabu hiki kinakemea vitabu vyote vingine. Injili ni kamili na imejaa enzi ya kujenga ulimwengu mpya.

Enzi ya Mungu haikuja ulimwenguni kwa njia ya injili ya Kristo, ili aiharibu dunia yetu ovu, lakini kwa kuiokoa, kwa sababu Mungu anatamani watu wote wapate kuokolewa na kufikia ufahamu wa ukweli. Baba yetu wa mbinguni siye dikteta. Yeye hamlazimishi mtu akubali injili ya Mwanawe, lakini anaitoa ukweli wake kwa wanadamu wote bure. Yeyote anayefungua moyo wake kwa maneno ya Kristo na kumtegemea, atapata kuonja enzi ya Mungu. Hivyo, hakuna wokovu bila imani. Yeyote atakayeamini ataunganishwa na Mwana wa Mungu, anayeweka uungu wake ndani ya mwumini, naye anamsafisha, kumtakasa na kumhuisha kwa upya.

Imani ndani ya Kristo inajenga wokovu wa milele ndani ya mtu yeyote, aliye tayari kufungua moyo wake kwake; na tumaini ndani ya Mwana wa Mungu. Ndiyo njia ya pekee kwa ukombozi. Kwa Imani mwumini hupokea msamaha na kufufuliwa kutoka kwa wafu. Kwa hiyo, imani ndiyo hatua thabiti katika waraka kwa Warumi, maana bila imani huwezi kumfahamu Mungu wala kusikia nguvu zake. Yule aaminiye basi, ndiye atakayepata kuhesabiwa haki na kuishi kweli kweli.

Wayahudi walionja ukweli huo wa kupendeza, ingawa wengi wao walimkataa Kristo, wakimchukia na kumsulibisha. Hata hivyo, wateule walionyenyekea wakapata kumtambua na kumwamini. Wakapata kujazwa na Roho Mtakatifu na kuendelea ndani ya upendo wa Mungu. Enzi ya Utatu Utakatifu, hata siku hizi, inaishi ndani ya watu kutokana na ushuhuda wa Mitume wa kwanza.

Wakati wale wachache wa Wayahudi walipopokea wokovu wa Kristo, umati wa Wayunani na wa mataifa mengine, waliofungua mioyo yao kwa injili ya wokovu, wakafuatana nao.

Walitambua kwamba, ujumbe huo haikuwa maneno matupu, bali ilijaa nguvu ya Mungu, inayowaunganisha waumini na Kristo aliye hai ndani ya agano la milele.

Mpendwa ndugu, kama utasoma injili ya Kristo kwa uangalifu, basi ufungue moyo wako kwa neno lake, uamini habari ya uungu wa Yesu, nawe useme naye katika maombi yako; utatambua kwamba, Kristo aliyesulibiwa na kufufuka ndiye Mwokozi wa kweli na Kuhani, Mfalme mwenye Enzi na Mkombozi wa ulimwengu. Basi, uwe na moyo mkuu na kujenga maisha yako kabisa juu ya injili, ili na nguvu ya Mungu ipate kukuzwa ndani ya udhaifu wako.

SALA: Tunakutukuza, Ee Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kwa sababu unajitangaza mwenyewe ndani ya injili ya Kristo, na unatutakasa katika imani, nawe unaishi ndani yetu kwa ukamilifu wako. Pia tunakutukuza, kwa sababu nguvu yako inatenda kazi kikamilifu kwa herufi za barua kwa Warumi na kumwaga ukweli kutoka katika kila kitabu cha Agano Jipya. Fungua macho na utambuzi wetu, tupate kusikia sauti yako, tukutegemee na kukabidhi maisha yetu kabisa kwa busara na maongozi yako.

SWALI:

  1. Tamko gani ndani ya mstari wa 16 unafikiria kuwa muhimu zaidi? Na kwa nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)