Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 010 (The Wrath of God against the Nations)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)

1. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mataifa imewekwa wazi (Warumi 1:18-32)


WARUMI 1:18-21
"18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uwezo wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.“

Baada ya Paulo kulisalimia Kanisa la Rumi kwa unyenyekevu, upendo na hamu, akikazia kwao neno kuu la Injili, ambalo ni haki ya Mungu ndani ya Kristo, basi alianza sehemu ya kwanza ya uchunguzi wake wa kuchimba sana chini. Aliweka wazi kwamba, ghadhabu ya Mungu ya haki inashuka chini dhidi ya uchafu wetu wote dhidi ya Mungu na makosa kwa watu. Siku hizi hatuishi tu katika wakati wa neema, lakini pia katika wakati wa ghadhabu ya Mungu, ambayo ndiyo nia na fumbo wa siku zetu hizi. Yeyote anayemfahamu huyu Mtakatifu atamstahi na kutetemeka kwa hasira yake. Hakuna anayejifahamu mwenyewe, hadi atakapotambua ingawa kidogo kuhusu mianga ya utakatifu wa Yule Mtakatifu. Chuki za watu dhidi yake zinaonekana sana katika ukuu wa kimungu.

Mungu aliwaumba wanadamu kwa mfano (sura) wake (Mwanzo 1:26-27), lakini wao kwa kiburi chao cha kikorofi, kwa ujinga wao walichagua uhuru watoke kwake. Hata hivyo katika uvumilivu wake, hakuwaangamiza hao maskini na wa kutokutii, lakini alitazamia kwamba, waelekee kwake tena kwa shukrani, na kujisalimisha kwake mara. Lakini walijipenda wenyewe zaidi ya Mungu, na wakabaki mbali naye, hadi walipopata kuwa vipofu kiroho. Hapo wakakoma kusikia utukufu wa Mtakatifu, lakini waliendelea katika maovu, wakirushana wao kwa wao, na hata kuwazuia wengine wasipokee wokovu, wakikazia upotovu wao na uchafu kuwa ndiyo njia ya kufaa.

Mbali na kuanguka kwake katika dhambi, mwanadamu bado anayo uwezo wa kutambua kuwepo kwake Mungu kwa njia ya miujiza yake katika mambo ya asili. Uchunguze tu muundo wa mimea, uwezo wa chembe (atom), na ukuu wa manamba ya nyota yasioweza kuhesabika, basi ukiyazingatia hayo, utamwabudu Mwumbaji, maana ndiye mwenye hekima yote, mwenye enzi yote na wa milele. Je, unatambua uzuri wa utu wako, utambuzi wa dhamiri yako, na uwezo wako wa akili ya kuunda vitu na mambo mengine ya kushangaza? Unasikiliza mapigo ya moyo wako, inayopiga mara mia elfu (100 000) kutwa, ili kupeleka damu kwenye sehemu zote za mwili wako? Miujiza hiyo haiendi kwa kujiendea kwenyewe, bali ni zawadi za Mwumbaji kwako.

Basi, nani kati yetu atakosa kusimama kwa kicho na kutetemeka tunapoona utukufu wa Mungu katika mambo ya asili? Shuhuda za utukufu wake zinasema bila kukoma. Mtu wa maendeleo wa wakati wetu, basi, hana muda wa kutosha asome kwenye kitabu kilicho wazi cha mambo ya asili, ingawa kimeandikwa wazi kabisa kwa mkono wa Mungu.

Yule akosaye kumheshimu Mwumbaji, akirudisha kwake shukrani kwa yote aliyoyatenda na kujikabidhi kwa utukufu wake, huyu atapumbaa. Atapoteza hekima ya Roho Mtakatifu, na atakuwa kipofu akilini mwake na atapata tabia ya kinyama. – Hivyo, ndugu mpendwa, umtukuze Mungu kwa upendo na hofu, maana alikuumba kwa mfano wake na kukupulizia pumzi ya uhai ndani yako. Wewe ni mali yake, wala huwezi kuishi bila yeye.

Watu wote wasiomwabudu Mungu katika ukweli, wamepotea, ni wenye dhambi na hawaamini. Walipoteza kiini cha uwezo na nguvu zao, walikandamiza dhamiri zao na kutia giza akilini na rohoni. Wanadhania maongo katika shabaha zao kuwa ya kweli, wanapinda ufahamu wa Mungu na kuikomesha kwa ukali. Kwa hiyo, umwulize Bwana wako akujalie Imani iliyo hai, ndipo uwaongoze na wengine wapate kuamini habari ya kuwepo kwake Mungu, maana pasipo kutegemea ndani ya utukufu wake na shukrani kwa ajili ya rehema zake, ubinadamu utaangamia kwenye hasira ya Mungu, iliyofunuliwa dhidi yao.

SALA: Ewe Mungu mtakatifu, uliye mwenye enzi yote, tunakushukuru kwa sababu umetuleta kwenye uhai, na kutufanya kuwa kwenye mfanyizo bora. Twaomba utusamehe ujuujuu na ulegevu wetu wa kukusifu. Utusaidie tuelekee kwako, tushuhudie kuwepo kwako hadharani, tuendelee katika upendo wako kila siku, tukutukuze wakati wowote, pia na tueleze wazi habari ya hasira yako ya haki dhidi ya hali yote ya kutokukutambua na ya kuwa bila uadilifu wote, ili watu wapate kuungama na kukugeukia.

SWALI:

  1. Kwa nini ghadhabu (au hasira) ya Mungu imefunuliwa?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 01:05 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)