Previous Lesson -- Next Lesson
b) Hamu ya muda mrefu ya Paulo atembelee Rumi (Warumi 1:8-15)
WARUMI 1:8-12
“8 Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubbiriwa katika dunia nzima. 9 Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu, 10 nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu. 11 Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara; yaani tufarijiane, 12 mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.”
Paulo aliwahi kusikia mengi kuhusu kanisa la Rumi, akikutana na baadhi ya washiriki wao wakati wa safari zake za kimissionari, naye akagundua kwamba, imani yao ni ya kweli, ni hai na kukomaa. Alimshukuru Mungu kwa moyo wote kwa mwijiza huo, maana kila Mkristo ni mwujiza wa upatanisho ndani ya Kristo, ambao kiini chake kinadai shukrani yetu. Popote ambapo kundi la watu wanamtumikia Mungu na Mwana katika Roho Mtakatifu, hapo inatupasa kumwabudu Baba tukimsifu na kufurahia ndani yake mchana na usiku.
Paulo alimwita Mungu “Mungu wangu”, kana kwamba yeye ni ya kwake. Alijua kwamba moyo wake ulifungamana naye katika agano mpya, naye alimpenda kabisa kwa moyo. Lakini mbali na huo uhusiano wa karibu, hakuomba kwake huyu Mungu aliye juu sana katika jina lake lenyewe, lakini katika jina la Kristo, akitambua kwamba, maombi yetu yote, hata na shukrani zetu hazistahili kuletwa mbele za utukufu wa Mungu. Yote tunayoyamwaga kutoka kwa mioyo yetu yanahitaji nguvu ya utakaso wa damu ya Yesu Kristo. Kwa njia ya utakaso huo tu tunaweza kumwomba Mungu, anayetujalia Roho yake, ili tuweze kutukuza jina lake la kibaba na kumwabudu na furaha. Watumishi wake wote ni takatifu kwake, nao ni mali yake kama watumwa wa upendo wake.
Kiini cha huduma yao ndiyo Injili. Tunatambua kwamba Paulo katika mstari wa kwanza wa barua hii alitamka injili kuwa ni “Injili ya Mungu”, ambapo katika mstari wa 9 tunasoma “Injili ya Mwana Wake”. Kwa neno hilo anamaanisha kwamba, habari njema tukufu ya wokovu inategemea kwenye asili ya Mwana wa Mungu. Hamu zote za Paulo zinazunguka uwana wa Kristo na ubaba wa Mungu. Yeyote anayekataa injili hii kwa juhudi na kuikemea kwa kusudi, huyu na alaaniwe.
Paulo aliendesha maisha katika ushirikiano wa karibu sana na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Aliitia umoja wa Utatu Utakatifu kushuhudia kwamba, alikuwa akifikiria wakati wowote habari ya kanisa la Rumi na kuliombea. Mtume wa mataifa hakusahau makanisa mbali na shughuli zake kadhaa, naye aliwaombea kwa uaminifu hata watu mmoja mmoja. Hakuna mchungaji mwaminifu au kasisi aliyejaliwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, isipokuwa anakuwa na maombi ya kuendelea kila wakati. Ambapo kuna nguvu kutoka kwa fulani, sababu yake lazima iwe ni upendo, sala, na hamu kwa ajili ya Mungu na watu pia.
Paulo alikuwa amehifadhi kusudi lake la kutembelea Rumi kwa miaka, na hasa katika kipindi alichokiita “sasa”, ambapo ilikuwa ni muda wa kutumika kule Anatolia, Makedonia na Ugriki. Alitambua kwamba muda huo sasa ni wa kuvaa kiatu cha kutembelea Italia.
Hata hivyo, hakuamua kuanza safari yake kufuatana na kusudi na mipango yake mwenyewe. Daima aliangalia sana atembee katika mapenzi ya Mungu, akiangalia ukweli kwamba, mipango ya binafsi tu, bila kuambatisha, inaweza kupeleka kwa kukosa, bahili na shida. Paulo hakuwa mfungwa kwa tamaa zake mwanyewe na kutaka kwake, lakini alipanga mambo yote kabisa chini ya uongozi wa Baba yake wa mbinguni.
Ingawa hivyo, kujitoa kwake hivyo haikuzuia hamu yake ya kweli ya kutembelea kanisa la Rumi, ambapo hajawahi kufika. Alitambua sana kwamba, alijawa na Roho Mtakatifu. Alikuwa kama mlima (volkeno) mwenye kutupa nguvu ya Mungu kuelekea pande zote, na kwa sababu hiyo, alitamani kulifanya kanisa la Rumi liwe la kushiriki katika nguvu alizokabidhiwa na Kristo, ili kanisa lipate kufufuka kwa upya, tayari kwa huduma na kujengwa katika upendo, imani na tumaini la kweli. Hiyo ndiyo sura pekee ya utumishi na shabaha kuu ya Matendo ya Mitume kwamba, waumini wajengeke na kuimarishwa.
Paulo hakupenda kufikia Rumi kama mfadhili mkuu, bakini alijinyenyekeza sana, akaandika kwamba, hakut6aka kuwafikia kwa kutoa tu, bali pia kwa kupokea kwa mnjia ya kusikiliza na kuona. Alifanya hivyo kwa kusudi la kutambua yale, ambayo Mungu alitenda nini kwa wale waumini wa Mji Mkuu, bila yeye Paulo; hivyo angefarijika pamoja na mitume wote, kutokana na ushuhuda wa Mfariji mtukufu ndani ya watakatifu wa Rumi.
Paulo naye alishuhudia kabla ya hapo kwamba, hatawafikia na imani mpya, bali kwamba imani ile ile, ufahamu na nguvu hufanya kazi ndani ya Wakristo wote wa kweli, walio washiriki wa mwili wa kiroho wa kristo. Kila mmoja anayedai kwamba, kuna zaidi ya kanisa moja, huyu ni mwongo; maana Roho Mtakatifu ni mmoja, Kristo ni mmoja na Baba ni mmoja. Kote wanakokutana waumini waaminifu, wanajumlika kama watoto wa Baba mmoja, hata kama hawakufahamiana kabla ya hapo. Huwa wanafurahi mno, na kukutana katika hali ya kupatana, kama waliozaliwa na Roho yule yule na kuwa washiriki wa familia moja iliyo sawa, na kuunganishwa katika taratibu na shabaha zile zile.
SALA: Tunakuabudu, Ee Baba, kwa sababu wewe unalikusanya kanisa lako kutoka katika ulimwenguni kote, na unaliimarisha, pia na kulijaza na sifa zako. Tufundishe namna ya kuwaombea ndugu zetu kokote. Asante sana kwa watoto wako waaminifuwote kila mahali. maana kila mmoja aliyezaliwa na Roho wako Mtakatifu ni mwujiza. Tufungulie macho yetu, ili tupendane na kueleana wote na kufurahia katika kuwepo kwako. Utujalie hekima na msamaha, ili ushirikiano wetu udumu na kutunzwa katika imani yako, wala tusisogee mbali na ushirikiano wetu na wewe, na wa Mwana, na wa Roho Mtakatifu.
SWALI:
- Kwa nini Paulo alikuwa akimshukuru Mungu kila wakati?