Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 005 (Identification and apostolic benediction)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Ufunguzi Wa Barua: Salamu, Shukrani Kwa Mungu, Na Mkazo „Haki Ya Mungu” Kama Neno Kuu La Barua Hii (Warumi 1: 1 – 17 )

a) Tambulisho na Mbaraka wa kitume (Warumi 1:1-7)


WARUMI 1:7
7 „Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo“.

Mbaraka wa kitume, ambao kwa hiyo Paulo huanza karibu zote za barua zake, ndiyo jumlisho la ufahamu wake wa ki-theologia, ni mkusanyiko wa nguvu yake ya kitume, pia ni ufahamu wa baraka zake nyingi, anazozimimina juu ya wasomaji wake. – Basi na wewe ujiweke kwa makini chini ya mwagiko wa neema iliyo ndani ya maneno haya, na uyazingatie moyoni mwako, ili upate kuwa tajiri katika Mungu. Haya, tunza Mbaraka wa Kitume moyoni mwako na uifurahie neno kwa neno.

Jambo la kwanza ambalo mtume anakutolea ni neema kamili, maana kiasili wewe umepotea na utahukumiwa, lakiniMungu akupenda naye hataki kukuharibu. Kwa sababu ya kifo cha Mwana wake wa pekee, badala ya kukuhukumu wewe, atakujalia hali ya haki. Neema ndiyo namna ya halali ya upendo wa Mungu. Yeye Mtakatifu anaendelea kuwa sahihi, hata anapokupatia uadilifu, usiyestahili kupewa haki. Zawadi zote za Mungu ni zako, na majibu yote ya maombi yako ni upendeleo tu, maana hustahili kitu ila ghadhabu tu.

Pamoja na hayo, msimamo wetu upande wa Mungu umebadilika tangu kifo cha Kristo; zamani kulikuwa na uadui kati ya Mungu na watenda dhambi. lakini amani sasa umeshinda kwa sababu ya upatanisho ndani ya msalaba. Huyu Mtakatifu wa milele hatatuharibu hata kidogo. Maneno ya kwanza aliyoyasema Kristo baada ya ufufuo wake yalikuwa: „Amani iwe kwenu“. Yeye alitimiza yote yaliyotakiwa na Sheria, na hakuna tena malalamiko kabisa dhidi yetu mbele za Mungu, kwa sababu ya damu ya Kristo linalotusafisha. Muda mpya kabisa ulianza pamoja na amani ya kweli unaotawala sasa mioyoni mwa wale waliotakaswa.

Yeyote atakayepokea neema ya Kristo inavyofahamika kweli na kuishi katika amani na Mungu, basi atatambua mwujiza mkuu, kwamba Mwumbaji na Mwenye Enzi siye mjeuri anayetutaka tumwabudu kwa kutetemeka, lakini yeye ni Baba yetu atupendaye na kututunza. Hatatuacha, tena bila kukoma anatuvumilia. Hakuna maneno ndani ya Agano Jipya yanayopendeza zaidi kuliko haya „Mungu Baba yetu“. Ufahamu huu wa kitheologia unaletwa na Kristo mwenyewe. Tamko hilo la ubaba wa Mungu ndiyo ufunuo mpya ndani ya Ukristo. Zaidi ya hapo, kusudi la msalaba si lingine ila kutusafisha, ili tuweze kustahili kupokelewa kama watoto, ndiyo kuzaliwa mara ya pili na uhai wa milele kuishi ndani yetu. Hiyo ndiyo utaratibu kwamba Mungu awe kweli Mungu wetu na sisi watoto wake.

Je, wewe unamfahamu Yesu Kristo? Unatambua ukuu wake na pia unyenyekevu wake? Yeye ni yote mawili, mwanadamu na Mungu ndani ya nafsi yake moja. Alitujalia utukufu wake, akajinyenyekeza mwenyewe kwa ajili ya kutukomboa. Na alipokamilisha upatanisho kwa binadamu wote, alipaa kwa Baba yake, anapoketi mkononi mwake wa kulia, mwenye kuheshimiwa sana, kwa sababu ndiye pekee aliyeweza kupatanisha ulimwengu na Mungu.

Ndiyo sababu Yesu alirithi enzi yote ya Mungu. Yeye ndiye Bwana mwenyewe; je, naye ni Bwana wako? Anapenda kuwa na mamlaka juu ya maisha yako; kukusafisha, kukutakasa na kukutuma apendavyo.

SALA: Ewe Baba wa mbinguni, wewe ni Baba yangu ndani ya Yesu Kristo. Ulinichagua hali nimepotea na mchafu, nipate kuwa mtoto wako. Naanguka kifudifudi, nikikuabudu na kukupenda, nikitoa maisha yangu, pesa zangu,nguvu zangu na muda wangu kwako na kwa Mwana wako. Unitengeneze ikupendezavyo, ili nisiwe aibu kwako, lakini nitukuze ubaba wako kwa adabu kamili kwa ajili ya jina lako. Asante sana kwamba ulimtuma Mwana wako Yesu awaokoe wenye dhambi wote. Nakuabudu na sifa zisizokoma.

SWALI:

  1. Tamko gani ndani ya Mbaraka wa Kitume unahesabu kuwa lenye uzito zaidi na na kukufaa zaidi kuhusu maisha yako?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 14, 2022, at 02:08 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)