Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 007 (Paul’s Desire to Visit Rome)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Ufunguzi Wa Barua: Salamu, Shukrani Kwa Mungu, Na Mkazo „Haki Ya Mungu” Kama Neno Kuu La Barua Hii (Warumi 1: 1 – 17 )

b) Hamu ya muda mrefu ya Paulo atembelee Rumi (Warumi 1:8-15)


WARUMI 1:13-15
“13 Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu nyingi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine. 14 Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima. 15 Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.”

Katika barua hii Paulo anafungua moyo wake kwa watu wa kanisa la Rumi. Anawaeleza jinsi alivyokusudia mara nyingi na hata kupanga kuwatembelea, lakini kwamba Mungu alikatiza mipango yake yote. Ilimpasa huyu mtume mkuu kujifunza mapema kwamba, mawazo ya Mungu ni tofauti na ya kwake, na njia za Mungu ziko juu sana jinsi mbinguni iko juu zaidi ya dunia. Roho wa Kristo alimzuia asitimize mipango yake, hata kwake mwenyewe ilionekana ni ya kufaa, ni nzuri na takatifu. Zaidi ya hapo, wakati nafasi ya kusafiri kwake ilipoonekana kuwa bora, hata hapo Mungu alimzuia.

Pamoja na hayo, Paulo aliweka moyoni mwake kwamba, ilimpasa kuhubiri kwa ulimwengu kote. Kwa maisha yake alipenda kuanzisha ufalme wa Mungu pia mjini Rumi na katika mataifa mengine. Yeye hakukusudia kufundisha mtu mmoja mmoja binafsi, badala yake alikusudia kufundisha mataifa, maana alikuwa na hakika ya baraka ya Kristo, aliyetenda kazi ndani yake. Aliwahi kumwona Bwana wake mwenye utukufu na alijua kabisa kwamba, dunia yote ni mali ya Mfalme wa wafalme, na kwamba ushindi wake ni jambo la uhakika.

Mtume wa Mataifa alijiona mwenyewe kuwa mwenye kudaiwa na watu wote, si kwa sababu alichukua fedha kwao, lakini kwa sababu Mungu alimkabidhi madaraka yake na nguvu.. Kwa hiyo alijisikia kuwa chini ya masharti kukabidhi hiyo nguvu na mamlaka kwa wote waliochaguliwa na Kristo. – Ni kweli kabisa, sisi sote hata siku hizi tunaishi kutokana na vipawa vya Mungu kwa Paulo, ambavyo kwa njia za barua zake anatufanya tuwe washiriki katika nguvu zake. Kufuatana na maana hiyo, sisi nasi tumepata kuwa wadaiwa kwenu, jinsi na wewe kuwa mdaiwa kwa watu wanaokuzunguka wewe, maana roho anayefanya kazi ndani yetu sio yetu tu, lakini yu tayari kutawala ndani ya mioyo ya wengi.

Paulo alitenda kazi kati ya daraja la Wayunani waliosoma, naye Bwana aliimarisha huduma yake kwa njia ya udhaifu wa Paulo. Alianzisha makanisa kwenye sehemu za nchi karibu na Bahari ya Kati, zinazozunguka viziwa vya Uyunani. Ndipo wakati alipoandika barua hiyo, alikusudia kwenda kufanya kazi kati ya washenzi nchini Ufaransa, Spania na Ujerumani. Alikuwa na shauku kueneza kwa kila mtu wakati wa baraka kwamba, Mungu anaye Mwana aliyetukomboa msalabani. Katika kusudi lake hili na moyo wa kujitoa ibadani huyu Mtume wa Mataifa alikuwa anafanana na fataki tayari kurushwa juu. Alikuwa amepokea ujumbe, ili apate kuushirikisha kwa wengine.Hata kutokana na upendo wake kwa washenzi, alitamani kuchuma uangalifu wa Warumi, ili wao nao wapate kusindikizana naye na kushiriki naye katika shabaha yake ya kuwahubiri mataifa. Hivyo, alitaka kuhubiri kwa waumini kule Rumi, kusudi wao nao wapate kuwa wahubiri, maana mpato wa wokovu inaumba ndani yake aliyeokolewa msukumo wa ulazima kupeleka ujimbe wa wokovu kwa watu wengine.. Paulo alikazia macho Rumi kama mji mkuu wa kuanzia huduma ya kuhubiria kwa ulimwengu mzima.

Pamoja na hayo, Mungu alijibu sala za mtume wake kwa njia nyingine. Hakumtuma balozi wake kwenda Rumi moja kwa moja, ila kwanza alimrudisha Yerusalemu alipokamatwa na kutiwa gerezani. Baada ya miaka mirefu na ya kuumizwa Paulo alifikia mji mkuu hali ametiwa mapingu na kuwa mfungwa, ila hata hivyo akiwa mtumwa wa Kristo. Pamoja na hayo, enzi ya Mungu haikukoma ndani yake. Akiwa akitembea na mapingu, alihubiri kwa ulimwengu mzima kwa barua yake kwa Warumi, ambalo bado linaendelea kuhubiri kwa watu na mataifa na kwetu sisi hadi leo.

Haya, sisi sasa, tulio wajukuu wa mbali wa wale Washenzi, ambao Paulo alikusudia kuwahubiria pia, sisi kwa furaha tunaeneza injili ya Mungu jinsi alivyokusudia Paulo afanye wakati wake. Pengine haikupita mawazoni mwa Paulo kwamba, barua yake hii kwa Warumi ndiyo ukamilisho wa mapenzi yake kuhubiri kwa mataifa yote. Hakuna kitabu kingine, pembeni ya Injili ya Yohana, kilichobadilisha ulimwengu kama barua hii, iliyoandikwa pamoja na maombi mengi na kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (Warumi 8:26b) kwa Roho.

SALA: Ee Bwana, wewe ndiwe Mfalme, nawe huwaongoza watumishi wako kufuatana na mapenzi yako. Utusamehe, kama tulikusudia mambo yasiofuatana na mapenzi yako. Utufundishe kabisa kwa uongozi wako, ili tusikimbie nje ya mipango ya upendo wako, lakini tutii maagizo ya Roho yako, tukitimiza mahitaji yako kwa furaha, hata ikiwa yanakuwa kinyume cha matazamio yetu. Ee Bwana, njia yako ni takatifu, nasi tunajikabidhi kwa maongozi yako. Tunakushukuru kwa sababu hutaturuhusu kwenda mbali na rehema yako.

SWALI:

  1. Jinsi gani, na mara ngapi Mungu alimzuia Paulo kutimiza mipango yake ya binafsi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:35 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)