Previous Lesson -- Next Lesson
3. Yesu awatokea wanafunzi wake pamoja na Tomaso (Yohana 20:24–29)
Yohana 20:24-25
“Walakini mmoja wa wale thenashara , Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.”
Usifikiri kwamba mateteo yote ni kinyume cha Roho Mtakatifu; wala si kila mmoja anayekataa ushuhuda wako atakuwa ni mkaidi au wa kupotea. Hapo Yohana anaonyesha kwamba kati ya mengi yaliyotokea katika zile siku 40 kabla ya Kristo kupaa mbinguni, kulikuwa na jambo la ajabu. Hii inaonyesha jinsi neema inayoumba imani ndani ya moyo wa mtu; si kwa matendo yoyote, utambuzi au akili yake, lakini kwa neema na rehema peke yake.
Tomaso alikuwa ni mtu aonaye yote kuwa mabaya, akiona tu upande wa giza wa matokeo. Ilimpasa kujaribu kufikia kina cha chini cha mambo ili afikie kweli sawasawa (Yohana 11:16; 14:5). Alikuwa mwenye kuwaza sana, akijaribu kukomesha mambo kiakili. Alikuwa ameona ndani ya kifo cha Kristo kupoteza maana ya maisha. Akajitenga na kundi la wanafunzi, hivyo hakumwona Yesu jumapili ile ya kwanza, wakati Yesu alipotokea katikati ya wafuasi wake.
Pengine Tomaso angehoji kwamba kutokea kwake ilikuwa ni maono ya uongo ya kishetani kwamba roho mbaya fulani alijichukulia sura ya Kristo, ili kuwaongoza kwenye upotovu. Hivyo haishangazi kwamba, alipokuwa nao alisisitiza kupewa thibitisho ya salama kabisa juu ya mambo yaliyotukia, ya kwamba Yesu kweli aliwajia binafsi. Hakuweza kusadikishwa, ila kwa kushika kabisa kovu za misumari mkononi mwake. Kwa njia hiyo alipigania na Mungu apate kuamini, akihitaji kuona kabla ya kukubali.
Kwa hali hiyo alirudi kundini mwa wanafunzi, ambao walikuwa wanajaa furaha kutokana na kutokea kwake Kristo kati yao. Lakini yeye basi, alikuwa na huzuni, akisema kwamba anahitaji kuwa na hakika kwamba Yesu alifufuka.
Yohana 20:26-28
“Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa , akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu, ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!“
Juma moja baada ya hapo, Yesu aliwatokea wanafunzi wake tena. Bado walikuwa na hofu na milango ilikuwa imefungwa. Kimwili Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu, aliwatokea ndani bila kusikika kabisa. Aliwabariki na amani yake, akiwapa uradhi wanafunzi wake wadhaifu.
Tomaso alimwona Bwana wake kwa mshangao mkubwa machoni, akisikia na sauti yake. Yesu akawaona wote pamoja, ila macho yake yakachoma mashaka ya Tomaso kwa mtazamo mtukufu wa upendo. Alipojikunja Tomaso, Yesu akamwomba amguse, kinyume cha agizo kwa Mariamu Magdalene, akimwambia, “Niguse na kusikia, mimi ni mtu kweli, nikiwa hapo kati yenu kimwili.” Yesu hakumwomba tu kutambua alama za misumari, lakini “karibia na kuweka kidole chako ndani ya kovu ukaamini.”
Alimsukuma mwanafunzi wake mwenye kusitasita ashinde mashaka yake. Basi Yesu anatazamia tumaini kamili toka kwetu, maana aliwahi kutangaza msalaba wake , ufufuo wake, kurudi kwake kwa Mungu na kurudi kwake mara ya pili, yote kwa ajili ya faida yetu. Yeye akataaye kweli hizo zote atamfanya kuwa mwongo.
Shabaha ya Bwana yenye upendo ilivunja mashaka ya Tomaso, akanong’ona (kama kujumlisha sala na kutafakari kwake) shuhuda kubwa kuliko yote yaliyotamkwa kwake Yesu: “BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!” Alitambua, akitamani kwa huzuni kuelewa ukweli, kwamba Yesu si Mwana wa Mungu anayejitegemea mbali na Babaye, bali ni Bwana mwenye enzi mwenyewe, akiwa na ukamilifu wa uungu ndani ya nafsi yake. Mungu ni mmoja , sio wawili. Tomaso akamwita Yesu Mungu, akajua kwamba huyu Mtakatifu hatamhukumu kwa ajili ya kutokuamini kwake, lakini kumjalia neena yake ya kumwamini Bwana Mwenyewe alivyo. Tomaso pia alimwita Bwana kwa kukabidhi yote yaliyopita na mambo yake ya mbeleni yote ndani ya mikono ya Mwokozi wake, akiamini kabisa yaliyosemwa na Yesu katika hotuba yake ya kuwaaga. - Ndugu je, wewe unasemaje? Unashiriki katika ushuhuda wa Tomaso? Huyu Mfufuka amekujia wewe, kiasi cha kukushangaza juu ya enzi yake na kushinda mashaka na ukaidi wako? Ujitupe ndani ya mikono yake ya rehema na kukiri mbele zake, “Bwana wangu na Mungu wangu.”
Sala: Tunakushukuru, Bwana Yesu Kristo, kwa sababu hukumkataa Tomaso mwenye mashaka, lakini ulijifunua kwake. Upokee maisha yetu yawe ya kwako, na ukatakase ulimi wetu na udanganyifu yote.
Swali 127: Ushuhuda wa Tomaso inadokeza nini?