Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 122 (Jesus appears to the disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)

2. Yesu awatokea wanafunzi wake kwenye chumba cha orofani (Yohana 20:19-23)


Yohana 20:22-23
„Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; nao wo wote ntakaowafungia dhambi, wamefungiwa.“

Pengine wanafunzi walikuwa wameshtushwa, Yesu alipowaambia, „Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.“ Bado walikuwa ndani ya chumba kilichofungwa kwa hofu ya Wayahudi. Hawakusikia nguvu yoyote ndani yao wenyewe, ila hivi juzijuzi walionja hali ya kushindwa kabisa. Basi Yesu akawavuvia wanafunzi wake, jinsi Mungu alivyovuvia roho yake ya uhai ndani ya Adamu apate kuwa mtu mwenye uhai na kupata nguvu ya kuishi. Kwa kuwavuvia hivyo, Yesu aliwaonyesha wazi hali yake ya kuwa Mwumbaji; hapo alianzisha uumbaji mpya ndani ya wale wanafunzi na kuwahakikishia kwamba, Roho yake pamoja na nguvu yenye mamlaka itawatawala, ikiwawezesha, kuonyesha sura ya Baba ndani ya kuishi kwao.

Wanafunzi baada ya kupokea Roho Mtakatifu, Kristo aliwakabidhi mambo yanayohitajika kwa watu wapate msamaha wa dhambi. Walitakiwa kutangaza uradhi kwa wote wanaokubali masharti hayo, na pia kutangaza zuio la radhi kwa wale wanaokataa yale masharti.

Walitakiwa kueleza msamaha ya makosa kwa niaba ya Bwana Kristo. Kwa msingi wa kutubu kwao watakubaliwa kuwa washiriki katika Kanisa la Kristo.

Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kutangaza msamaha, wala si wao wenyewe kusamehe; ni Mungu pekee ndiye anayesamehe ( Isaya 43:25 ).

Yesu anakusihi na wewe upate kuwa balozi wake katika dunia hii ovu; anatamani kuendeleza nguvu yake ya kuokoa kwa kukutumia na wewe. Usiondoke kwa moyo wa kuzungumzia uwezo wako mdogo, lakini endelea kudumu katika ushirikiano na Bwana wako, jinsi balozi katika maisha ya kawaida anavyoendeleza maongezi na Mfalme au Rais wake, ili apokee maagizo na uongozi wa kila siku, ndipo ayatumie kila siku. Wewe sio mungu mdogo mwenye kutenda kwa uhuru, lakini utakuwa ni mtumwa wa Bwana. Yeye anatamani kuokoa watu kwa njia yako. Leo ukisikia sauti yake, usifanye mgumu moyo wako, bali kufungua akili na dhamiri yako, ili Roho Mtakatifu apate kukufanya uwe shahidi wa Kristo mwenye ujasiri, lakini hata hivyo mwenye unyenyekevu na hekima.

Sala: Bwana Yesu, mimi sistahili wewe upate kuingia nyumbani kwangu; hata hivyo, wewe umesema na kunijalia Roho Mtakatifu wako, akanimulikia na kunihuisha. Umenituma nishuhudie kwa niaba yako kwa wanadamu. Asante sana, kwa sababu nguvu yako umekamilika ndani ya udhaifu wangu. Nitunze katika hali ya unyenyekevu bila unafiki; nisafishe na mawazo yote ya ubinafsi, ili siku zote niwe ninakwenda sambamba na mapenzi yako. Ndipo naamini amani yako itawafikia wengine wengi.

Swali 126: Roho Mtakatifu ni nani? Atatenda nini kwa njia ya ushuhuda wako juu ya Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 05:51 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)