Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 124 (Jesus appears to the disciples with Thomas)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)

3. Yesu awatokea wanafunzi wake pamoja na Tomaso (Yohana 20:24–29)


Yohana 20:29
“Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.”

Hatuna uhakika kama kweli Tomaso aligusa jeraha za Yesu, au aliridhika kwa kuona makovu. Pengine alikuwa na haya kwa kutokuamini kwake na akapungua ujasiri wa kumgusa. Yesu aliita imani ya Tomaso kuwa ni ushuhuda wa kukiri kutokana na msingi wa kuona kwa macho. Lakini Bwana anahitaji kuumba imani kwenye daraja la juu zaidi, tumaini ndani yake inayotegemea Neno lake tu bila kumwona binafsi. Yeye anayetamani ndoto au maono au hata matokeo fulani kwa kuhakikisha imani yake, yeye bado ni mtu wa kuanza, bado hajakamilika wala kuwa na msingi imara. Hata hivyo, Yesu aliwatokea mitume wake mara kwa mara, ili kuimarisha imani yao kwa ajili ya matukio yenye mashaka.

Wale waaminio bila kumwona mwenyewe, hao wanabarikiwa na Yesu na kufikia furaha kuu. Imani ya kweli inakusanya nguvu zaidi ndani yetu kuliko maono yasiyoshikika. Tumaini la mtu ndani ya Neno la Mungu inamheshimu Msemaji asiyeonekana.

Tangu matokeo ya Kristo mara kwa mara, wainjilisti na mitume wameanza kuhubiri kwetu kwa njia ya Injili na Barua kadhaa. Kufufuka kwake Yesu ndiyo tangazo la millennium mpya, ambamo uhai wa Mungu inatawala mioyo ya waumini. Imani yetu sio kusadiki tupu au mawazo; hapana, ni uhai na kuunganika na Kristo aliyefufuka. Hii ndiyo mwujiza wa siku zetu; mamillioni wa watu wanaamini ndani ya Yesu bila kumwona, maana kwa imani wametambua nguvu ya uzima wa milele.

Wakristo wengi hapo baadaye walipoteza mali yao, jamaa na hata maisha yao. Walikuwa na ukweli kwa njia ya imani ndani ya Neno la Kristo, imani inayoshinda hata elimu ya akili tu. Yesu hutuza imani ya namna hii kwa neno lake na kwa kuleta uhai wake ndani ya mwumini. Imani yetu inakumbatia uhai na maisha yetu yote na kutuunganisha na Yesu Mwokozi wetu.

Sala: Bwana Yesu, wewe ndiwe mweka misingi na mkamilishi wa imani yetu. Wewe watupenda, na ukweli wako unatufikia kwa njia ya Neno lako. Sasa naamini kabisa kwamba utaniokoa hadi mwisho, pia na wengi wa marafiki zangu; wewe utawahuisha na kuwaimarisha ndani ya imani iliyo hai kwa jina lako, ili nao wawe na uzima wa milele na furaha kuu.

Swali 128: Kwa nini Yesu huwaita waumini “wabarikiwa”, ambao hawakumwona binafsi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 05:54 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)