Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 106 (Jesus arrested in the garden)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
A - Matokeo kuanzia kukamatwa kwake Yesu hadi kuzikwa kwake (Yohana 18:1 - 19:42)

1. Yesu ankamatwa bustanini (Yohana 18:1-11)


YOHANA 18:1-3
„Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng’ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake. Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.“

Yesu alisema na Baba yake katika sala, akikabidhi maisha yake mikononi mwa Mungu, pamoja na ya mitume na wafuasi wake. Kwa sala hiyo ya kuaga alikamilisha maneno yake, huduma na maombi yake. Ndipo akaingia katika hatua mpya ya mateso na taabu, ili akamilishe wito wake kuwa Kondoo wa Mungu abebaye dhambi ya ulimwengu.

Hivyo akaingia ndani ya bustani iliyozungushwa na ukuta kule penye mlima wa Mizeituni ng’ambo ya mto Kidroni, palipo na kishinikizo cha zabibu. Hii ilikuwa mahali pa kutulia na faragha, ambapo yeye na wanafunzi wake walirejea mara kwa mara, hata kulala.

Yuda alijua mahali pale pa utulivu, akajulisha wakuu wa Wayahudi mahali ambapo Yesu alipo. Wakafurahi na kukusanya walinzi wa hekalu na viongozi wa mafarisayo. Hawakuwa na haki ya kumkamata mtu usiku wala kubeba silaha, ila kwa kibali cha watawala wa kirumi. Basi wakamjulisha liwali. Viongozi wa Wayahudi hawakuridhika na taarifa ya Yuda tu, bali walimsukuma aongoze lile kundi la kumkamata Kristo. Hivyo, Yuda hakuwa msaliti tu, lakini pia alimkabidhi Yesu kwa maadui zake. Mungu anakataa kwamba angeruhusu Mwana wake kuchukua usawa wa msaliti au yeye vivyo. Mungu yu juu ya ubaya kama huo.

YOHANA 18:4-6
“Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.

Hatuna habari jinsi gani hao washambulizi walivyofaulu kuingia ndani ya bustani. Bila shaka walikuwa na taa nyingi, ili wapate kumtafuta, ikiwa angejaribu kukimbia. Yesu alikuwa kabisa ndani ya maombi, na huku wanafunzi wake wakilala usingizi. Hata hivyo akatambua lile kundi likikaribia pamoja na msaliti. Hakuchukua hatua ya kukimbia, ingawa alifahamu yale yaliyomngojea kwa hukumu kali na mateso. Alitambua mambo yote, akaendelea kuwa mtii kwa Baba. Akainuka na kujitoa kwa kundi lile lililokaribia; enzi na heshima yake bado zikionekana. Kwa kweli, haikuwa Yuda aliyemkabidhi Yesu, lakini Bwana mwenyewe aliyejitoa kwa ajili yetu.

Aliwauliza, “Ni nani mnayemtafuta?” Walipotamka jina lake, alijibu kwa matamshi tukufu, “Mimi ndimi”. Yeyote mwenye utambuzi wa kiroho angefahamu hapo kwamba, ndani ya Yesu Mungu mwenyewe alikuwa amesimama kati yao, akiwaambia yale ambayo Mungu alimwambia Musa, “Mimi ndimi”. “Eti, kweli mnakusudia kumwua Mwokozi wenu? Ni mimi, angalieni mtakayofanya. Mimi ndiye Mwumbaji na Mwokozi, nikisimama hivi mbele zenu.”

Wakati uo huo Yuda alikuwa amesimama pale, na maneno hayo yalichoma moyo wake. Hapo ndipo mara ya mwisho anapotajwa katika Injili ya Yohana. Yohana hataji lile busu la Yuda, wala jinsi alivyojiua. Fikira ya kwanza ya Yohana lilikuwa ni Yesu, anayemchora kwa maneno matukufu mbele ya adui zake. Kujitoa kwake hivi kwa hiari ilichoma moyo wa Yuda, maana akaona Yesu alikuwa tayari kufa. Hapo basi Yuda na kile kikosi wakaanguka nyuma kwa mstuko mbele ya hiyo enzi. Walikuwa wamefanywa tayari kwa pigano la kumfunga mstakiwa. Basi yupo hapo akiwaelekea na heshima ya kuhani mkuu siku ya kafara akisema, “Mimi ndimi mnayemtaka”. Walianguka ardhini, na Yesu angaliweza kuondoka kwao, lakini aliendelea kusimama mbele zao.

YOHANA 18:7-8
“Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.”

Kristo aligeuza uangalizi wa washambulizi wake kwake. Wengine wao walitokea kuwakamata hata wanafunzi wake, lakini Yesu alijaribu kuwakinga, hali akiwatazama adui zake na kuwaonyesha kifua chake. Yeye ndiye Mchungaji Mwema, atoaye uhai wake kwa ajili ya kondoo; akawaagiza askari wawaachilie wafuasi wake. Heshima yake iliwasitusha, nao wakatii agizo lake. Akarudia kusema, “Ni mimi”, kana kwamba kusema, “Mimi ni Mkate wa Uzima, mimi ni Nuru ya ulimwengu, ndimi Mlango, Mchungaji Mwema, Njia, Kweli na Uzima. Mimi ndimi Mwokozi aliyeteuliwa. Kwa namna ya kibinadamu Mungu asimama mbele zenu.” Jina la “Yesu” linamaanisha, “Mungu ateua na kuokoa.” Huyu Msaidizi mtukufu alikataliwa na Wayahudi. Hawakumtaka huyu Mnazareti mnyonge awe Masihi wao.

YOHANA 18:10-11
“Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je, Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?”

Petro hakumwelewa Bwana wake au kuzingatia maneno yake. Alikuwa amelala, akaamka, bado akisinzia. Akatambua maaskari akakasirika na kufuta upanga wake, ambao Yesu alikuwa amemruhusu kuibeba. Akaiinua na kumpiga mtumishi wa Kuhani Mkuu bila agizo la Bwana wake. Sikio la yule mtumishi ilikuwa imekatwa.

Ni Yohana tu anayetueleza hilo, muda mwingi baada ya Petro kufa. Yohana anasisitiza agizo la Yesu kwa Mwanafunzi wake wa kwanza arudishe upanga wake alani, akizuia kumwaga damu zaidi, pia na kukinga wanafunzi wengine wasikamatwe.

Ndipo Yesu akasema na wanafunzi wake habari ya kikombe cha ghadhabu tukufu alichokikubali wakati wa maombi yake. Basi tunasoma hayo kama marejeo ya ndani kwa mahangaiko yake ya kiroho yaliyoendelea ndani ya nafsi ya Bwana kabla ya kufungwa kwake. Tunatambua sana kwamba, alikuwa tayari kuteswa na ghadhabu hiyo, akibeba hukumu zote ndani ya nafsi yake kwa ajili yetu. Kikombe kile kilimjia moja kwa moja kotoka kwa mkono wa Babaye. Hivyo akachukua kilichokuwa chungu mno kutoka kwa yule aliyekuwa mwenye upendo kabisa kwake. Na hiki hakuweza kukibeba isipokuwa kwa upendo, maana Baba na Mwana wako pamoja katika kuwakomboa binadamu. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee.

SALA: Tunakuabudu, Ee Baba, kwa sababu ya upendo wako unaovuka uwezo wa ufahamu wetu. Ulitoa Mwana wako kwa ajili yetu. Tunakutukuza, Ee Mwana, kwa ajili ya rehema zako na enzi na utayari wako wa kutufia. Hukutoroka bustanini, lakini kuwakinga wanafunzi wako, na mwenyewe kujitoa kwa adui zako. Tunakushukuru kwa ajili ya kujikinahi mwenyewe, kwa sababu ya wema na uaminifu wako. Asante sana.

SWALI:

  1. Nini ni maana ya Yesu kujiweka wazi mwenyewe kwa adui zake pale penye lango la bustani?

QUIZ - 6

Mpendwa msomaji, ututumie majibu sahihi kwa maswali 15 kati ya hizo 17 zinazofuata hapo chini. Ndipo tutakutumia masomo yanayofuata katika mfululizo huo.

  1. Jinsi gani Yesu alipata kuwa Mzabibu wa kweli?
  2. Kwa nini tu ndani ya Yesu na yeye ndani yetu?
  3. Jinsi gani Yesu aliwafanya wale waliokuwa watumwa wa dhambi wapate kuwa wapendwa wake?
  4. Kwa nini ulimwengu unamchukia Kristo na wapendwa wake?
  5. Jinsi gani Mungu anafariji ulimwengu, ambayo ulimsulibisha Kristo?
  6. Kwa nini dunia inawachukia wale wanaoamini ndani ya Kristo?
  7. Jambo gani Roho Mtakatifu anatenda ndani ya ulimwengu?
  8. Jinsi gani Roho Mtakatifu hufanya kazi katika maendeleo ya ulimwengu?
  9. Jinsi gani Mungu Baba anajibu maombi yetu katika jina la Yesu?
  10. Kwa nini na jinsi gani Mungu Baba anatupenda?
  11. Wazo kuu katika sehemu ya kwanza ya maombezi ya Yesu ni lipi?
  12. Ipi ni maana maalum ya kufunuliwa kwa jina la Baba kwa njia ya Yesu?
  13. Jambo gani linaonyeshwa wazi kutokana na utunzaji wetu katika jina la Baba?
  14. Jinsi gani Yesu alimwomba Baba yake atulinde na maovu?
  15. Jambo gani Yesu alitaka kwa Babaye kwa ajili ya fadhili zetu?
  16. Jumla au kiini cha sala ya maombezi alilolitamka Yesu ni nini?
  17. Ni nini maana ya Yesu kujiweka wazi mwenyewe kwa adui zake pale penye lango la bustani?

Mwishoni usisahau kuandika jina lako na anwani kamili kwenye karatasi ya QUIZ, wala si kwenye bahasha tu . Ndipo uitume kwa anwani ifuatayo:

Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 Stuttgart
Germany

Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 12:05 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)