Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 105 (Jesus intercedes for the church's unity)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
E - Maombezi ya Yesu (Yohana 17:1-26)

4. Yesu anaombea umoja wa kanisa (Yohana 17:20-26)


YOHANA 17:24
„Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ulimwengu.“

Mara sita katika sala hii ya maombezi Jesu anamtaja Mungu „Baba“, na mara moja „Mungu wa Kweli“. Kwa jina hilo la pekee alikusudia kueleza tegemeo lake mwenyewe na hamu yake kwa Mungu. Maana alikuwa mmoja pamoja na Baba tangu asili, lakini alijimwaga mwenyewe na kuwa mnyenyekevu kwa ajili ya ukombozi wetu. Hakuwa na hamu kuringa au kuwa na mali. Mara 13 alitumia maneno hayo, „wewe umenipa“. Mwana alichukua unyenyekevu kwamba, wafuasi wake, kazi yake na enzi yake yote kuwa ni zawadi toka kwa Mungu, kana kwamba hazikuwa zake hata hivyo. Naye akiwa bila hayo mwilini, alijiweka chini ya enzi na heshima ya Babaye. Uvumilivu huo ulihakikisha upatano wa kudumu, ili kwamba Mwana aliweza kutimiza mawazo ya Babaye na makusudi yake kabisa.

Kwa sababu ya huo utii kamili aliweza kutamka katika maombi yake bila ushupavu, „Nadai.“ Basi, dai hiyo ilikuwa nini iliyotamkwa na Mwana wa Mungu? Ni hilo kwamba, wafuasi wake wote popote na wakati wowote wawe pamoja naye kote alipo yeye. Hata Paulo anashuhudia kwamba, alisulibishwa pamoja na Kristo na kuzikwa naye, ili ashiriki na kufufuka kwake, na apewe kiti naye mbinguni, ili agundue na utajiri wa neema ya Mungu nyingi mno kwa ajili ya upole wa Kristo Yesu. (Rum.6:1-11; Efe. 2:4-7)

Umoja wetu na Kristo unaendelea hata ng’ambo ya mateso yake na upendo wake, na inajumlisha hata na utukufu wake. Anatamani kwa ajili yetu tuone utukufu wake na tuishi katika ushirikiano na yeye daima. Mitume walifahamu shabaha hiyo ya tumaini letu. Tutarukaruka na furaha ya milele, bila kuweza kuitamka wakati tutakapomwona kwa macho. Pia tutarudisha utukufu wake, tukibadilika katika mfano wake, kwa sababu hali ya mwangaza huo tutakuwa tumepewa katika kumwagwa wa upendo wa Mungu ndani ya mioyo yetu (Rum.5:5 na 8:29). Alishirikisha utukufu wake, kwa sababu alikuwa tukufu hata katika unyonge wa ubinadamu wake. Mitume walitambua wakiwa karibu naye kwamba, utukufu wake ulitokana na ule upendo usioweza kutingishwa kati yake yeye na Baba, hata kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. Kule kuwepo kwetu hivyo ndani ya Utatu Utakatifu ndiyo asili ya kuwepo kwetu, pia na ukombozi wetu.

YOHANA 17:25
„Baba mwenye haki, ulimwengu hakukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.“

Mungu aendelea kuwa mwenye haki na usahihi, hata kama ulimwengu hautambui. Kwa asili yeye ni mtakatifu, wala hakuna giza lolote ndani yake. Yeyote atambuaye upendo wake ndani ya Kristo, na atagundua pia kwamba, sio kosa lake ya kwamba watu hawaamini ndani ya Mwana wala kuugundua wokovu.

Lakini Kristo alimfahamu Babaye tangu milele, kwa sababu Mwana alimwona Babaye uso kwa uso. Hali yake, tabia na majina yake yote yanajulikana kwake Mwana. Pia maana za ndani zaidi ya uungu haikufichika mbele zake Yesu.

Kwa wote wanaompokea Mwana, Mungu anawapa haki ya kuwa watoto wake. Yesu aliwafunulia siri ya ubaba wa Mungu. Wale waliofanywa wapya wanatambua kwamba, Kristo alitoka kwa Mungu; hakuwa ni nabii tu au mtume, lakini tukufu, kweli kutokana na Mungu. Ukamilifu wote wa Mungu ulikuwa ndani yake kimwili. Roho atumulikia hata tutambue uungu wa Yesu ndani ya ubinadamu wake, pia tuwe na umoja naye na Baba aliyemtuma. Hivyo yeye ndiyo kiungo kati ya Mungu na binadamu.

YOHANA 17:26
„Nami nimewajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.“

Kwa ujumla, Kristo alitufundisha ufunuo wa jina la Babaye. Mafafanuzi ya wazi kabisa ni ndani ya msalaba, ambapo Baba alimtoa Mwanaye kuwa sadaka, kafara takatifu kwa ajili yetu ili tupate kushiriki haki za uwana. Roho Mtakatifu alipotujia juu yetu, tulilia, „Abba, Baba“ kutoka kwa chini kabisa ya mioyo yetu. Sala ya Bwana ndiyo taji ya sala zote, jinsi linavyomtukuza Baba, ufalme wake pia na mapenzi yake.

Tunamtambua Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kiasi kwamba, upendo unaoendelea kati ya Baba na Mwana unamwagwa na ndani yetu. Alimtaka Baba yake aumbe ukamilifu wa upendo ndani yetu. Hivyo sio Baba tu anayetujia, lakini na Yesu ambaye binafsi anatamani kudumu ndani yetu. Ndivyo alivyoomba katika maombezi yake kwamba, ukamilifu wa uungu ungetelemka chini kwetu, jinsi Yohana anavyoshuhudia katika waraka wake: Mungu ni upendo, naye akaaye katika upendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. (I.Yoh.4:16 b).

SWALI:

  1. Jumla au kiini cha sala ya maombezi alilolitamka Yesu ni nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 12:03 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)