Previous Lesson -- Next Lesson
a) Yesu na ndugu zake (Yohana 7:1-13)
YOHANA 7:1-5
“Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda , ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini.”
Makutano walishangaa jinsi Yesu alivyoshuhudia habari ya utukufu wake. Baadhi ya rafiki zake walikuwa wakitembea naye kule Yerusalemu, wakati wengi wa wafuasi wake kule Galilaya walimwacha. Wenye mawazo mafupi kwenye mji mkuu hawakutaka kuamini kwamba huyu mtu mwenye umri mdogo ndiye mfufuaji wa wafu na hakimu wa ulimwengu; Wakati huo wacha Mungu wa Galilaya walichukizwa na tazamio lake la kula mwili wake na kunywa damu yake kwamba ni lazima. Walikosa kuelewa kwamba hayo yalikuwa ni ishara za Ushirika Mtakatifu.
Kule Yerusalemu baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu tayari waliamua kumwua Yesu. Walituma agizo la kumfunga, tena wakawatisha waumini wa kiyahudi kwamba watatengwa na Sinagogi na hivyo kukatwa na baraka za Mungu, wakinang’ania kumfuata Yesu. Wapelelezi toka barazani wakizunguka Galilaya wakaanza kumtafuta na kumwulizia Yesu. Basi haishangazi kwamba, makutano waliondoka kwake, maana chaguo lao sasa ikataka kuleta mateso toka kwa viongozi wa taifa, au wokovu wa mashaka ambao labda utapatikana kwake Yesu. Hivyo walichagua ya karibu kuliko ya mbeleni, wakipendelea usalama wao zaidi kuliko zawadi kutoka kwa Mungu.
Ndugu zake Yesu walihofia matazamio ya kufukuzwa kutoka maisha ya jamii ya taifa lao. Basi wakajitenga naye wazi mbele za watu, ili wasije wakaharimishwa na sinagogi ya Wayahudi (Marko 6:3). Zaidi ya hayo wakamtaka aondoke Galilaya, ili waweze kutupa wajibu wao kwa ajili yake, pengine kwa kumsukuma kwa hatua ya kufunua utukufu wake kule Yerusalemu. Ingawa walikuwa wameishi naye kwa miaka, hawakuamini katika uungu wake, wakihesabia upendo na wema wake kuwa namna yake ya kawaida. – Ni huzuni, hata leo waumini wengi wanakubali kumheshimu Yesu kwa upendo wake, lakini bila kufahamu kiini cha ukweli wake.
Ndugu zake Yesu waliona miujiza yake. Hata hivyo, hawakuamini kwamba ndiye Masihi ajaye, ambaye kwake kila goti lipigwe. Walijisikia vibaya kuhusu mshuko wa mwenendo wake na ya kwamba, hata umati wa watu waliondoka kwake. Walimjaribu Yesu jinsi Shetani alivyomjaribu mapema jangwani, alipomtaka Yesu aonyeshe utukufu wake hekaluni mbele za watu walioabudu pale, ili awakumbe kwa kitendo cha kuwashangaza. Ila Yesu hakuwa na nia ya kujikuza, alichagua unyenyekevu na udhaifu wa hali ya kibinadamu, wala hakutamani kupata waumini kwa maonyesho ya ajabu.
YOHANA 7:6-9
“Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.”
Watu huwa ni wenye kiburi, kwa sababu roho ya ibilisi aliwafuja. Kiburi ndiyo dalili ya ugonjwa wa kiroho na alama ya maradhi ya hali ya utu. Kwa kweli, mtu yeyote kulingana na Mungu ni mdogo sana, mdhaifu na lazima afe. Mtu hujaribu kufunika udhaifu wake kwa kujivisha kwa kung’aa. Mwenye kiburi anajiona mwenyewe kama mungu mdodo, awezaye kufanya lolote apendalo au asifanye chochote. Anapanga siku zake na njia zake kwa kutokumjali Mungu. Kwa asili, yeye anakuwa mwasi dhidi ya Mwumbaji wake. Mtu hujipenda mwenyewe, wala si Mungu; hutukuza jina lake, wala hakuzi jina la Baba wa mbinguni.
Sio mawazo na makusudi tu za watu ni mbovu, bali na matendo yao kwa jumla. Hivyo yeyote aishiye pasipo Bwana wake, anaishi kinyume chake. Karibu mambo yote ya kubuni na mavumbuzi ya kisayansi, hata na taratibu za kisiasa na desturi za ki-filosofia, zote zahusika na eneo la dhambi. Ndani yake mbegu za kifo zimo.
Kristo alionyesha kwamba, ulimwengu ulimchukia. Hakuja kutenda yale aliyopendelea mwenyewe. Yeye ni mmoja na Baba na kutenda kazi katika ushirikiano na yeye. Hata wacha Mungu walimwona kama kikwazo, maana upendo aliyowaonyesha haikuwa ya kisheria, bali tukufu. Walimchukia kwa sababu kuwepo kwake kuliondoa kabisa dai yao ya kuwa wenye haki wao wenyewe.
Ndugu zake Kristo walimkataa Roho Mtakatifu, kinyume walikuwa wamejaa roho ya kidunia, na hivyo kwa jumla walilingana na Mafarisayo. Upungufu wao wa imani ulithibitisha kwamba roho wa upendo wa Mungu haikutawala ndani yao; ila roho mwingine uliwaongoza, roho wa kuringa na kuasi kinyume cha Mungu. Walijidanganya wenyewe, wakiamini thamani ya matendo yao mema.
YOHANA 7:10-13
“Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi, bali kana kwamba kwa siri. Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? Kukawa na manung’onoko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.”
Kila mwaka Wayahudi walikuwa wakisherekea sikukuu ya Vibanda kwa furaha. Kwa matawi ya miti walikuwa wanatengeneza vibanda kwa kulala ndani, wakizipanga juu ya dari tambarare za nyumba zao au pembeni ya barabara. Watu wakitembeleana na kufurahia vyakula vitamu. Sikukuu hii ni ya kumshukuru Mungu kwa kujaliwa mavuno mazuri. Vibanda hivi na mahema ziliwakumbusha safari zao za kupitia jangwani: Wakati ule walikuwa hawana mji wa kukaa hapa duniani.
Yesu hakushiriki kwenye uchangamfu wa sikukuu hii, maana alianza kudhulumiwa pamoja na wanafunzi wake. Aliwaacha ndugu zake mwenyewe waende zao. Baadaye naye alienda Yerusalemu akasema kwa heri kwa Galilaya, ambapo ni nyumbani kwake hapo duniani. Hapo nafasi ya kudanganywa ilikuwa imemfikia. Kilele cha historia - kifo chake kwa ajili ya wokovu wetu kutoka kwa ghadhabu tukufu.
Wayahudi walikuwa na maoni tofauti juu ya Yesu. Baadhi yao walimwona kwamba ametoka kwa Mungu, mtu mwema na mtengenezaji. Wengine walimhisi kwamba anawaongoza watu wapotee na kustahili kufa; pia kuwepo kwake kungeleta ghadhabu ya Mungu juu yao na kuharibu taratibu zao za sikukuu. Baraza la Sanhedrin walikuwa wametoa agizo na kuieneza kwa watu, wakihisi kwamba wafuasi wake wangesita kuendelea kumfuata. Baada ya hayo hakuna aliyethubutu tena kusema wazi habari za Yesu.
SALA: Bwana Yesu, twakushukuru kwa uvumilivu na utii wako kwa Mungu. Utuweke huru na matazamio ya kidunia, ili Roho Mtakatifu aweze kutujalia. Utukinge na njia bovu, na utuponye na umimi uilyo ndani yetu, ili tuweze kukutumikia jinsi unavyostahili.'
SWALI:
- Kwa nini dunia ulikuwa unamchukia Yesu?