Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 049 (Disparate views on Jesus)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

b) Maoni tofauti tofauti juu ya Yesu kati ya watu na kwenye Baraza Kuu (Yohana 7:14-53)


YOHANA 7:14-18
“Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? Basi Yesu akawajibu,akisema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda, mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzu, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyenipeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu”.

Yesu hakuogopa kifo au kuteswa na adui zake. Alisonga mbele katika amani na mapenzi ya Baba yake akienda Yerusalemu, kwa siri, katikati ya sikukuu. Lakini pale hakujificha, bali alienda kwenye ua la hekalu, akifundisha Injili yake kwa ujasiri, kama mwalimu mwenye Shahada. Watu walisikia kama kwamba Mungu alikuwa amesema nao moja kwa moja. Hivyo wakaanza kuulizana: Namna gani huyu mtu mwenye umri mdogo anayo mawazo ya ki-theologia ya ndani sana? Hakusoma chini ya mwalimu wa Maandiko. Jinsi gani huyu seremala bila masomo ya chuo kikuu anawezaje kutufahamisha mambo kuhusu ukweli kamili juu ya Mungu?

Jesu alijibu kana kwamba alisema, „Kweli, ninayo mafundisho, nami ni mwalimu wa ukweli. Zaidi ya hapo mimi ndimi Neno la Mungu. Kila wazo na mapenzi yake Mungu imo ndani yangu. Mafundisho yangu sio ya kwangu; mimi mwenyewe ndiyo sauti ya Mungu. Yeye huishi ndani yangu, Baba yangu ndiye mwenye kunifundisha. Nafahamu ukamilifu wa mawazo yake, mipango na makusudi yake, pia na uweza wake. Mimi sikuja na mawazo yangu ya binafsi, maana mawazo yake Mungu kipekee ni ya kweli. Mimi nakamilisha ufunuo wake ambapo bado haijawa wazi“.

Hivyo alimtukuza Baba yake na kujinyenyekeza chini yake, akijiita Mtume wa Mungu. Yeye hakujituma kwa mapenzi yake, bali alikuja katika jina la Babaye, hali amejaa enzi tukufu. Basi Yesu anakuwa ni Mwana wa Mungu na Mtume wake wakati mmoja, akistahili usikivu wetu, imani yetu na kuabudiwa kama Baba mwenyewe.

Ili kuhimiza imani ndani yake kutoka kwa Wayahudi, aliwaonyesha nja ya wazi kuwahakikishia kwamba, mafundisho yake yanapatana na mapenzi ya Mungu. Hivyo, jambo gani ndiyo hakikisho thabiti kuhusu ukweli wa mafundisho ya Yesu na nafsi yake? Alisema: „Mjitahidi kutenda kwa usawa na Injili yangu, ndipo mtagundua ukuu wake. Linganisheni maneno ya Kristo mstari kwa mstari, nanyi mtaona kwamba maneno yangu sio ya kibinadamu, lakini tukufu.“

Jaribu la kufuata mafundisho ya Kristo linahitaji kwanza nia yako. Je, unayapenda yale anayoyapenda yeye? Bila kibali hicho cha mapenzi yako na mapenzi ya Mungu hutaelewa ufahamu wa kweli wa Bwana. Ambapo mapenzi yako yataanza kupatana na yake, yaani ya Kristo, hapo utaanza kupanda kwenye daraja ya juu na mpya ya utambuzi - utamtambua Mungu jinsi alivyo.

Yeyote anayejizoeza kutenda mapenzi ya Baba, jinsi Yesu alivyotufundisha, atatambua ule ufa pana kati ya Injili na sheria. Bwana wetu hakuweka tu hivi hivi mzigo mzito mabegani mwetu, bali wakati uo huo anatujalia nguvu unaohitajika kuibeba. Utawezeshwa kutenda mapenzi yake kwa furaha kweli. Yeyote anayekubali maagizo ya Kristo, atapokea uwezo wa kuishi kufuatana na upendo wake. Mafundisho yake hayatatufikisha kwenye hali ya kushindwa, jinsi ilivyokuwa wakati wa sheria za Musa, bali kuishi katika ukamilifu wa rehema ya Mungu. Yeye apendaye kufuata mapenzi ya Mungu yalivyofunuliwa katika mafundisho ya Kristo, binafsi ataunganishwa na Mungu, na hivyo kutambua kwamba, Kristo siye mmoja wa waalimu wa kibinadamu, bali yeye ni Neno la Mungu mwilini. Yeye haji na maneno matupu ya ki-filosofia, bali huja na msamaha wa dhambi kwanza, ndipo anatuhakikishia na uwezo kutokana na uhai wa Mungu.

YOHANA 7:19-20
Je, Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetaka kukuua?”

Mwenendo wa Kristo katika utakatifu ulimwezesha kuwaambia Wayahudi: „Mlipokea sheria, lakini hakuna hata mmoja anayeifuata ipasavyo!“ Tamko hili lilichoma moyo wa taifa la Wayahudi, kuwahakikishia kwamba hakuna kabisa kati ya watu wa Agano la Kale aliyetimiza matakwa ya sheria. Yeyote anayevunja agizo hata moja anayo hatia ya yote. Hasira ya Mungu itaendelea juu yake. Kwa tangazo hilo Yesu alifuta madai ya Wayahudi ya kuwa wenye haki, akawaonyesha kwamba jitihada na bidii za kisheria ni kujidanganya tu. Ndipo aliwatangazia kwamba anatambua nia ya viongozi wao kumwangamiza. Hakuna kinachojificha mbele ya Yesu. Aliwaonya wasikilizaji wake dhidi ya bidii yoyote ya juu juu tu, tena akawakazia pia gharama ya kumfuata yeye.

Pamoja na hayo akawaulitza: “Kwa nini mwataka kuniua?” Mkutano wakastaajabu kwa tamko la Kristo, baada ya kuonywa naye kwamba hakuna hata mmoja wao kuwa mwenye haki. Jibu lao lilikuwa ni kufunika hila zao: “Hapana, hasha, - nani ataka kukuua? Mungu atulinde!” Hata baadhi yao wakahisi kwamba roho mchafu ilimwingia. Walikuwa vipofu katika hasira zao, nao hawakuweza kutofautisha Roho Mtakatifu na roho mbaya. Walipoteza usikivu wowote kwa ajili ya ufahamu wa upendo wa Mungu.

SWALI:

  1. Kuna thibitisho gani kwamba Injili inatoka kwa Mungu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:07 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)