Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 019 (The first six disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

3. Wanafunzi sita wa kwanza (Yohana 1:35-51)


YOHANA 1:47-51
47 “Basi Yesu akamwona Nathlanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, “Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake”. 48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akamjibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 49 Nathanieli akamjibu, Rabi (Mwalimu), wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israel! 50 Yesu akamjibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuonachini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya! 51 Akamwambia, Amin, amin nawaambia, mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu”.

Nathanaeli alistaajabu mno alipogundua ya kwamba, Yesu alikuwa ameangalia ndani ya utu wake na kumfahamu. Nathanaeli alikuwa mwumini wa namna ya Agano la Kale, kwa kuwa amekiri dhambi zake kwa Mbatizaji na akatamani ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote. Hali hii haikuwa uadilifu wa kibinafsi, bali mwelekeo wa moyo uliyovunjika kwa ajili ya dhambi, ukimlilia Mungu amtume Masihi, ambaye atakuwa Mwokozi wake.

Yesu alisikia ombi hili na akamwona mwombaji akiwa mbali kidogo, akipiga magoti chini ya kivuli cha mti. Nguvu hii inayothibitisha mambo yanayofichwanafsini mwa mtu, ndiyo utambuzi tukufu.

Yesu hakumkataa, bali akamhesabia haki akimweleza kama mwumini wa kuigwaaliyeweka imani yake kwenye msingi wa Agano la Kale, huku akitazamia kuja kwa Kristo.

Maelezo ya Kristo yalifuta shaka lolote la Nathanaeli. Alijitoa kwake Yesu na kumheshimu kwa kutumia majina ya kibiblia yanayomhusu Masihi: “Mwana wa Mungu” na “Mfalme wa Israeli”. Matamshi kama haya yakitamkwa hadharani yangemweka Nathanaeli kwenye hatari ya kufa. Kwa kuwa waandishi na wajumbe wa baraza la wayahudi walikataa kwamba Mungu angekuwa na mwana. Matamshi kama haya yangechukuliwa kama kukufuru.Tena mtu kujidai kuwa mfalme wa Israeli kungemfanya kuhukumiwa na Herode,aliyekuwa Mfalme wakati ule, pia hata kushikwa na utawala wa Kirumi. Kwa hiyo mwumini huyu wa kweli alionyesha kushika sana unabii wa maana uliyofunuliwa na manabii. Aliogopa Mungu kuliko mwanadamu, hata akamheshimu kwa kutumia neon la “Baba” bila kujali gharama yoyote.

Hakuna katika wale wanafunzi wa kwanza aliyempa Kristo majina kama haya, kama yaliyotajwa na Nathanaeli. Kiajabu, Kristo hakukataa lolote katika haya majina, bali akainua ufahamu wake kwa kumwonyesha habari ya kufunguka kwa mbingu: Mazingara ya Kristo yalikuwa yamezungukwa na malaika wasioonekana, wakipaa juu mbinguni, wakionyesha miujiza yake kwa Baba, ndipo wakirudi kwa Mwana, hali mikono yao ikifurika baraka. -Hivyo na ufunuo waYakobo wa zamani ukatimilika, kwa maana ndani ya Jesu ukamilifu wa baraka unapatikana. - Kama vile Mtume Paulo alivyoandika kwa Waefeso 1: 3: “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.”Kuanzia kwa kuzaliwa kwake Kristo na ubatizo wake mbingu iliendelea kuwa wazi. Kabla ya hapo ilifungwa kwa ajili ya ghadhabu ya Mungu, kukiwa na malaika wakilinda milango yake, wenye mapanga yaliochomolewa tayari. Lango linaloelekea kwa Mungu sasa limefunguliwa kwa kazi ya Kristo.

Ndipo kwa mara ya kwanza Yohana anatumia tamko lililo kawaida kwa Kristo “Amin, aminnawaambia”. Ukweli wa wakati huu wa neema ulikuwa wa juu mno, kiasi cha kutoelekwa na mwanadamu, na hata hivyo mwanadamu anauhitaji kuwa msingi tukufu wa imani yake mpya. Kwa kuwa kila mara Yesu anaporudia tamko hili, sisi tunapaswa kutulia na kutafakari sana juu ya makusundi yake,maanaa lile linalofuata tamko hilo ni ufunuo wa kiroho, ambao uko unapita sana mafikiria yetu.

Baada ya kujitambulisha hivyo, Kristo alisahihisha ushuhuda wa Nathanaeli kama tahadhari kuhusu mateso ambayo yangewezayakaelekea kwake na kwa wafuasi wake wapya. Yesu hakusema, Mimi ni mfalme mtarajiwa, Mwana wa Mungu, lakini alijiita “Mwana wa Adamu”. Hili ndilo jina ambalo Yesu alilitumia mara nyingi kujieleza mwenyewe. Kuingia kwake mwilini kulikuwakuharibu kwake kwa ajabu sana, maana aliye Mungu akawa kama sisi –hii ni mwujiza mkuu sana- Mwana wa Mungu kuwa mwanadamu, ili afe kama Mwana-Kondoo wa Mungu kwa ajili yetu.

Kwa njia nyingine hili jina “Mwana wa Adamu” linaelekeza kwa fumbo linalotajwa katika kitabu cha Danieli. Pale Mungu alimkabidhi Mwana wa Adamu kufanya hukumu. Nathanaeli alitambua kwamba Yesu hakuwa ni Mfalme na Mwana wa pekee tu, lakini pia kuwa hakimu wa ulimwengu- Mtukufu ndani ya maumbile ya kibinadamu. Hivyo Yesu akamwongoza mwumini huyu mzito kwenye hali ya juu sana kiimani. Imani kama hii haikuwa rahisi, maana kwa sura ya nje Yesu alikuwa kijana wa vijijini tu. Lakini kwa imani mwanafunzi huyu aliona ule utukufu uliofichwa ndani yake-na mbingu ikifunguka juu yake.

SALA: Tunakuabudu,Mwana wa Mungu na hakimu wa wote. Hatustahili chochote ila ghadhabu,lakini tunaomba msamaha kutokana na neema yako, na pia huruma kwa marafiki zetu. Mwaga baraka zako kwa wote wanaomtafuta Mungu, ili waweze kukuona, wakufahamu na wakupende, ili wakutegemee na kukua katika ufahamu na matumaini.

SWALI:

  1. Ni uhusiano gani ulioko kati ya majina ya heshima ya Yesu ya “Mwana wa Mungu” na “Mwana wa Adamu”?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)