Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 018 (The first six disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

3. Wanafunzi sita wa kwanza (Yohana 1:35-51)


YOHANA 1:43-46
43 “Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia “Nifuate”. 44 Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45 Filipo akamwona Nathanaeli akamwambia, “Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti”. 46 Nathanaeli akamwambia, “Laweza neno jema kutoka Nazareti?”Filipo akamwambia, Njoo uone”.

Kwenye vifungu vilivyotangulia tumesoma mambo yaliotendeka kwa siku nne mfululizo. Siku ya kwanza ule ujumbe ulikuja kutoka Yerusalemu, siku ya pili Yohana alimtangaza Yesu kuwa Mwana-Kondoo wa Mungu. Siku ya tatu Yesu aliwaita wanafunzi wanne. Siku ya nne aliwaita Filipo na Nathanaeli wajiunge na shirika lawanafunzi.

Yesu ndiye aliyemtafuta Filipo. Bila shaka Filipo amesikia mapema kutoka kwa Mbatizajiya kwamba Yesu alikwisha kuwa pamoja nao. Alistaajabu wakati Yohana Mbatizaji alipoelekeza kwa Yesu kwamba ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu. Filipo hakuthubutu kumkaribia Yesu. Alitamani kumfahamu Bwana, lakini alijiona kwamba hangekubalika kushiriki na huyu Mtukufu. Kwa hiyo Yesu alienda kwake, akaondoa wasiwasi wake akamwambia ainuke na amfuate.

Yesu alikuwa na haki kuchagua watu kwa ajili yake, maana aliwaumba, akawapenda na kuwaokoa. Sio sisi wenyewe tunaochagua kumkubali, ila yeye anatuona kwanza. Yeye alitutafuta, akatupata na kutuita kwenda katika huduma yake.

Haiwezekani kufufuata bila wito, hakuna huduma ya maana bila agizo toka kwa Yesu. Yeyote anayehudumu bila kuchaguliwa kwa shabaha hiyo katika ufalme wa Mungu, atajisumbua mwenyewe na wengine nao. Lakini yeyote amsikiaye Kristo na kuwa tayari kumtii, atafurahia jinsi Kristo atakavyomwongoza kwa upole. Yesu atawajibika kwa yote maishani mwake wakati wowote.

Filipo mapema aliinuka kupeleka injili. Alipompata rafiki yake Nathanaeli akamjulisha hii habari njema. Akiitamka kwa namna ya washiriki waaminio: “TumemwonaMasihi”, sio “Mimi nimemwona”; hivyo alijijumlisha kwa unyenyekevu na waumini wenzake wanavyokiri.

Inaonekana kwamba, Yesu aliwajulisha wanafunzi wake kuhusu namna ya utume wake. Yusufu alikuwa Baba yake kwa kumlea na kumtunza. Yesu hakuwaambia lolote kuhusu kuzaliwa kwakeBethlehemu. Na wakati ule wanafunzi wake hawakujua chochote huhusu mahali pa kuzaliwa kwake.

Nathanaeli alikuwa msomi kwa kuelewa maandiko. Kwa hiyo alitafuta kwenye vitabu vya Musa na Manabii, na alikuwa amejifunza kuhusu ahadi zilizomlenga Kristo. Aligundua ya kwamba anayetarajiwa angezaliwa Bethlehemu, wa ukoo wa Daudi, na angekuwa mfalme kwa watu wake. Basi Nathanaelil aliona vigumu kukubali ya kwamba Masihi azaliwe katika mji ndogo ambayo haikutajwa kwenye Agano la Kale, na hakuna unabii uliohusishwa na Nazareti. Nathanaeli alikumbuka kwamba mji huu wa Galilaya ulikuwa eneo la kundi la waasi waliofanya mambo ya ukaidi na watu waliotetea imani yao dhidi ya utawala wa Kirumi. Maasi haya yalipigwa vikali na damu nyingi ikamwagika.

Mambo hayo hayakumsumbua Filipo. Furaha yake ilikuwa kubwa sana kwa kumtambua Kristo. Shauku yake ilikuwa ikashinda mashaka ya Nathanaeli. Akasema bila kuhojiana naye “Njoo uone”. - Tamko kama hilo kwa uinjilisti ndilo msingi wa kufaa kwa utambuzi wa kweli, na litaendelea kuelekeza kwa neno hilo “Njoo uone”. Usizushe mabishano kumhusu Yesu, lakini uchangamke kwa nguvu na ushirika wake. Ushuhuda wetu hauwekwi kwenye mawazo tunayotunga, lakini ni kwa nafsi ya mtu ambaye kweli ndiye Bwana na Mwokozi.

SALA: Ewe mpendwa Bwana Yesu, asante sana kwa furaha inayojaa mioyo yetu, inayotusukuma katika uzuri wa ushirika wako, ili tuwaongoze wengine kwako. Tupe hamu ya kuhubiri kwa unyenyekevuna upendo. Utusamehe woga wowote, kukawia kwetu na kujidharau kwa kulitangaza jina lako kwa ujasiri.

SWALI:

  1. Kwa njia gani wanafunzi wa kwanza walitangaza jina la Yesu kwa watu wengine?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)