Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 020 (Jesus' first miracle)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

4. Mwujiza wa kwanza wa Yesu kwenye Arusi ya Kana (Yohana 2:1–12)


YOHANA 2:1-10
1 “Na siku ya tatu palikuwa na Arusi huko Kana ya Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamojana wanafunzi wake. 3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, “Hawana divai”. 4 Yesu akamwambia, “Mama, tuna nini wewe na mimi? Saa yangu haijawadia”. 5 Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio (kipimo) mbili au tatu. 7 Yesu akawaambia, “Jalizeni mabalasi maji.” 8 Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa tekeni mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. 9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), 10 yule mkuu wa meza alimwita Bwana Arusi, akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njemahata sasa!”

Yesu aliwaongoza wanafunzi wake kutoka kwa bonde la toba kwenye mazingara ya Mbatizaji kwenye korongo la Yordani, wapandie milima ya Galilaya na kushiriki kwenye furaha ya arusi. Safari hii ya kilomitamia moja inatuonyesha mabadilikomakubwa kati ya maagano mawili. Hakuna tena waumini waishi kwenye kivuli cha sheria, bali kwenye furaha ya kupewa haki kwa Yesu aliye kamajua linalochomoza na aliye mgawaji wa amani.

Yesu hakuwa mwenye kujinyima vyakula fulani(Ascetic) kama Mbatizaji alivyokuwa. Kwa sababu hiyo kuelekea kwake Yesu na wanafunzi wake kwenye furaha ya kawaida ya sikukuu ilikuwa kama mwujiiza kipekee. Hakukataza divai, kwa kuwa alifundisha ya kwamba sio kile kinachoingia mwilini kinamharibu, bali ni mawazo maovu yanayotaka moyoni ndiyo yanayomharibu mtu. Wala Yesu hakukataa maisha ya kujinyima vyakula au furaha fulani, lakini alifundisha ya kwamba mambo haya yako na maana ndogo tu. Mioyo yetu potovu huhitaji umbo mpya na kuzaliwa kwa upya. Biblia linalokataa ni ulevi wa pombe na kutawaliwa na vileo.

Wanafunzi waliungana na Yesu kwenye sherehe, wakati Nathanieli mwenyewe alikuwa mwenyeji wa Kana (21:2). Inaonekana mamake Yesu alikuwa anahusiana na familia ya Bwana Arusi. Inadhaniwa kwamba Yusufu alikuwa amekwisha kuaga dunia. Mariamu alikuwa mjane wakati huo, na Yesu alikuwa anashughulika kama kifungua mimba katika familia yake.

Kwa hiyo mama yake alimwelekea, ili kupata msaada kwa upungufu wa nduguze. Tangu atoke Yordani Yesu hakuwa mtu wa kawaida tena, lakini hali amebadilishwa na Roho Mtakatifu akaelekea kutokamambo ya kawaida ili amtumikie Mungu tu -wito ambao wanafunzi wake wangemfuata.

Mariamu alimtegemea kijana wake, maana alielewa utunzi na upendo wake. Basi, upendo wake ukatokeza mwujiza wa kwanza kwa mikono ya Yesu. Imani katika upendo wa Yesu inatembeza mkono wa Mungu. Mama aliwashauri watumishi watende kulingana na vile Yesu atakavyowaambia. Alikuwa na hakika ya kwamba atasaidia kwa njia hii aunyingine.

Maneno yake kwa watumishi hadi leo yanatumika kama usemi kwa waumini wa mashirika yote “Lolote atakalowaambia fanyeni”!Kwa vyovyote umtegemee Kristo peke yake; utiifu kwa neno la Yesu hutokeza miujiza mingi mikubwa.

Mabalasi ya desturi ya utakaso,makubwa na tupu, yenye ujazo wa lita mia sita yakajazwa. Hii inaonyesha ya kwamba wageni walitumiakiasi kikubwa cha maji kwa kusafishwa. Utakaso wa tofauti huhitajika wakati Yesu akiwa karibu. Hakuna mtu awezaye kushiriki kwenye Arusi ya Mwana Kondoo mpaka awe ameoshwa kikamilifu.

Hata hivyo wakati huu utakaso haukuwa jambo la dharura kwa Kristo. Alijua kusherekea kwa Arusi lazima kuendelea mbele. Kwa unyenyekevu Yesu aligeuza maji ya utakaso kuwadivai tamu. Jinsi gani jambo hili lilivyotendeka hatujui. Lakini tunafahamu kutokana na tendo hili ya kwamba damu yake iliyomwagika inatosha kwa utakaso wa washiriki wote katika Arusi ya Mwana-Kondoo. Hapo hakuna ruhusa yoyote ya ulevi.Roho Mtakatifu hawezi kuruhusukunywa kupita kiasi. Lakini utoaji wa divai tamu kwa ukarimu inatoa mfano wa wingiuisio na mwisho wa msamaha wa Kristo kwa ajili ya dhambi za wanadamu. - Heri sisi sote tuwe tukishiriki furaha za mbinguni! Wote huchukua kwa shukrani mkate na divai kwenye ushirika wa meza ya Bwana, ambazo niishara ya kuwepo kwa Kristo kati yetu-tukijaliwa msamaha na tunapopumzika katika furaha yake.

YOHANA 2:11-12
11 “Huo ni mwanzo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya hayo, akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake,wakakaa huko siku si nyingi.”

Wanafunzi wake walishangazwa na uwezo wa Kristo wa ajabu. Walitambua enzi yake juu ya sheria za asili za maumbile. Waliona utukufu wake na kuamini kwamba Mungu alimtuma. Hayo yakawapelekeka kwa hali ya kumtegemea kabisa. Imani inahitaji muda wa kukua na utiifu kwa kuelewa vema. -Unapothubutu kusomea vema kazi zake Yesu, na ukichimba ndani ya matamshi yake, ndipo utagundua ukuu wa nafsi yake.

Yesu aliondoka kwa familia yake, akawa huru na majukumu ya duniaili amtumikie Mungu. Hata hivyo uhusiano na mama yake na nduguze uliendelea. Kwa muda fulani waliendelea kusafari pamoja na wanafunzi wake. Ndugu zake walienda naye Kapenaumu, mji mkuu kando ya ziwa Tiberia. Wanafunzi wake hata hivyo walimtegemea nafsini mwao, wala sio kwa ajili ya ile ishara ya Kana tu. Tangu hapo aliambatana naye kabisa kwa wakati wowote mbeleni.

SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa kuwa umetuita kwenye Arusi, ili tuambatane nawe kwenye furaha ya ushirikiano na wewe. Utusamehe makosa yetu na kutujalia Roho wako Mtakatifu. Tutaambatana nawe na kudumu katika uadilifu na usafi, jinsi wewe ulivyofanya na kujitoa kabisa kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengi.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu aliwapeleka wanafunzi wake kwenye arusi?

Mfululizo wa Maswali

Mpendwa msomaji, ututumie majibu sahihi 20 kutokana na maswali haya 24. Ndipo na sisi tutakutumia mafuatano ya mfululizo wa masomo haya.

  1. Ni nani aliyeandika injili hii ya nne?
  2. Niuhusiano gani ulioko kati ya injili ya nne na zile injili tatu za mwanzoni?
  3. Injili ya Yohana inayo lengo gani?
  4. Injili hii ya pekee iliandikiwa kwa wakina nani?
  5. Inawezekanaje kugawa injili hii ukiipanga kulingana na mambo kimafundisho?
  6. Ni neno gani ambalo limerudiwa tena na tena kwenye mstari wa kwanza sura ya kwanzaya Yohana na maana yake ni nini?
  7. Ni sifa gani 6 za Kristo ambazo Yohana anazoonyesha mwanzoni mwa injili yake?
  8. Ni tofauti gani ilioko kati ya nuru na giza kwa maana ya kiroho ya maneno haya?
  9. Ni malengo gani makuu yaliyoko katika huduma ya Yohana Mbatizaji?
  10. Ni husiano gani ulioko kati ya nuru ya Kristo na giza la dunia ?
  11. Ni yapi wanayoyapata wale wanaomkubali na kumwamini Kristo?
  12. Maana ya kufanyika mwili kwa Kristo ni nini?
  13. Ni nini maana ya ukamilifu wa Kristo?
  14. Ni fikira gani mpya Kristo aliyoleta kwetu duniani?
  15. Ni nini shabaha ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe kutoka baraza kuu la dini yaWayahudi?
  16. Ni jinsi gani Mbatizaji alivyowaita watu kutengeneza njia ya Bwana?
  17. Ni nini ilikuwa kilele cha ushuhuda wa Yohana Mbatizaji kwa Yesu mbele ya wajumbewa baraza la wazee wa Wayahudiiitwayo “Sanhedrin”?
  18. Ni nini maana ya „Mwana-Kondoo wa Mungu“?
  19. Ni kwa nini Yesu alipata kuwa mwenye kugawa Roho Mtakatifu?
  20. Ni kwa nini wanafunzi wale wawiliwaliamua kumfuata Yesu?
  21. Ni kwa njia gani wanafunzi wa kwanza walitangaza jina la Yesu?
  22. Ni kwa njia gani wanafunzi wa kwanza walitangaza jina la Yesu kwa watu wengine?
  23. Kuna husiano gani uliyo kati ya majina “Mwana wa Mungu” na “Mwana wa Adamu”?
  24. Ni kwa nini Yesu aliwapeleka wanafunzi wake kwenye Arusi?

Ututumie jina na anwani yako, hali imeandikwa wazi, pamoja na majibu yako ukituandikia kwa anwani hii:

Waters of Life,
P.O.Box600 513
70305 STUTTGART
GERMANY

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)