Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 025 (We are Justified by Faith in Christ)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
B - Njia Mpya Ya Kuhesabiwa Haki Kwa Imani Iko Wazi Kwa Wanadamu Wote (Warumi 3:21 - 4:22)

2. Tumehesabiwa haki kwa imani katika Kristo (Warumi 3:27-31)


WARUMI 3:27-28
"27 Ku wapi basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya Imani. 28 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo mateno ya sheria.”

Kuhesabiwa haki kwa ulimwengu na upatanisho wetu na Mungu yamekamilishwa msalabani. Hata hivyo, mwanadamu anapewa haki tu kwa imani. Neno la “Imani” tunalisoma mara tisa katika mistari ya 21 hadi 31, ambamo mtume anashuhudia kwamba, unahesabiwa haki tu kwa imani yako iliyo hai.

Taratibu hii ndiyo alama ya badiliko kamili katika imani ya dini zote na filosofia zote, maana Mungu amekwisha kuwasamehe wanadamu wote dhambi zao bila kuwaadhibu. Kwa hiyo, taratibu za ulimwengu kuhusu neema yake, bidii, thawabu, matendo mema, na kufuata sheria, hayo yote yanachakaa, maana Mungu ametupatanisha bure, alitubeba ndani ya eneo la neema yake, pia na kutuweka huru na laana ya sheria. Wewe utaendelea kuwa na dhambi, mbali na kufunga kwako, kutoa sadaka na kumcha Mungu, usipokubali damu na uadilifu wa Kristo kwa imani kabisa na kwa shukrani. Wewe huwezi kuongeza lolote ndani ya hatua hizo takatifu za kutengeneza haki. Jambo hilo lakujia kama zawadi kutoka kwa Mungu. Yeye amekuhesabia haki kamili, si kwa sababu ya unyofu wako au kutenda haki kwako, bali kwa sababu damu ya Kristo imekusafisha katika dhamiri yako ya ndani. Loo, ni neema ya kushangaza namna gani !

Kukubali kwako kwa neema hii, shukrani yako kwa ajili ya hayo, na umoja wako na huyu Mtoaji ndiyo imani hasa. Huyu Msulibishwa ndiye zawadi ya Mungu kwetu sisi wahalifu. Ndani yake, Mwumbaji hukujia wewe na kukusafisha, akijitoa mwenyewe kwako, uliye mhalifu aliyefanywa haki. Haya basi, shikamana na Kristo, kwa njia ya maombi na uaminifu, ili haki yake iliyo na nguvu kamili ipate kuimarika ndani yako. Ujitoe kabisa kwake katika kutambua kabisa upendo wake.

Imani humfanya mwenye dhambi kuhesabiwa haki. Jambo hilo linabadilisha wazo la ustadi wa akili yake, na kuweka mwisho wa namna zote za kujifanya haki mwenewe, kujiokoa mwenyewe na kujivuna, maana ndani ya Kristo twafahamu kwamba, tu wajinga, waovu, wakorofi na maskini. Hapana wokovu wowote isipokuwa mkononi mwa Mungu mwenye Rehema. Wewe huwezi kukubalika kwa urithi, wala kwa elimu ya juu, au uraia wako wa pekee, kwa sababu huwezi kuokolewa kwa urithi wako, shahada zako za elimu, au vipawa vya pekee, lakini kwa imani yako ndani ya Kristo. Basi, ujitoe kabisa kwake Mwana wa Mungu, na uingie ndani ya agano lake jipya, kwa sababu maisha yako bila yeye, itadumu katika hali ya kifo na dhambi, lakini ndani yake utapata kuwa na utukufu kweli, na haki yako itaendelea daima. Kweli, hakuna kabisa njia nyingine ya kumpendeza Mungu, ila tu kwa kukubali damu ya Kristo na kuendelea ndani yake. Mungu anakuvisha haki yake, basi uamini ndani yake, maana imani pekee inakufanya kuwa mshiriki wa haki zote na nguvu zote pia zilizo za baraka ya Kristo.

WARUMI 3:29-31
"29 Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; 30 kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia iyo hiyo. 31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo, twaithibitisha sheria.”

Paulo aliandika waraka huu wa kipekee kwa kanisa la Rumi. Alipomaliza kueleza njia ya kupewa haki kwa nguvu na kwa kifupi, alisikia rohoni mwake makatazo fulani:

Wayunani walisema: „Ikiwa kifo cha Kristo ilifafanua haki yake katika kusamehe dhambi za watu wa sheria (Wayahudi), ambazo ziliachwa kuadhibiwa, ndipo habari ya msalaba ni wa kwao peke yao, na sisi tumetengwa“.

Na Paulo aliwajibu: „Lakini Mungu amewasamehe wanadamu wote makosa yao“. Hakuna mungu aliye wa Wayahudi tu, na mungu mwingine kwa ajili ya wengine, maana Mungu ni mmoja, na tena, kwa kifo cha Yesu msalabani aliwahesabia haki wote, waliotahiriwa na wale wasiotahiriwa kwa imani yao“.

Hapo basi, Wayahudi kadhaa walilia: „Hii haiwezekani! Maana ndipo Mataifa mengine wanapata kuhesabiwa haki bila kutahiriwa au sheria, ambayo ni dharau mbele za Mungu. Ewe Paulo, unapindua ufunuo wa Mungu juu chini.“

Paulo aliwajibu hao wachokozi: „Liwe mbali nami hatua ya kubadilisha ufunuo wa Sheria. Sisi, kinyume cha hayo, tunathibitisha sheria kwa njia ya habari njema ya msalaba, nasi tunaweka wazi kwamba, sheria ndiyo utangulizi wa sadaka ya Mungu. Msalaba unafuta madai yote, ambayo kawaida sheria inayaleta juu yetu.

Sisi tunaelewa kutoka kwa mahangaiko ya Paulo dhidi ya watu wale wakali na wale walio wapole wa pande zote mbili kwamba, si waumini wote wanaotambua hali ya haki ya Mungu pamoja na ukuu wake; maana wanaogopa habari njema kwamba, wanadamu wote wamejaliwa haki kwa imani. Ni wachache wanaofikia uhuru wa kikristo, ambayo haikusimikwa juu ya sheria, wala ubaguzi wa kabila, taifa au rangi, wala ya bidii yoyote ya kibinadamu, bali imewekwa msingi kipekee juu ya imani yetu. Imani yetu ndiyo alama kuhusu kujitoa kwetu kwa Yesu, na tumaini letu ndani yake yeye aliyetupenda tangu milele.

SALA: Ee Baba, tunakushukuru kwa sababu umetuweka huru na tabia yetu ya kudai kuwa haki sisi wenyewe, na ulitujalia haki kwa nguvu ya Kristo. Tu wenye dhambi tunapojiangalia wenyewe, lakini tunapomwangalia Mwana wako aliyesulibiwa, tunatambua hiyo haki tuliyopewa. Utufungulie na namna yetu ya kuabudu kinyume, ili tusitafute matendo ya kibinadamu ya kutupatia haki sisi wenyewe, bali tupate kuridhika na kazi ya Mwana wako kwa ajili yetu. Asante sana kwa kutujalia haki kamili, na tunapoungama hayo twajikabidhi sisi wenyewe kwako daima.

SWALI:

  1. Kwa nini tumepewa haki kwa imani tu, wala si kwa matendo yetu mema?

Mwanadamu hujaliwa haki kwa imani mbali na matendo ya sheria.
(Warumi 3:28)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 10:47 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)