Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 024 (The Revelation of the Righteousness of God)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
B - Njia Mpya Ya Kuhesabiwa Haki Kwa Imani Iko Wazi Kwa Wanadamu Wote (Warumi 3:21 - 4:22)

1. Ufunuo wa njia hii mpya ya haki ya Mungu katika kifo cha Kristo cha kulipia (Warumi 3:21-26)


WARUMI 3:25-26
"25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; 26 apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.”

Sio ubinadamu tu uliomsulibisha Kristo, lakini Mungu aliupenda ulimwengu wetu mbaya kiasi hicho kwamba, akamtoa Mwana wake wa pekee mikononi mwa wenye dhambi, akijua kwamba, watamwua. Hata hivyo katika utambuzi wake wa ki-mbinguni alikusudia kwamba, kifo cha Huyu Mtakatifu kiwe ni sadaka na malipo kwa ajili ya watenda dhambi wote na kwa wakati wote. Damu ya Kristo hutusafisha na dhambi zetu zote. Hakuna ukombozi isipokuwa katika damu ya Mwana wa Mungu asiyekuwa na kosa.

Katika enzi zetu za mashangilio ya ajabu na ya ki-teknologia (ya maendeleo), tumepoteza ufahamu kwamba, ghadhabu na hukumu ya Mungu ndizo ni nguvu za kutenda kazi katika historia ya ulimwengu na ya kwamba, hizo ndizo zenye maana zaidi kuliko ndege (eropleni), manowari (submarines), hodhi (tanks) na H-bomu. Kila kimoja cha dhambi zetu kinadai kuadhibiwa na malipo, maana kwa jumla sisi sote tumekuwa tunastahili kifo, ila sadaka ya Kristo badala yetu ndiyo njia yetu ya pekee ya wokovu. Kwa kusudi hilo Mwana wa Mungu akawa mwanadamu, ili apate kuteketezwa kwenye madhabahu ya msalaba ndani ya miali ya moto ya ghadhabu ya Mungu. - Sasa basi, yeyote amjiaye kwa uaminifu, atajaliwa kupewa haki. Mamilioni ya watu tayari wamekwisha kutambua kwamba, nguvu zote za Mungu zafanya kazi kwa njia ya damu iliyomwagika ya Kristo. Kwa sababu hiyo, tunakuita, wewe ndugu mpendwa, usijizuie kuwa karibu naye huyu aliyesulibiwa. Basi, ungekabidhi familia na nyumba yako, kazi yako, maisha yako yaliyopita, mambo yaliyo mbele yako, hata kanisa lako pamoja na wewe binafsi, yote hayo uyaweke chini ya damu inayobubujika ya Mwana Kondoo wa Mungu, ili upate kutakaswa na kulindwa ndani ya ukweli wa Mungu daima. Hakuna ulinzi dhidi ya mashitaka ya shetani na pia dhidi ya mahangaiko ya ghadhabu ya Mungu, isipokuwa ndani ya damu ya Yesu Kristo tu.

Ingefaa ujifunze kwa moyo mistari 21 hadi 28. Yasome maneno hayo tena na tena, ili maana yake iingilie moyoni mwako. Ndipo utatambua kwamba, jambo la muhimu sana ndani ya somo hilo sio kumweka haki mwenye dhambi, lakini ni maonyesho ya haki na Rehema ya Mungu, ambayo yanatajwa mara tatu ndani ya somo hilo.

Mungu mpendwa wetu hakuwaangamiza watenda dhambi katika enzi zilizopita, jinsi sheria ilivyodai. Huyu Mwenye Rehema alisamehe na kutokuangalia maovu yote kutokana na upendo na uvumilivu wake hadi hapo ambapo palitazamiwa na viumbe vyote, yaani wakati huo ambapo upatanisho wa ulimwengu na Mungu ulipokamilika katika mlio wa kifo wa Kristo msalabani. Hapo hata malaika wote nao wakashangilia, maana katika ufufuo wa huyu Msulibiwa, wenye dhambi wote wakajaliwa kupewa haki.

Hivyo, yeyote atakayesema kwamba, Mungu mwenyewe aweza kumsamehe yeyote na wakati wowote akitaka, huyu haelewi, ila anasikiliza mawazo ya binadamu tu ya kiakili. Maana Mungu hawi huru kabisa, ila alijiwekea mipaka yeye mwenyewe kwa maneno na maana ya utakatifu wake; na kutokana na hayo inampasa kila mmoja atendaye dhambi afe. Pamoja na hayo alifunua kwamba, bila kumwaga damu hakuna kusamehewa. Ikiwa Kristo asingetolewa kuwa sadaka, basi Mungu angetenda kinyume, kama angesamehe hivi hivi bila kutimiza madai ya haki aliyeiweka mwenyewe.

Mambo mawili yalitendeka katika usulibisho wa Kristo: Mungu alifafanua haki yake, naye akatuhesabia haki kabisa wakati moja.Yeye Mtakatifu hawi bila haki kwa ajili ya kutusamehe, maana Yesu alitimiza madai yote ya msimamo wa haki ya Mungu. Yeye Mnazarene aliishi bila dhambi kabisa, mtakatifu na mnyenyekevu. Yeye kama wa pekee kati ya viumbe vyote aliweza kujitwisha dhambi yote ya ulimwengu kwa sababu ya upendo wake wenye nguvu mno. Basi, tuinuke na kumwabudu Yesu na kumpenda kabisa, pia na kumtukuza Baba yake, aliyependelea kufa badala ya Mwana wake mpendwa, lakini kutokana na hali ya kuendelea kwa ulimwengu, na huku kuwa na ulazima wa kuleta hukumu juu yake asulibiwaye, basi Baba hakuweza kujitia mwenyewe afe badala ya Mwana.

Katika Sala yake ya kikuhani (Yohana 17), Yesu alimwelekea Mungu kwa maneno haya, “Ee Baba Mtakatifu”. Katika maneno hayo tunakuta maana ya kuingia ndani sana katika kiini cha haki ya Mungu. Mwumbaji amejaa upendo na ukweli. Yeye hawezi kuwa na upendo usio na haki, lakini anajenga rehema yake juu ya haki tupu. Katika kifo cha Kristo mahitaji yote ya hali yake ya utakatifu na haki yamejumlika pamoja. Upendo huo usio na mipaka, ambayo umejengwa juu ya kweli iliyo ya haki, hali hiyo twaiita “NEEMA”, maana imetolewa kwetu kwa njia ya ukombozi wa bure, huku Mungu anapoendelea kuwa mwenye haki, ingawa hapohapo anatupenda na kutusamehe kabisa.

SALA: Ee Utatu utakatifu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tunakuabudu, kwa sababu upendo wako unapitiliza mbali na ufahamu wetu wote, na utakatifu wako una kina zaidi ya bahari. Ulitukomboa kutokana na madhambi yetu yote; ulituokoa na kifo na utawala wa shetani; na hayo sio kwa fedha au dhahabu, lakini kwa njia ya mateso machungu ya Kristo na kifo chake kwenye mti wa msalaba. Damu yake ya thamani ilitusafisha na dhambi zetu zote, nasi tukapata kuwa wenye haki na takatifu kwa neema . Tunaheshimu kabisa sadaka ya Yesu, tunajikabidhi kwako, tukikushukuru kwa ukombozi wako na kutufanya tuwe wa haki.

SWALI:

  1. Ipi ni maana ya sentenso: “kuonyesha haki ya Mungu”?

Wote wamefanya dhambi
na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake
kwa njia ya ukombozi uliyo katika Kristo Yesu.

(Warumi 3:23-24)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 10:42 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)