Previous Lesson -- Next Lesson
d) Kutahiriwa haina faida ya kiroho (Warumi 2:25-29)
WARUMI 2:25-29
"25 Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. 26 Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa? 27 Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, ashikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati? 28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; 29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.”
Alipomaliza kuvunja kiburi cha waumini wa asili ya kiyahudi, wakiwa watu wa sheria, na waliokuwa walimu wa watu wengine, Paulo alisikia rohoni mwake wengine wao wakisema: “Ndiyo, tu wenye makosa, maana hakuna aliye mkamilifu ila Mungu. Lakini tunayo ahadi kutokana na kutahiriwa, maana Aliye Juu alihusika, kwa alama hiyo ya Sheria, pamoja na baba yetu Ibrahimu na uzao wake wote. Hivyo tu mali ya Mungu, si kwa sababu tu wenye haki, lakini kwa sababu alituchagua sisi.”
(Mstari wa 25) Ndipo Paulo, aliyekuwa bingwa katika mafundisho ya kidini ya sheria ya Musa, alijibia maoni yao yaliyokuwa si kweli, akisema kwamba, agano na Ibrahimu haifuti nguvu ya sheria, maana agano inategemea Sheria, jinsi upande wa pili Sheria inategemea agano, jinsi Bwana alivyosema wazi kwa Ibrahimu: “Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu” (Mwanzo 17:1). Mstari huu ilikuwa ni sharti kwa kuthibitisha ile agano, wakati Ibrahimu hakuamini ahadi ya kwanza, akawa alimzaa Ishmaeli bila uongozi wa Mungu, ikawa alikuwa mzaliwa wake wa kwanza kutoka kwa mjakazi Mmisri.
Hivyo Paulo aliwahakikishia Wakristo wa asili ya kiyahudi kule Rumi kwamba, hakuna agano bila sheria na kwamba, kutahiriwa hakukuwa na thamani bila kufuata maagizo ya amri. Kwa jumla, aliona katika kutahiri ishara nzuri, kwamba Mungu hutakasa mtenda dhambi na asili yake, ndipo mwumini na uzao wake watamtii Mungu.
Hata hivyo, taratibu hiyo inafaa tu wakati mshiriki wa agano anafuata mapenzi ya Mungu. Wakati mwumini anavunja maagizo na na kuyavuka kinyume cha Mungu, atahesabiwa ya kwamba, hakutahiriwa, ingawa ametahiriwa, lakini mbali na Mungu na mgeni kwake.
(Mstari wa 26) Ila kama Mpagani alijifunza na kufuata Sheria katika nguvu ya Roho Mtakatifu, ndipo huyo aliyeangaliwa kwa hali ya kutokutahiriwa kimwili, ataangaliwa na Mungu kuwa ametahiriwa na kuunganishwa katika Sheria, pia na kuchaguliwa tangu milele, kwa sababu agano na kuchaguliwa zitaleta upya wa maisha na kumleta kwa wale waliochaguliwa. Yeyote anayefikia shabaha za nidhamu katika mwenendo wake, hata akiwa bila kuta za agano la kale, atahesabiwa kwamba ameingizwa ndani ya agano.
(Mstari wa 27) Kwa Myahudi kupata kuwa mvunja sheria, machoni pa Mungu kweli inamfanya kuwa bila kutahiriwa. Wala si Mpagani tu ni Myahudi wa kweli anapofuata mahitaji ya Sheria, lakini hata huyu ambaye hakutahiriwa kimwili ataketi na kuhukumu juu ya Myahudi aliye na hali ya kimwili ilivyopasa, lakini hana lolote katika njia ya utiifu; Maana alama ya tohara haimwokoi mtu, lakini matendo yake matakatifu ya mtu pamoja na maisha yake yatathibitisha kwamba, amejihusisha na Mungu, na kwamba nguvu ya Mungu inatenda kazi hata katika udhaifu wake.
(Mstari wa 28) Baada ya mpigo huo wa ufundi, aliyoilenga kwa mapokeo ya kiyahudi, sasa Paulo alileta na kielelezo la jina “Myahudi”, ambacho ni lazima kukumbuka na kuthibitisha hata siku hizi. Myahudi sio yule aliyezaliwa kutokana na mzizi (uzao) wa kiyahudi, awezaye kusema lugha ya kiebrania, na akiwa na pua la kupinda, wala si Myahudi machoni pa Mungu anayeamini ndani ya Sheria, apate kutahiriwa, au kusali siku ya Jumamosi. Myahudi anayekubalika kwake Mungu ni yule anayethibitisha uhusiano wake na Mungu kwa upendo, unyenyekevu, utakatifu na ukamilifu. Kufuatana na maelezo hayo ya kiroho, Yesu pekee ndiye Myahudi mkamilifu. Kwa sababu alikuwa ni kinyume cha Wayahudi washupavu, waliomsulibisha katika unafiki wao; na kwa sababu ya roho yake ya unyenyekevu, wazao wa Ibrahimu bado wanawatesa watu wa Yesu hadi leo. Kielelezo cha maana ya “Myahudi” jinsi Paulo alivyoiandika inadai badiliko ya akili (au mawazo) yetu.
(Mstari wa 29) Kutahiriwa basi siothibitisho kwamba, Mungu ni wa taifa au mwumini fulani, hata kama ingeandikwa mara mia nyingi ndani ya Kitabu Kitakatifu; kwa sababu Mungu hawahitaji washiriki wavivu katika agano lake, lakini walio na upendo na mioyo iliyofanywa upya na kujaa Roho wake Mtakatifu. Wale tu waliozaliwa mara ya pili wanahesabiwa machoni pa Mungu kuwa washiriki wa agano, naye anawabariki wote wanaoleta matunda ya Roho yake pamoja na baraka zinazozidi kuongezeka. Lakini basi, wale wanaojiita Wayahudi au Wakristo na wakiwa kinyume cha Roho wa upendo wa Kristo, hao hawakubaliki na Mungu mbali na imani yao safi, lakini wanahesabiwa kuwa adui zake na yeye kuwa Hakimu wao.
SALA: Ee Mungu mtakatifu, tunakushukuru kwa sababu ulijihusisha zamani na rafiki yako wa karibu Ibrahimu na watoto wake kwa ishara ya tohara. Tunakushukuru pia kwa sababu ulitukubali ndani ya Agano lako Jipya. Utusamehe pale ambapo hatukutembea kikamilifu katika utakatifu, au kutokuwa na mwenendo kana kwamba mioyo yetu bado haikutahiriwa na kufanywa upya. Utusafishe na roho zote za kigeni, na utujalie unyenyekevu na upendo wa Kristo, ili tumfuate wakati wowote. Amina.
SWALI:
- Maana ya kutahiriwa ni nini katika zote mbili Agano la Kale na Agano Jipya
“Kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba,
wajiwekea akiba ya hasira
kwa siku ile ya hasira
na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”
(Warumi 2:5-6)