Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 021 (The Privilege of the Jews does not Save them)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)
2. Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa dhidi ya Wayahudi (Warumi 2:1-3:20)

e) Pendeleo kwa Wayahudi haiwaokoi na ghadhabu (Warumi 3:1-8)


WARUMI 3:1-5
"1 Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? 2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. 3 Ni nini basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutukuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? 4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu. 5 Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.“

Paulo kabla hajaandika waraka yake kwa kanisa la Rumi, yalikuwapo maswali kadhaa kati ya washiri wa kanisa. Waumini wa asili ya Mataifa hawakuwahesabu Wayahudi kama watu waliopendelewa sana au kustahili heshima. Kwa hiyo, walipendezwa Paulo alipothibitisha katika barua yake kwamba, sheria na tohara itawahukumu watu wa agano lile la awali.

Upande wa pili, Wakristo wa asili ya kiyahudi, walioambatana na Sheria, waliweka jambo la haki kwa imani ndani ya swali. Hawakupendezwa na masahihisho ya Paulo, kwa vile alivunja mapendeleo yao kutokana na Sheria na agano.

Paulo alifahamu habari ya misimamo hiyo tofauti kwa njia ya safari zake za kimisheni, na alijibu maswali yao mbele mapema ndani ya baua yake kwa Warumi. Alisadiki kwamba fulani alimwambia: „ Wewe uko sawa, Paulo; Wayahudi sio wakubwa kuliko sisi.“ Na Paulo alimjibu pamoja na kicheko: „Ndugu yangu mpendwa, wewe si sawa, maana Wayahudi bado wanayo pendeleo kubwa. Sio kabila lao, wala ustadi wao, wala si taifa lao, ambazo zote hizo ni kama vumbi na majivu. Pendo lao la pekee ni neno la Mungu lililowekwa mikononi mwao. Ufunuo huo utadumu kuwa fahari na wajibu wao daima.

Ndipo Paulo alisadiki kwamba, mpinzani mwingine alisema: „Lakini wao hawakuwa waaminifu na wafuasi wa Amri za agano“. Na Paulo aliitikia kwa shtaki hilo zito akisema: „Je, unafikiri kwamba, kosa la binadamu zitazibadili ahadi na uaminifu wa Bwana zifutike na ziwe bure? Mungu siye mwenye kusitasita, wala hawezi kusema uongo. Neno lake ndilo ukweli wa milele na chemchemi ya ulimwengu. Neema ya Bwana, mbele ya ukafiri wa watu, ni ya uaminifu na ya kudumu daima. Ikiwa Mungu angalitangua agano la kale kwa sababu ya dhambi za watu wake, basi kusingekuwa na ufulizo wa agano letu jipya. Kwa kweli, sisi tulio ndani ya agano jipya tunatenda dhambi zaidi ya wale wa ile ya zamani, tukilinganisha na vipawa vingi vya kustahili kufikiriwa tuliyopewa. Kwa hiyo, hatujengi tumaini letu juu ya makosa yetu yaliyo wazi, au juu ya kufaulu kwetu tunayojiwazia, bali kipekee juu ya neema ya Mungu. Tunakiri kwamba tu waongo na wadanganyifu kama watu wote, na tunashuhudia kwamba, Mungu pekee ni wa kweli na wa kuaminiwa. Uaminifu wake pamoja na ahadi zake hazikosi kufikia shabaha.

WARUMI 3:6-8
"6 Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? 7 Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? 8 Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.“

Jinsi Paulo alivyokazia habari ya tumaini letu, iliyojengwa kipekee juu ya uaminifu wa Mungu, alisikia rohoni mwake sauti ovu zikilia kwa kuchokoza: “Jinsi gani Mungu anaendelea kuwa mwenye haki, kama uaminifu na neema yake inathibitika kwa njia ya dhambi zetu? Je, ni haki kwake Mungu kuadhibu dhambi na kutokuamini kwetu, wakati hatia ya jumla ya binadamu na uchafu wa wanadamu zatoa sababu ya kuthibitisha uaminifu wake kuu? Ikiwa hivyo, basi twende; tufanya dhambi, ili kumtukuza Yeye!“

Paulo hakunyamaza juu ya shtaki hili zito, lakini aliliweka wazi zaidi na kuchimba chini zaidi kimawazo kwa kutumia katazo zingine, naye akaweka wazi kwamba, hakutaja hayo kama mtume, bali kama mtu wa kawaida. Akasema: Hakika, kama uaminifu wa Mungu inathibitika kwa njia ya udhalimu wetu, haitakuwa haki kwake Mungu kuwa hakimu wa ulimwengu wote; na kama maongo yetu yanatia nguvu kwa ukweli wake, hatakuwa na haki ahukumu ulimwengu. Maana ndipo kwa kweli ingekuwa bora kwetu sisi tutende dhambi ili kuleta hali ya kutukuza yaliyo mema.

Katika majadiliano hayo ya kukanusha, Paulo hakutoa jibu kwa swali lile la mwanzoni, lakini alikaza na kuweka hoja wazi zaidi, na akafunua roho mbaya ndani ya waulizaji, ili aondoe hoja zote kwa washindani wake mapema. Ndipo akajumlisha jibu lake ndani ya maneno mawili: Kwanza, „Hasha, kwa kweli hapana!“ yakidokeza katika lugha ya Kiyunani, „Heri wazo hilo lisingetungwa ndani yangu.“ Silikubali tena hata kidogo, na Mungu ni shahidi wangu kwamba, sikubali matukano ya namna hii moyoni mwangu. Na la pili, alisema kwamba, hukumu ya Mungu itawaangukia hao wakufuru, nao hawataweza kutoroka hasira yake, maana atawaangamiza mara moja. Kutokana na mtindo huo wa kitume, tunatambua kwamba, wakati mwingine tunafikia pamoja na maadui wa Kristo hatua fulani, ambapo inatupasa kusimamisha hoja na maswali yote, ili tusiingie katika hatua ya kukufuru. Hapo tunahitaji uhodari wa kufunga mjadala, ndipo kuwaweka hao watu mbele za Mungu kabisa na mbele ya haki yake tukufu.

SALA: Ee Mungu mtakatifu, utusamehe sisi sote hoja zetu za kutokutii. Asante sana kwa uvumilivu wako, maana hujatuangamiza kwa sababu ya uchokozi na kutokujali kwetu, lakini unatuita kutumia akili kwamba, tupate kusikia neno lako vizuri, na tuitikie mvuto wa Roho wako Mtakatifu. Tuondolee maswali yote ya kupinga dhidi ya mpango wako wa upendo, na ututunze katika hali ya kubaliano na mapenzi yako. Ee Bwana, hatutaki kuwa watoto wa kutokutii. Basi, utufundishe unyenyekevu wa Mwana wako na utujalie namna ya hekima ya mitume wako, ili tusihoji tu katika fikara ya kibinadamu tunapojadiliana, bali tutafute uongozi wako bora katika huduma zetu zote.

SWALI:

  1. Yapi ni maswali ya kimsingi yaliyopingana katika barua ya Paulo kwa Warumi, na yapi ni majibu yake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 08:06 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)