Previous Lesson -- Next Lesson
c) Mtu huokoka si kwa kufahamu, lakini kwa matendo (Warumi 2:17-24)
WARUMI 2:17-24
"17 Lakini wewe , ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu, 18 na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati, 19 na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani, 20 mkufunzi wa wajinga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati, 21 basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? 22 Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? 23 Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? 24 Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.“
Mungu aliwakabidhi wazao wa Ibrahimu sheria takatifu kama pendeleo, maana inashuhudia ukuu na utukufu takatifu ya Mungu. Ndiyo,Wayahudi walitambua thamani ya Sheria. Waliitegemea kabisa, nao walijisikia mno kwa pendeleo hilo, na wakafikiri kwamba, hii inatosha kuwapeleka mbinguni, wakati ambapo sheria kwa kweli ikawa sababu kwa ghadhabu na lawama kutokana na namna walivyotenda.
Paulo alihesabia tabia safi na baya, zilizowaeleza Wayahudi. Hiyo funuo tukufu iliwapa watu wapitao jangwani (baada ya kutoka Misri) utulivu, tumaini, pia na fahari, kwa sababu walimfahamu Mungu na mapenzi yake. Walitambua njia bora kwa maisha yao, nao zamani zile wakapata kuwa walimu wa watu wengine na nuru kwa mataifa.
Upande mwingine, Paulo aliwathibitishia kwamba, sheria haina uwezo wa kumbadilisha mtu. Ni kweli kwamba kwa njia ya sheria Wayahudi walifahamu yale waliyopaswa kutenda, bali hawakutimiza kanuni walizopewa. Walifahamu siri za Mungu, lakini hawakutembea ndani ya mipaka yao. Wengi wao walifikia daraja la juu sana ya kicho ya kisheria ya nje na kuitimiza kwa bidii kali kama chuma. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu haikumwagwa ndani ya mioyo yao.
Pengine hawakuiba kwa tendo hasa, lakini macho yao yalikuwa yamepofuka na uchoyo. Pengine hawakutimiza uzinzi waziwazi, lakini mioyo yao ilifurika na mawazo machafu. Walivunja sheria za Mungu mara elfu nyingi. Na kwa kuongeza hapo, Paulo aligundua upungufu wa upendo hata ndani ya maisha ya waumini wakati wake. Walivunja heshima ya Mungu kwa dhambi zao, na pia kuwachokoza watu wa mataifa mengine kukufuru dhidi ya jina lake takatifu.
Paulo mwenyewe alikuwa ni Mkristo wa asili ya Wayahudi na akaandika, mbali na fahari yao ya kudanganya, mali yote ya kiroho yaliyokuwa ya juu kabisa ya hao watu wake. Na kutokana na tamko hilo wazi, yeye alikuwa na haki na nguvu kuweka wazi dhambi na mambo yote ya aibu ya taifa lake; kwamba haikubakia lolote la sifa na haki zao kwa kulinganisha uchokozi wao kuu na makosa yao ya kukasirisha. Hakuna lalamiko kukandamiza zaidi dhidi ya watu au taifa lingine kuliko kusema kwamba, jina la Mungu limetukanwa kutokana na mwenendo wao. Hawakuitika kwa wito wao wa awali kuwaangaza watu na sheria, lakini walitenda yaliyokuwa kinyume. - Basi sisi siku hizi tungeweza kupata tu shahidi wa ushujaa kama ya Paulo, asiyekana mapendeleo yetu tuliyo nayo, lakini anayeondoa kifuniko cha uso ya kicho kutoka usoni mwa jamii yetu chafu, ili lisibakie lolote ila ungamo na kuvunjika kimoyo.
Je, unawahukumu watu wa Ibrahimu? Uwe mwangalifu! Wao ni wenye dhambi kama wewe.
Mungu alitamka wazi: „Uwe mtakatifu, jinsi nilivyo mtakatifu“. Wewe kweli ni Mkristo takatifu na kamili, jinsi Baba yako wa mbinguni alivyo? Je, nuru yako inang’aa mbele za watu, ili waweze kuyaona matendo yako mema na kumtukuza Baba yako aliye mbinguni, kutokanana na badiliko la wazi ndani ya maisha yako? Rafiki zako je, wanadharau dini yako, kwa sababu wewe sio bora kuliko wale wanaokataa kazi ya ukombozi wa Kristo? Unaweza kuwa sababu ya kukufuru dhidi ya jina la Mungu? Baba yetu wa mbinguni anaweza kujifunua kwa njia ya upendo na unyenyekevu wako?
SALA: Ewe Mungu mkuu na mtakatifu, dhambi zangu ni kubwa kuliko ninavyotambua. Katika kutokutii kwangu na unafiki wangu, mimi nami nimekuwa sababu ya tukano kwa wengi. Unisamehe ambapo yeyote anatukana dhidi ya jina lako takatifu, kwa sababu mimi sikutembea kikamilifu mbele zako. Nisamehe upungufu wangu katika upendo, usafi na uvumilivu. Uniumbe katika sura yako, ili wengine wakuone wewe ndani yangu; hivyo unisaidie kutii maagizo yako na kufuata mfano wako, ili na sura yako ing’ae zaidi na zaidi ndani yangu. Uniokoe na udhaifu wangu, makosa yangu na umimi wa kujiona tu.
SWALI:
- Zipi ni mapendeleo na pia mizigo ya sheria (torati) juu ya Wayahudi?