Previous Lesson -- Next Lesson
b) Petro na Yohana wanakimbia haraka kaburini (Yohana 20:3-10)
Yohana 20:6-8
„Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake. Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini.“
Yohana alisimama nje ya kaburi akingojea kufika kwa Petro, dalili ya heshima kwa mtume mkubwa; na ndiye wa kwanza wa kuona kaburi katika hali tupu. Kijana Yohana alitetemeka kwa yale aliyoyaona kwanza lile jiwe kuvingirishwa mbali, kaburi kuwa wazi na mwili umetoweka. Pia na sanda ilikunjwa na kuwekwa kwa uangalifu. Mawazo yakavurugika kichwani mwake; akaomba kwa kutafuta nuru kutoka kwa Bwana kuhusu hayo yaliyotukia.
Kitambo Petro naye akafika na kuingia moja kwa moja ndani ya kaburi wazi; alitambua kwamba kile kitambaa kilichokuwa usoni pake Yesu ilikuwa imewekwa peke yake pembeni. Hii ilimaanisha kwamba mwili haikuibiwa, kwa vile kuondokewa kwake kulienda kwa taratibu na kimya.
Petro aliingia kama kwamba yeye alikuwa ni mkaguzi, hata hivyo hakutambua maana ya dalili ambazo zilikuwa wazi. Yohana, mwenye kutafakari zaidi, akawaza-waza na kuomba, hata akatambua tumaini fulani. Alipoitika kwa wito wa Petro na kuingia, roho yake ilimulikiwa na kuanza kuamini katika ufufuo wa Kristo. Kwake haikuwa hatua ya kukutana na Mwenye Kufufuka kilichoumba imani ndani yake, lakini kaburi tupu na sanda iliyowekwa kwa kukunjwa taratibu, ndiyo dalili zilizomdokezea kweli na kuamini.
Yohana 20:9-10
„Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka. Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao.“
Yesu hakubakia kaburini kama wengine wote, kama vile wanafilisofia, manabii, na wenye dhambi wote wengine, lakini alifufuka , akiachia nyuma kifo kama vile mtu anavyoondoa nguo. Mtakatifu huyu alisalia bila dhambi. Kifo haikuweza kumshika. Upendo wa Mungu haukosi kushinda.
Maadui wa Kristo hawawezi kudai kwamba mwili wa Yesu ulioza ndani ya kaburi, kwa sababu ilikuwa tupu. Kristo hakutoroka wala hakuchukuliwa kwa nguvu, kwa sababu chumba cha maiti yake ilikuwa na picha ya utaratibu kabisa. Hii ilikuwa ni ushahidi kwake Yohana kwamba Yesu alitupa namna yake ya kidunia kwa vile hakuihitaji tena. Katika nguo za kitoto na kulazwa ndani ya hori alianza safari ya maisha yake, na katika sanda ya kuzikwa aliondoka. Hivyo wakati wa ufufuo wake hatua mpya ya kuwepo kwake kulianza katika hali ya kimbinguni. Hata hivyo aliendelea na namna yake ya ubinadamu.
Mawazo kama hayo yalivuruga akili ya Yohana, wakati aliporudi kutoka kwa kaburi wazi. Lakini hakujisifu na mambo aliyoyaona, akiwa wa kwanza wa kutambua ushindi wa Mwana wa Mungu katika kufufuka, lakini alikiri kwamba aliamini mwujiza huo kwa kuchelewa, iwapo ilikuwa imefunuliwa wazi katika Maandiko. Macho yake bado yalifumbwa kwa yale aliyowahi kusoma kuhusu kifo na ushindi wa Mtumishi wa Mungu badala yetu, tusomavyo kwa Isaya 53, wala hakushika utabiri wa Mfalme Daudi juu ya mambo hayo ha yo (Luka 24: 44-48; Matendo 2:25-32; na Zaburi 16:8-11)
Asubuhi ya Sikukuu kubwa ilishuhudia wanafunzi wawili wanaporudi nyumbani kwao, hali wanahangaika sana, lakini bado wenye moyo wa kutumaini, wakitegemea pamoja na maswali magumu moyoni na wakiomba kwake Yesu, aliyetoka kaburini, bila wao kutambua alikoenda.
Sala: Bwana Yesu, twakutolea shukrani toka moyoni hasa, maana wewe u Mshindi ndani ya mioyo ya wanafunzi wako, ukiumba ndani yao tumaini la kufufuka kwako. Umetujalia tumaini kuu kwa ajili ya uzima wa milele. Tunakuabudu, maana ndiwe Mungu wa milele, na sisi twapata hali ya kutokufa kwa neema yako. Waokoe rafiki zetu kutoka kifo cha dhambi zao na kuwajalia wao nao uzima wa milele kwa imani ndani ya dhabihu yako.
Swali 120: Yohana alitumaini nini akiwa ndani ya kaburi tupu?