Previous Lesson -- Next Lesson
a) Mariamu Magdalene akiwa karibu na kaburi (Yohana 20:1-2)
Yohana 20:1-2
„Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.“
Wanafunzi na wale wanawake waliomfuata Yesu walikumbwa na matokeo ya siku ya Ijumaa. Kutoka mbali wanawake walitazama jinsi Yesu alivyowekwa kaburini. Wote, wanawake na wanafunzi walikuwa wamefanya haraka kufika nyumbani, wasije wakalaumiwa kwa kuvunja Sabato, inayoanza Ijuma kunapokuchwa, kama saa kumi na mbili.
Kwenye Sabato hiyo kubwa inayokutana na sikukuu ya Pasaka, hakuna aliyethubutu kwenda kaburini. Wakati umati wa watu waliposhangilia juu ya wazo kuu kwamba, Mungu amepatanishwa na taifa, kwa ishara ya kuchinja kondoo za Pasaka, Wakristo walikuwa wamekutanika na hofu na machozi. Matumaini yao yalikuwa yamezikwa pamoja na kuzikwa kwa Bwana wao.
Kwenye jioni ya Sabato, wanawake hao hawakutoka nje ya malango ya jiji, wala kununua manukato au vitu vingine kwa ajili ya kupaka mwili wa maiti wao. Walikuwa wakingojea kwa matazamio ya pekee kukicha siku ya Jumapili. Huyu mwinjilisti anadokeza kutembelea kwa Magdalene kwenye kaburi, lakini kuna dokezo fulani katika tamko la Magdalene kusema „sisi“. Salome, mamaye Yohana na wachache wengine walienda pamoja mapema Jumapili asubuhi wakiwa na majonsi, ili wapake mwili.
Ilikuwa mapema sana asubuhi kulipokucha, hali wametaabika na huzuni, walipokaribia kaburi na kusadiki kwamba imefungwa kwa muhuri. Tumaini lao likatingishwa mno na kutandwa na hali ya kukata tamaa. Nuru ya ufufuo ilikuwa bado haijawamulikia, wala uzima wa milele haijainuka ndani ya mawazo yao.
Kwa kufika tu wakastushwa walipoona lile jiwe kubwa limeondolewa langoni mwa kaburi, ambalo walikuwa wakiwazawaza namna ya kuliondoa.
Kaburi wazi ndiyo mwujiza wa kwanza wa siku hiyo, ushahidi kwa hofu zetu zote na mashaka yetu kwamba, Kristo anaweza kuvingirisha mbali mawe yote yanayoweza kulemaza mioyo yetu. Yeye aaminiye ataona msaada kwake Mungu; imani inaona mambo yaliyo mbele kuwa bora na safi.
Yohana hatuelezi chochote kuhusu kutokea kwa malaika. Inategemewa kwamba, Mariamu Magdalena aliwapita rafiki zake mbio na kuchungulia ndani ya kaburi. Basi hakuona mwili ndani. Kwa kutishwa sana, aliwakimbilia wanafunzi. Alikuwa akifahamu kwamba, yule wa kwanza katika kundi la mitume lazima afahamu habari ya mwujiza huu, pamoja na wanafunzi wote wengine. Wakati Mariamu Magdalena alipomfikia Petro na wenzake, akatokeza maneno hayo, “Mwili wa Yesu umepotea.“ Hii ni taksiri nyingine. – Basi hayo yaonyesha kwamba wanafunzi na yeye naye walikuwa vipofu kiroho, kwa sababu walifikiri watu fulani waliiba mwili. Haikutokea mawazoni mwao kwamba Bwana alikuwa amefufuka, alivyowahi kuwaeleza, kwa kuwa yeye ndiye Bwana.
b) Petro na Yohana wanakimbia haraka kaburini (Yohana 20:3-10)
Yohana 20:3-5
“Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini. Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia.”
Hii ilikuwa ni kimbilio kwa ajili ya upendo. Kila mmoja wao alitaka kuwa wa kwanza karibu na Yesu. Petro, mwenye umri zaidi, alikuwa anahenya nyuma ya kijana Yohana bila kuweza kushikamana naye. Wote wawili walisahau hofu kwa ajili ya wapelelezi au walinzi wakitoka nje ya malango ya jiji. Yohana alipofikia kaburi, hakuingia; katika hali ya kustahi alijizuia. Kwa kuchungulia ndani ya shimo la kaburi mwambani alitambua gizani vitambaa vyeupe vya sanda vilivyokunjwa na kusalia pale kama buu ambamo mdudu wake ameesha kutoka. Ile sanda haikuanguka, bali kubakia pale ambapo mwili ulilazwa. Hii ndiyo mwujiza wa tatu kuhusu ufufuo. Kristo hakurarua ile sanda, lakini alikwea kutoka katika vile vitambaa. Malaika hawakuondoa lile jiwe kwa kumsaidia Yesu atoke, bali waliliondoa ili wanawake na wanafunzi waweze kuingia. Bwana mwenyewe alipitia ndani ya mwamba njiani kutokea nje.
Sala: Bwana Yesu Kristo, twakushukuru sana kwa kufufuka kwako kutoka kwa wafu. Wewe ulishinda nguvu zote mbaya na kutufungulia njia kwenda kwa Mungu. Wewe u pamoja nasi katika bonde la uvuli wa mauti bila kutuacha. Sasa uhai wako ni wetu; nguvu zako umekamilika ndani ya udhaifu wetu. Tunakuinamia na kukupenda mno, kwa sababu umewajalia waumini wote tumaini kuu la kushangilia.
Swali 119: Zipi ni zile dalili tatu za ushahidi kwa ajili ya ufufuo wa Yesu?