Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 112 (Christ's word to his mother; The consummation)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
A - Matokeo kuanzia kukamatwa kwake Yesu hadi kuzikwa kwake (Yohana 18:1 - 19:42)
4. Msalaba na kifo cha Yesu (Yohana 19, 16b – 42)

c) Tamko la Kristo kwa mama yake (Yohana 19 : 25 – 27)


Yohana 19:24b -27
“Basi ndivyo walivyofanya wale askari. Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalena. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”

Yohana haelezi neno la kwanza la Yesu, aliposamehe ulimwengu wote. Wala hatamki dharau iliyoendelea kutajwa na Wayahudi, wala Yesu alivyomsamehe yule mhalifu upande wake wa kulia. Mambo hayo tayari yalikuwa yamejulikana na makanisa wakati Yohana alipoandika injili yake.

Makuhani walipoondoka mahali pa msalaba bila kusikia maombezi yake na alivyomsihi Baba atoe msamaha, hata makundi ya watu wakaondoka, wakikimbilia Jerusalemu ili watoe sadaka ya kondoo wa Pasaka. Muda wa maandalio uliowabakia ulikuwa fupi. Pia na viongozi wa kidini walienda kutimiza mapokeo ya sikukuu kubwa ya kitaifa. Baragumu zililia kutoka kwenye kuta za jiji, kondoo waliochinjwa hekaluni, na damu ilitiririka tele. Hekalu ilivuma sauti za kutukuza. Nje ya Yerusalemu alitundikwa Kondoo takatifu ya Mungu kwenye mti uliolaaniwa, kukataliwa na kudharauliwa. Walinzi wa Warumi wa kipagani walikuwa wanachunga hao watatu kwenye misalaba.

Wakati uo huo wanawake kadhaa wakakaribia msalabani bila kusema na kusimama kwa ukimya. Mambo yaliyotangulia yalifumba akili zao. Mwenye Enzi yote alitundikwa juu ya vichwa vyao katika maumivu makali. Maneno ya kupooza hayakutamkwa, hata mioyo ilishindwa hata kusali. Pengine baadhi yao walinong’ona maneno ya Zaburi.

Yesu alisikia milio ya kimoyo ya mamaye, pia na kuelewa machozi ya mwanafunzi wake mpendwa Yohana. Hakutafakari sana juu ya hali yake, iwapo hali ya kuzimia ilikaribia. Mara moja wakasikia sauti yake, “Mama, tazama mwanao.”

Upendo wa Kristo ulifikia kilele, akiangalia kwa utunzo wa wapendwa wake katikati ya mateso yake kwa kupatanisha ulimwengu. Neno lililotabiriwa na Simeoni kwa huyu Bikira lilitimia hapo, kwamba upanga utachoma moyo wake (Luka 2:35)

Pasipo namna ya kumpatia mamaye fedha au nyumba, akamtolea upendo ambao aliimimina ndani ya wanafunzi wake. Yohana alikuwa amekuja na mamaye Kristo (Mathayo 27:56); hata hivyo hataji jina lake wala la Bikira, kana kwamba hakutaka kupunguza heshima aliyoistahili Kristo pekee katika saa hii ya utukufu. Alipomsemesha Yohana na kukabidhi mamaye kwa tunzo lake, ndipo tu huyu mwanafunzi aliingia ndani ya mngao wa msalaba. Akamkumbatia Mariamu na kumpokea nyumbani kwake.

Wanawake wale wengine walishuhudia hiyo ipasayo. Mmoja wa wale wengine Bwana alikuwa amemwokoa na mashetani saba; huyo alikuwa na Mariamu Magdalene. Huyu alisikia kabisa rohoni mwake enzi ya ushindi wa Yesu rohoni mwake. Alimpenda mno Mwokozi wake na kumfuata.


d) Ukamilisho (Yohana 19 : 28 – 30)


Yohana 19:28-29
“Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.”

Mwinjilisti Yohana alikuwa na kipawa cha kusema mengi katika maneno machache. Hasemi lolote kuhusu giza uliofunika nchi, wala hatusikii kwake mlio wa Kristo kwa ajili ya kuachwa peke yake katika ghadhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini tunajulishwa kwamba, mwisho wa taabu yake ya kifo iliyoendelea masaa matatu, alitambua kukaribia kwa kifo. Yohana hakutamka kifo kwamba ilimmeza Yesu, lakini kwamba Yesu alijitoa kwa kutaka kuipokea. Roho yake ilikuwa umechoshwa kabisa katika kukamilisha kazi ya kiulimwengu ya ukombozi. Yesu aliona wokovu kamili uliopatikana kwa wote sasa, na jinsi kifo chake itakavyoweka huru mamillioni ya watenda dhambi kutokana na hatia zao na kuwajalia haki ya kumjia Mungu. Aliona mavuno na matunda ya kifo chake mapema.

Hapo hapo midomo yake ikapumua hilo tamko, “Naona kiu”. Yeye, aliyekuwa ameumba ulimwengu wote na kutembea juu ya maji yaliyotengenezwa na uweza wake, yeye aona kiu. – Upendo ulioingia mwilini ulitamani kuwa na upendo wa Babaye, aliyekuwa ameficha uso waka kwa Mwana wake. Hii ni tukio kama ya kuzimuni, ambapo watu huona kiu cha kimwili na cha kiroho bila uwezo wa kuburudika tena. - Wakati fulani Kristo alikuwa anamtaja mtajiri akiwa kuzimuni pamoja na kiu kali ndani ya moto kuu, ambaye hapo alimsihi Ibrahimu amtume Lazaro achovye kidole chake katika maji baridi ili apooze koo lake uliovimba. Jesu alikuwa mtu kweli, akivumilia kiu cha kawaida, lakini hakuridhisha kiu chake hadi kazi ya ukombozi ulipokamilika. Ndipo Roho Mtakatifu alimfunulia kwamba, huduma yake ya ukombozi ulikuwa umetangazwa miaka elfu moja kabla ya hapo katika Zaburi 69:21.

Hatujui kama askari walimpelekea kinywaji kilichokuwa siki tupu au ilichanganywa na maji.

Mwanadamu Yesu, aliyekuwa Mwana wa Mungu, katika jambo hilo alikuwa bila uwezo.

Yohana 19:30
“Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”

Baada ya Yesu kuionja siki ya ghadhabu, akalitamka neno hilo la ushindi, “Imekwisha!” Siku moja kabla ya mlio huo wa shangilio, Mwana alikuwa amemwomba Baba yake amtukuze pale msalabani kwa ajili ya ukombozi wetu, ili na Baba mwenyewe apate kutukuzwa. Mwana alithibitisha kiimani kwamba, ombi hilo litajibiwa, ya kwamba alikamilisha ile kazi nzito ambalo Babaye alimtwisha (Yohana 17:1,4).

Inashangaza jinsi Yesu alivyokuwa msafi pale msalabani! Hata neno moja la chuki halikutoka mdomoni mwake, wala tamko la kujihurumia au mlio wa kukata tamaa, hakuna; Lakini aliwasamehe watesi wake, aliendelea kushikamana na upendo wa Mungu, aliyeonekana hapo kama adui kwa ajili yetu. Yesu alifahamu kwamba alimaliza kazi ya ukombozi, kwa sababu Mungu alimkamilisha huyu mpenyezi wa wokovu wetu kwa njia ya kuteseka. Hakuna awezaye hata kubuni kina wala urefu wa upendo wa Utatu, maana Mwana alijitoa mwenyewe kwake Mungu kwa njia ya Roho wa Milele, akiwa bila doa, atoe sadaka iliyo hai (Waebrania 9:14).

Tangu mlio huo wa mwisho wa Kristo pale msalabani ulisikika, ukombozi ni kamili, bila kuhitaji kukamilishwa zaidi. Sio michango yetu, si matendo yetu mema au sala, au kujitakasa sisi, inayoweza kuleta haki, au hata kuongeza utakatifu ndani ya maisha yetu. Mwana wa Mungu ametutendea hayo yote, tena mara moja kwa ajili ya wote. Kwa kifo chake millenium mpya imepambazuka na amani inatawala, kwa sababu Mwana Kondoo wa Mungu aliyechinjwa ametupatanisha na Baba wa mbinguni. Kila mtu aaminiye hayo atahesabiwa haki. Barua za Biblia ndiyo mafafanuzi juu ya maneno ya Yesu, kamili na tukufu, “Imekwisha!”

Yesu akainama kichwa chake mwishowe, ikiwa katika heshima na enzi. Alikabidhi roho yake katika mikono ya Baba yake, aliyempenda bila kukoma. Upendo huo ulimvuta hadi kwenye kiti chake cha enzi na neema, ambapo anaketi hata leo mkononi mwa kulia kwa Babaye, akiwa na umoja naye.

Sala: Ewe Mwana Kondoo mtakatifu, uliyeziinua na kuzibeba dhambi za ulimwengu, wewe unastahili kupokea enzi, utajiri, hekima, mamlaka, heshima, utukufu, baraka na pia maisha yangu. Uinue kichwa changu nikutazame wewe tu, ee Msulibishwa, nikitafuta rehema kutoka kwako kwa ajili ya makosa yangu yote; nami nategemea utanitakasa kwa neema na damu yako.

Swali 116: Maneno matatu ya Yesu msalabani ni yapi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 25, 2017, at 02:36 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)