Previous Lesson -- Next Lesson
a) Usulibisho na mavazi ya mazishi (Yohana 19, 16b – 22)
Yohana 19,16b-18
“ … nao wakampokea Yesu. Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fufu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.”
Kundi la askari walikuwa tayari kuondoka wawasulibishe wanyang’anyi wawili, wakati Pilato alipowakabidhi na Yesu kama “mhalifu” wa tatu. Maaskari waliwatwisha misalaba wote watatu, ili kila mmoja aibebe chombo cha kifo chake. Kristo hakukataa ule msalaba, wala hakutupa mti ule njiani. Hao watatu walipitia vichochoro vya mji wakiwa wakivuta hewa kwa mchosho, mwishowe kufikia lango la kaskazini la magharibi. Ndipo kufikia kilima kilichojulikana kwa jina Golgotha, maana palijumlika miamba kadhaa kwenye kilele chake, kilichoinuka kidogo juu ya kuta za jiji la Yerusalemu. Wenyeji waliweza kuangalia wanaume wale waliohukumiwa na kutundikwa juu ya misalaba yao nje ya jiji.
Yohana haelezi kinaganaga mambo ya msalaba, kalamu yake kilimzuia kukariri matukio hayo ya kuogofya. - Watu walikuwa wamekatalia upendo tukufu, na chuki ya kuzimuni ilikaa juu yao. Kwa ukorofi walimwondoa yule aliyezaliwa na Roho; na kwa dhambi zao walikamilisha dhabihu ya Kristo iliyolipia na dhambi zao. - Yeye hakubeba duara la dhahabu kwenye mti wa aibu, lakini kwa kina cha unyenyekevu wake alifunua utukufu wake kwa uvumilivu na kujikinahi katika utakatifu.
Fedheha gani iliyomfanya Yesu kutundikwa katikati ya wahalifu wawili? Wao walikuwa wakijipinda na kulaani wakiwa wamening’inia.
Huyu Mmoja mwenye rehema na safi alijifunua hata katika dakika zake za mwisho wa maisha yake kuwa mwungwana wa wenye dhambi. Kwa sababu hiyo Mwana wa Mungu alizaliwa kuwa Mwana wa Adamu, ili watoto wa Adamu wapotovu waweze kupata kuwa watoto wa haki wa Mungu. Alishuka kwenye kina kirefu cha udhilifu, kusudi asiwepo yeyote wa kusema kwamba Yesu hakutelemka kwenye uchini wake. Kokote ulipo na jinsi gani ulivyoanguka, Kristi aweza kukufikia na kusamehe hatia zako, akikusafisha na kukutakasa kikamilifu.
Yohana 19:19-20
“Naye Pilato aliandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani.”
Maaskari walimtundika Yesu katikati ya wahalifu wawili kama dalili ya dhihaka kwa ajili ya dai lake la kifalme. Wakati huo Pilato aliendelea kuwachokoza wale wa baraza la Kiyahudi waliomlazimisha kumhukumu Yesu kinyume cha dhamiri yake. Juu ya kichwa cha Msulibiwa, Pilato aliweka ubao uliokariri mashitaka ya Kiyahudi.
Mungu alitumia maneno hayo kichwani pa msalaba ili awahukumu Wayahudi, maana kweli Yesu alikuwa ni mfalme wao. Yesu kiasili ni Mfalme, ajaye katika uaminifu , pendo, upole na unyenyekevu. Yeye alianzisha mbingu hapo duniani. Wayahudi walipendelea kuzimu, wakimkataa Mfalme wao mtakatifu nje ya jamii yao. Na hivyo akapata kuwa Mfalme wa Mataifa; - lakini je, mataifa wanamkubali siku hizi Mfalme aliyesulibiwa, au wanamkataa tena Bwana wa upendo ?
Yohana 19:21-22
“Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi. Pilato akajibu, Niliyoyaandika nimeyaandika.”
Makuhani wakuu walielewa sana maana ya dharau na matisho ya Pilato, ingawa yalifichwa. Walikuwa wamemkataa Mfalme wao na kuona ndani ya udhaifu wake hali ya kinyume kabisa na yale ambayo Pilato aliyadai. Wakamchukia Msulibishwa zaidi na zaidi.
Pilato aliona hakika kwamba, maneno yaliyoandikwa ni kufuatana na mapenzi ya Kaisari, Na hivyo akayaandika kwa lugha tatu kwa watu wote walioweza kusoma, wenyeji sawa na wageni wapate kuyasoma na kufahamu kwamba, mwasi yeyote dhidi ya Rumi atafanyiwa vivyo hivyo. - Basi mwaka wa Bwana 70 (AD), wakati Wayahudi walipoasi dhidi ya utawala wa Kirumi, maelfu walitundikwa kwenye misalaba kwa kuzunguka kuta za Yerusalemu.
b) Kugawana nguo za Yesu na kupiga kura (Yohana 19 : 23 – 24)
Yohana 19:23-24
“Nao askari walipomsulibisha Yesu, Waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungo manne, kwa kila askari fungo lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Basi wakaambiana, Tusipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, navazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.”
Wale askari wanne waliomsulibisha Kristo walikuwa na haki ya kugawana nguo zake. Lakini yule akida (ofisa wa askari) hakujishusha kiasi cha kushiriki katika jambo hilo la aibu. Basi wale wanne walichukua ya mwisho aliyokuwa nayoYesu na kumwondolea heshima yote. Kawaida wahalifu waliosulibishwa walivuliwa uchi na hivyo kuwashusha zaidi.
Udhilifu huo ulitangaza kwa namna ya pekee enzi ya Yesu. Kanzu yake ambayo haikushonwa ililingana na ile ya Kuhani Mkuu. Yesu mwenyewe ndiye Kuhani Mkuu na mwombeaji wa binadamu wote. Kwa ajili ya huduma hiyo alivumilia yote hayo na kuteseka.
Miaka elfu moja kabla ya hapo Roho Mtakatifu alikuwa ametabiri mambo kinaganaga kuhusu usulibisho; na Zaburi 22 inasema hayo, “Nguo zangu waligawana kati yao”, jambo ambalo kwa askari ni ya kawaida. Tena Roho alitamka pia kwamba watapiga kura juu ya vazi lake. Roho ilifunua jambo la msalaba kikamilifu, akieleza kwamba kusulibiwa kwa Yesu ilikuwa ni kusudi la Mungu kabisa. Jinsi Yesu alivyokuwa ametamka: Hakuna hata unywele utakaodondoka bila Baba yenu wa mbinguni kufahamu. Yeyote asemayo kwamba jambo la msalaba haikutendeka, basi anakana tendo la kihistoria na pia atakuwa kinyume cha Roho wa Mungu aliyetabiri tukio hilo millenium moja kabla ya kutimia. Askari walishughulika bila kutambua hayo na pasipo kusikia utofauti yoyote hapo chini ya msalaba. Walizozana juu ya mabaki ya mteseka. Hawakusikia huruma yoyote; hawakudhania kwamba Msuluhishi wa ulimwengu alikuwa anamwaga damu yake hapo msalabani.
Ndugu je, ubinafsi wako umesulibishwa na Kristo, ndani ya umoja wa kifo chake? Au unakimbilia tu utajiri na heshima? Unampenda huyu Msulibishwa na umepokea haki tukufu na utakatifu wa kweli kutokana na kifo chake? Au unaendelea kuwa mwangalizi wa kimawazo, bila kuguswa na sura yake hapo anaposulibishwa? Roho Mtakatifu anaunganika na Mwana wa Mungu katika imani na upendo, ili na sisi tushiriki katika kifo chake, kuzikwa kwake na maisha ya kujitolea kabisa.
Sala: Bwana Yesu Kristo, twakushukuru sana kwa ajili ya kubeba msalaba. Twakuabudu kwa ajili ya uvumilivu wako, upendo na baraka. Tunakutukuza kwa ajili ya kutusamehe dhambi zetu pia na dhambi za ulimwengu wote. Uliondoa na makosa yangu mimi ulipotundikwa kwenye mti wa aibu na kupatanisha binadamu na Mungu. Wewe ndiwe mwokozi na mwombezi wetu.
Swali 115: Nini ni maana ya maandiko yaliyowekwa juu msalabani