Previous Lesson -- Next Lesson
e) Kuchoma ubavu wa Yesu (Yohana 19 : 31 – 37)
Yohana 19:31-37
“Basi Wayahudi, kwa sababu ni maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli, ili ninyi nanyi mpate kusadiki. Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lasema, Watamtazama yeye waliyemchoma.“
Wakiwa na bidii kupita kiasi kuhusu sheria na taratibu zao, Wayahudi hawakusikia tena huruma ya kibinadamu. Taratibu ya Musa ulisema kwamba, miili ya wasulibiwa iondolewe kabla ya giza la usiku. Basi Wayahudi walitaka hivyo kwa wale watu watatu waliosulibiwa. Walikuwa wakikataa kutazama mahali pale pa kuchukiza hasa wakati wa sikukuu hiyo. Walimwuliza Pilato awamalize hao watatu upesi kwa kuvunja miguu yao. Iliwezekana wasulibiwa wavumilie hata siku tatu bila kukata roho. Kushikiza miguu na mikonno kwa misumari mtini pengine kusitokeze damu kwa kutosha wafe. Basi askari walienda kuharibu miili kwa mapigo ya kuvunja mifupa.
Ndipo askari walisimama mbele za Yesu, wakatambua kwamba tayari amekufa. Mwili wake laini ilidhoofika kwa kupigwa mijeledi, na roho yake katika maumivu makuu ya uzito wa makosa yetu pamoja na ghadhabu ya Mungu juu ya ulimwengu. Yesu alifariki kwa uhuru wa kibali chake, ili aweze kutupatanisha na Mungu. Bila kujishughulisha zaidi na mambo ya kidini, Wayahudi walitamani sana kuhakikisha kwamba Yesu amekufa. Mmoja wa wale askari alichukua mkuki na kuchoma ubavu wa Kristo karibu na moyo wake. Maji na damu zikatoka mara, ikathibitika kwamba alikuwa amefia kabla ya saa sita wa Ijumaa ile Kuu.
Tukio hilo lamweleza Mkristo kwamba, Mungu ni mshindi kwa namna tatu: Kwanza, Wayahudi walichokozwa na Shetani watake kuvunja mifupa ya Kristo, ili mtu yeyote asidai kwamba huyu Msulibiwa ndiye dhabihu tukufu. Mapokeo ya Pasaka yalidai kwamba, yule kondoo awe mzima, bila mifupa kuvunjwa (Kutoka 12:46). Hivyo Mungu alimlinda Mwanawe hata kifoni, wala yeyote asiweze kukana kuteuliwa kwake kuwa Mwana Kondoo wa Mungu.
Pili, kuchomwa kwa ubavu wa Yesu kwa askari inapatana na tamko la Zekaria 12:10. Na kwa Zekaria 11:13 nabii aliona kwamba watu wa Agano la Kale walimthamini Mchungaji wao kwa kiasi cha vipande thelethini za pesa. Ijapokuwa hiyo kiasi ni cha dhihaka, Mungu atamwaga Roho ya neema na sala juu ya nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, kusudi hata macho yao yapate kufumbuliwa na kutambua huyu Msulibiwa alikuwa ni nani, na kwamba yu mmoja na Baba. Bila kutiwa nuru ya kiroho namna hii wasingemtambua Mungu wala wokovu wake. Huyu Msulibiwa pekee ndiyo namna ya kuweza kumpokea Roho wa Mungu, jinsi tusomavyo, “Watamtazama (kwa Mshangao) yule waliyemchoma”.
Tatu, mwanafunzi yule ambaye kwa uaminifu alibakia chini ya msalaba alikuwa ni mshahidi wa macho kwa yote yaliyotendeka na yaliyosemwa. Hakutoroka alipowaona askari wala hakumwacha Bwana wake hata baada ya kifo chake. Aliona kuchomwa kwa ubavu wa Yesu, na anatushuhudia habari ya upendo wa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, ili tupate kuamini ndani ya umoja wa Utatu, pamoja na uzima wa milele.
Sala: Bwana Yesu Kristo, wewe ndiwe Mshindi juu ya dhambi zote, Shetani na hukumu. Wewe ndiwe uishiye milele, Mfalme pamoja na Baba katika umoja na Roho Mtakatifu. Tunakushukuru sana, amina.
Swali 117: Tunajifunza nini kutokana na jambo la hakika kwamba, miguu ya Kristo ilibakia bila kuvunjwa?