Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 102 (Jesus intercedes for his apostles)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
E - Maombezi ya Yesu (Yohana 17:1-26)

3. Yesu anaombea mitume wake (Yohana 17:6-19)


YOHANA 17:9-10
“Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.”

Maombezi ya Yesu yalikuwa kwa ajili ya wote waliomwamini Mungu, aliye baba, mwenye umoja na Mwana kwa milele na milele. Yesu hakufikia hapo kwa ajili ya ulimwengu wote, kwa vile kwa jumla binadamu walikataa Roho ya Bwana, na hivyo kuchagua hukumu. Upendo na utunzaji ambazo Yesu alizozionyesha zilishughulikia Kanisa lake na waliochaguliwa na Mungu. Ukristo hautambui kanisa la ulimwenguni kote linalowapokea wanadamu wote, kwa sababu Kanisa lililochaguliwa kutoka kwa watu ni lingine, ni matunda ya kwanza ya kifo cha Kristo.

Yesu hakufanya dai awe na milki ya pekee kwa ajili yake, lakini tena na tena alishuhudia kwamba hao ni milki ya pekee ya Babaye, ingawa Baba alikuwa amempatia yeye. Mwana aliendelea kuwa mnyenyekevu, naye akawakabidhi walio wake kwa Baba katika sala.

Yesu alithibitisha kwamba alikuwa ametukuzwa ndani ya wale waliomtegemea, wakati sisi tu wepesi kunung’unika na kusema kwamba Makanisa yetu ni dhaifu na kumwaibisha Kristo; Basi, yeye hupima kwa ndani zaidi kuliko maneno hayo. Baba atuona ndani ya nuru ya msalaba. Yeye alimwaga Roho yake ndani ya waumini kwa njia ya Mwana. Kule kumwaga hivyo kiroho ilihakikisha kwamba Msalaba ulifaa kabisa. Kristo hakufa bure, lakini Roho Mtakatifu hutokeza matunda tele. Hivyo kila mmoja wa kuzaliwa mara ya pili huleta utukufu kwake Kristo.

YOHANA 17:11
“Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.”

Kristo alikuwa akirudi kwa Babaye, akiwa na hakika kwamba itatokea hivyo, ingawa msaliti alikuwa akikaribia pamoja na genge la askari ili wamkamate. Yesu aliweza kutazama hadi ng’ambo ya kifo chake, akiona utukufu wa Babaye, akitabiri, “Mimi simo tena ulimwenguni” iwapo bado alikuwa hapo ulimwenguni.

Yesu aliangalia ulimwengu kama mto pana na maji yake kukimbia na upesi zaidi, na mara kwa mara kuingia katika hali ya poromoko ya maji, yakitelemka toka juu. Kristo akiwa akiogelea kukata maji na kutaka kugeuza mwelekeo wa watu. Alifahamu kwamba wanafunzi wake hawatakuwa na nguvu ya kushindana na maovu. Basi akamwuliza Baba awatunze wapendwa wake ndani ya usalama wa jina lake.

Katika maombezi yake Yesu alitumia matamshi ya pekee, “Ewe Baba Mtakatifu”. Usoni pa maovu mengi mno ya dunia, Mwana alishuhudia kwa utukufu wa Babaye, aliye bila waa, pasipo hatia na bila makosa. Mungu Baba ndiye msafi na takatifu. Utakatifu wake ndiyo vazi la upendo wake, wakati utukufu unaenea ndani ya mwangaza wa upendo wake.

Hivyo jina takatifu la Mungu ni kingo ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kujikinga na utawala wa mwenye kujaribu. Yeye aishiye ndani ya Kristo naye aishi ndani ya Baba. Ubaba wa Mungu awahakikishia watoto wake kwamba, atawatunza ndani ya utunzaji na ulinzi wake. Shetani hawezi kuwanyakua kutoka kwa mkono wa Baba.

Kanuni inayothibitisha ulinzi huo ni kwamba, wasiishi katika hali ya chuki na utepe, bali wasameheane kila siku na upendo wao kwa wao, tena unaodumu imara. Upendo wa namna hii hairuki kutoka kwa mtu kwa sababu ya asili au hali yake, lakini yeyote anayedumu ndani ya upendo wa Utatu Utakatifu atapokea nguvu, subira na upendo kwa ajili ya wengine. Kristo alimwuliza Baba atutunze ndani ya ushirikiano wake, tuwe kitu kimoja naye daima jinsi Mwana alivyo mmoja na Baba: Tamko hilo siyo kuchanganua namna ya kushikilia kanuni au maelezo ya kimawazo juu ya uhusiano wetu na Mungu, lakini ndiyo haja ya Yesu wakati wa kuaga pamoja na jibu la Baba. Imani yetu sio ya kiburi au ya ki-fumbo, hapana; bali ni tunda la sala ya Yesu pamoja na mateso yake kwa ajili yetu.

YOHANA 17:12-13
“Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.”

Kwa subira na busara Yesu aliwalinda wanafunzi wake na majaribu ya Shetani, mbali na tabia zao mbalimbali. Alimwambia Petro, “Shetani alitamani kukushika, lakini nimekuombea, ili imani yako isikose”. Basi imani yetu nao inashinda kwa sababu ya maombezi yake, nasi tunaokolewa kwa neema peke yake.

Uwezo huo wa kuwatunza wafuasi wake uliondolewa kwa Yuda, kwa sababu alijiachia kwa roho ya uharibifu, akizuia Roho ya kweli. Akapata kuwa mwana wa kupotea milele. Baba yetu wa mbinguni hamlazimishi mtu yeyote kupata zawadi ya kupokelewa kama mtoto. Anafahamu yaliyomo ndani ya vifua vya watu, pia na jinsi mambo yatakavyoendelea anafahamu mapema, kiasi kwamba hata usaliti wa Yuda ilikuwa imetajwa ndani ya Agano la Kale miaka elfu moja kabla haijatokea. Hata hivyo, Yuda aliendelea kuwajibika kwa kukataa shughuli ya Kristo kwa ajili yake. Mungu wetu mwenye enzi yote siye mwenye kutawala kwa ukali, lakini ni Baba mwenye hekima; namna moja ya upendo wake ni zawadi ya uhuru kwa watu, jinsi hata wakina baba wa duniani wanaruhusu watoto wao wazima wawe na uhuru na wajibike wenyewe.

Yesu aliona njia yake kwenda kwa Baba kama njia yenye nuru katikati ya giza. Si Shetani, wala dhambi, wala kifo ziliweza kuharibu njia yake ya kurudi kwa Mungu. Mwana alikua mtakatifu daima, na kwa sababu hiyo furaha ilijaa nafsini mwake. Dhambi haikutafuna kwenye dhamiri yake. Hofu haikuleta kivuli juu ya sala zake. Mwana alikuwa huru na kulindwa na Babaye, akiwa mtiifu kila wakati. Mungu wetu ni Bwana wa furaha na uchangamfu. Yesu alimsihi sana Babaye kwa ajili ya hiyo uchangamfu tukufu kukumbatia mioyo ya wanafunzi wake. Hakupenda wafuasi wake wawe na huzuni, bali aliwataka wajae raha na kufurahia, ili furaha ya mbinguni iwe yao, ingawa kuishi kwao ni kati ya giza ya dunia na hali yake ya kukata tamaa. Furaha ya kuwa radhi na shukurani kwa ajili ya nafasi yetu ndani ya familia ya Mungu ndiyo matunda ya maombezi ya Kristo kwa ajili yetu.

SALA: Bwana Yesu, asante kwa kutuombea kwa Baba. Tunakusifu kwa ajili ya kututunza katika imani kwa njia ya maombezi yako. Tunakuabudu kwa ajili ya wewe kutufurahia. Kuwepo kwako na Roho wa Baba zinatujalia utajiri wa kiroho ndani yetu, pia na kubarikiwa milele. Tunakushukuru kwa ajili ya sala zako kwa ajili yetu; tunaishi hata sasa kwa ajili ya maombezi yako.

SWALI:

  1. Jambo gani linaonyeshwa wazi kutokana na utunzaji wetu katika jina la Baba?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:59 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)