Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 101 (Jesus intercedes for his apostles)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
E - Maombezi ya Yesu (Yohana 17:1-26)

3. Yesu anaombea mitume wake (Yohana 17:6-19)


YOHANA 17:6
“Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.”

Baada ya Yesu kujihakikishia kwamba, Baba atamtia nguvu kwa kukamilishia ukombozi, na alipojua kuwa utukufu wa Babaye utaongezeka kwa kuzaliwa kwa watoto wengi wa kiroho na kurithiwa uzima wa milele, basi mawazo yake yakasogea kwa wanafunzi wake, ambao aliwachagua kutoka kwa ulimwengu na kuwaunganisha katika umoja tukufu.

Kristo alitangaza jina mpya ya Mungu, ambalo ni “Baba”. Kwa tamko hilo wao wakapata kuwa watoto wake, waliochaguliwa kutoka katika ulimwengu. Namna hiyo ya kuishi ndiyo siri ya Kanisa. Maana wale waliozaliwa na Mungu sio mali yao wenyewe, bali ni ya yule aliyewapa kuzaliwa kwa upya, na aliwaweka kuwa wa Mwana wake, kwa vile wamenunuliwa kwa damu yake. – Na wewe, ukiamini ndani ya Kristo, nawe utakuwa mali yake.

Ubaba huo tukufu pamoja na waumini kufanywa watoto wake, hayo yalikamilika ndani ya wanafunzi kwa njia ya imani yao ndani ya Injili, pamoja na kushika neno lake la thamani. Maneno hayo siyo ya kulialia tupu wala si mvuke wa kupotea, jinsi zilivyo herufi nyingi nyingi nyeusi zinazochapwa katika magazeti ya dunia. Hayo ni Neno la Mungu pia ni herufi zinazofurika na enzi ya uumbaji. Yule ayashikaye maneno ya Baba ndani ya moyo wake, ataishi ndani ya hiyo enzi yake.

YOHANA 17:7-8
“Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.”

Neno la Mungu linalobebwa na Yesu linaumba ufahamu wa kuokoa, ili kubadilisha maisha yaliyokuwa yameharibika. Yesu aliishi kufuatana na ujumbe wake, pia na kukamilisha matendo yake kwa enzi ya “Neno la Mungu” lenyewe. Nguvu zake zote na baraka zake zinatujia kwa njia ya Neno la Baba. Mwana hakudai ufahamu wa binafsi, lakini aliweka enzi yake, nguvu na hekima na upendo, yote kwake Mungu aliyemjalia kupewa.

Kristo alitutolea mali yake ya thamani mno: Neno la Baba. Yote yalitoka kwake Baba, hata Mwana akapata kuitwa “Neno la Mungu mwilini”. Ndani ya neno hilo pia kuna nguvu zetu. Hivyo tunatambua nguvu ya neno hilo na kupata kumulikiwa nalo. Tumepokea alama hizo na maneno hayo kwa furaha sana. Mafululizo ya Injili yanatuwezesha kupambanua hali halisi ya kuwepo kwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Hapo tunamkuta Kristo akifunua katika sala yake ule undani wa wanafunzi wake na ufahamu wao juu ya maneno yake, maana alikuwa amepanda mbegu za imani ndani ya mioyo yao. Walipokea maneno yake kwa furaha, ingawa sio mara moja. Ndipo alikuwa amemwaga Roho yake juu yao; neno likakua na kuleta matunda kwa wakati wa Mungu. Kristo alitabiri hilo mapema kwa imani, kwamba matokeo hayo yatakuwepo kwa uhakika.

Maneno yake Kristo yalizaa imani pamoja na ufahamu ndani ya wanafunzi. Imani hiyi ilikuwa juu ya nini? Kule kutokea kwa Mwana kutoka kwa Baba, kuwepo kwa huyu wa Milele ndani ya wakati wao, utukufu wake takatifu kuingia ndani ya namna ya mwanadamu, upendo wake dhidi ya chuki, enzi yake ndani ya udhaifu, uungu wake, iwapo alikuwa katika hali ya kutengwa na Mungu msalabani, pia na uhai wake ng’ambo ya mauti. Roho Mtakatifu alikuwa amewaimarisha ndani ya Mwokozi wao, nao wakapata kuwa viungu katika mwili wake (kanisa). Hawakusinzia muda katika hali ya kusadiki kiakili tu, lakini walishikamana naye kwa moyo wote, naye akidumu ndani yao kiroho. Hivyo wakapata kutambua kwa njia ya kazi ya Roho ndani yao kwamba, uungu wa Kristo uliingia mwilini.

Katika kuwepo kwake Kristo hivyo, wanafunzi wakagundua namna ya usawa na kuzaliwa kwao maalum, wakigundua fumbo la neno la Yesu akisema, “Yule aliyezaliwa na Roho ni Roho”. Huyu Roho mbarikiwa ndiye enzi tukufu ndani ya miili ya wanafunzi. Naye huja kwa njia ya maneno ya Yesu.

SALA: Bwana Yesu, asante kutupatia maneno ya Baba yako – maneno yajaayo uhai, nguvu na enzi. Wewe umezalisha imani na ufahamu ndani yetu. Wewe ndiwe nguvu yetu, tunakupenda na kukutukuza pamoja na Baba, aliyekutoa wewe kwetu.

SWALI:

  1. Ipi ni maana maalum ya kufunuliwa kwa jina la Baba kwa njia ya Yesu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)