Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 100 (Introduction to the intercessory prayer; Prayer for the Father's glory)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
E - Maombezi ya Yesu (Yohana 17:1-26)

1. Utangulizi kwa sala za kutuombea


Yesu alihudumia hali ya utu mwema kwa Injili na matendo yake; akiwaponya walemavu; akiwalisha wenye njaa; akifungua macho ya vipofu na hata kufufua wafu. Upendo wake ulikuwa ni ufunuo wa utukufu wa Mungu kati ya hali ya chuki na kifo.

Mwanzoni mwa huduma yake umati wa watu walimzunguka. Wakati baraza la kidini la Wayahudi (wengi wao walikuwa washupavu na wanafiki) walipotambua kwamba, misingi ya dini yao na usheria wao ulianza kutapatapa, walimtisha Yesu na wafuasi wake kuwatenga, hata kuwaua. Basi uchangamfu wa maelfu ya watu ulififia na wakaondoka kwake. Wakati huo Kristo na baadhi ya wafuasi wake walionewa, hata hivyo yeye aliendelea kuwapenda wote.

Mwishowe maenezi ya baraza yalimshika mmoja wa hao thenashara (wanafunzi wake 12); huyu akaandaa namna ya kumsaliti Bwana wake, huku Yesu alikuwa akiwaandaa hao waliokuwa wake hasa wakati wa chakula cha agano cha jioni kwa ajili ya huduma yao kuwa mitume. Katika kuwaaga aliwatangazia umoja wake na Baba, na jinsi huyu Roho Mfariji atakavyowaimarisha katika ushirikiano wa upendo tukufu, mbali na mateso yatakayowapata.

Lakini wanafunzi walishindwa kutambua makusudi ya Bwana wao, kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajamiminwa ndani ya roho zao. Basi Yesu akaenda kwa njia ya sala moja kwa moja kwa Babaye akajikabidhi kwake na wafuasi wake mikononi mwa Baba yake kwa namna ya sala ya maombezi. Pia aliwataja na wale ambao baadaye wataamini kwa njia ya ushuhuda wa hao mitume.

Sala ya maombezi ya Kristo, jinsi ilivyokaririwa katika sura ya 17, kipekee inatupatia picha ya namna jinsi Mwana wa Mungu alivyoongea na Babaye, na aina ya upendo kati ya nafsi tatu ya Utatu Utakatifu. Namna ya roho ya maombi inajitokeza wazi hapo. Yeyote atakayechimba chini ndani ya sura hiyo, ataingia ndani ya hekalu la Mungu, ambapo ibada na maombezi yanaenea.


2. Sala kwa ajili ya utukufu wa Baba (Yohana 17:1-5)


YOHANA 17:1
“Maneno haya aliyasema Yesu akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;”

Kristo aliwatangazia wanafunzi wake kwamba, yeye alikuwa mmoja na Baba. Yeye yu ndani ya Baba, na Baba yu ndani yake. Yeyote atakayemwona yeye atakuwa amemwona na Baba. Lakini wanafunzi walishindwa kutambua ufunuo huo wa ajabu. Akili zao zilihangaika walipojaribu kutambua kuwepo kwa huyu Mtukufu ndani ya mwili. Basi Yesu alikabidhi hao wanafunzi wake wadhaifu na kijinga kwenye uangalizi wa Babaye, ili wamulikiwe na kutunzwa katika ushirikiano wa upendo tukufu na takatifu.

Kwa kuinua macho yake kuelekea mbinguni pengine Yesu angewashangaza hao wanafunzi. Jinsi gani alikuwa akiomba kwa Babaye mbinguni, huku akisema kwamba anaishi ndani ya Baba na Baba ndani yake? Ishara hizo ambzo hazikuweza kutambulikana zilihangaisha akili zao. Sisi tunafahamu kwamba mawazo hayo mawili yote ni kweli: Umoja kamili kati ya Baba na Mwana, na vilevile upekee wa kila nafsi, ya Baba na ya Mwana. Mungu ni mwenye enzi zaidi sana kupita akili zetu, na Roho Mtakatifu hutufundisha kutunza mawazo yote mawili kuwa kweli. - Umwombe Mungu kukumulikia, ikiwa ufahamu huo unakuwa ngmu kwako. Hata hivyo hakuna awezaye kuelewa kwa ndani kabisa habari ya Baba na Mwana, ila kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu.

Katika sala hiyo Yesu alimwita Mungu: Baba. Maana Mungu siyo Bwana mtakatifu tu, na Mhukumu wa kuogofya, lakini upendo wake wa rehema unafunika namna zake zingine zote. Mungu nafsini mwake ni upendo takatifu na kweli yenye rehema. Wazo hilo mpya juu ya Mungu kama Baba mwenye kupenda lilijitokeza Yesu alipozaliwa kutokana na Roho Mtakatifu, ya kuwa Mwana wa Mungu. Alikuwa akiishi milele na Mungu, lakini akaingia mwilini, ili atukomboe tuwe watoto wake yule Mtakatifu. Ufunuo huo wa jina la Baba kwa ajili ya Mungu ndiyo kiini cha ujumbe uliotolewa na Yesu kwa ajili ya ulimwengu. Kwa njia ya ukweli huo uliofunuliwa na Roho, Yesu alituweka huru na hofu ya hukumu, tangu huyu hakimu amekuwa Baba yetu, na mthibitishaji amekuwa Ndugu yetu, aliyelipia madeni yetu. Unapotambua jina la Baba ndani ya matamshi mengi ya Yesu akisema ndani ya roho zetu, na ukiishi kufuatana na ufahamu huo, utakuwa umefaulu kushika ujumbe wa Injili.

Kristo alithibitisha mbele za Baba yake kwamba, saa muhimu kuliko zote ilipiga kwa ajili ya ulimwengu, saa ya ukombozi kati ya Mungu na binadamu. Wanadamu kwa jumla, pia na malaika, dini zote na mafafanuzi yote ya maana ya uhai zilikuwa zilingojea bila kutambua saa hiyo muhimu kabisa. Ikatimia ! Kristo alikuwa amejitwisha hatia yote ya dunia kwa kukubali kuwa Kondoo wa Mungu. Akawa tayari kufa kwa upweke katika mwali wa moto wa ghadhabu ya Mungu. Katika dakika hizo za dhahiri huyu mdanganyi alikuwa akikaribia barabarani pamoja na kundi la polisi la hekalu, ili wamfunge Mwana wa Mungu, huyu Mwana wa Adamu, mnyenyekevu na mwenye nguvu, aliyekuwa tayari kufa bila ulinzi wowote.

YOHANA 17:2
“kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote mwenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.”

Wengi wanafikiri “utukufu” inamaanisha kung’aa na kutoa nuru. Yesu alikiri kwamba upendo wake wa kujitoa kuwa sadaka, hilo ndilo msingi wa utukufu na kiini cha kuwepo kwake tukufu. Alimwuliza Baba yake kumtunza katika upendo huo, hasa kwa saa zile akiwa juu msalabani, katika dhoruba kali za maumivu na hofu, ili na miali ya upendo tukufu ing’ae kwa ukamilifu ndani ya msulibiwa. Mwana alikuwa tayari kujitoa kuwa dhabihu kwa ajili ya waasi na wahalisi, ili na wao waweze kuthibitishwa kuwa na haki kwa njia ya kifo chake. Hii ndiyo kiini cha utukufu wa Mwana.

Wala yeye hakunyamaza , akasema kwamba haendi kufa kwa ajili yake mwenyewe, ila kwa ajili ya utukufu wa Baba, na ya kwamba alishughulikia jambo kuu, ambalo hakuna mwingine wa kuliweza. Alimtukuza Baba akiwa msalabani akikamilisha upatanisho wa binadamu na Mungu. Dhambi inapopata kusamehewa, upendo wa Mungu unajionyesha wazi, na wote wanakaribishwa wapate kupokelewa kama watoto. Roho Mtakatifu huwa anamwagwa juu ya waumini ndani ya Kristo, ili na hao watoto wapate kumtukuza Baba yao kwa namna ya kutembea kikamilifu katika usafi. Haiwezekani kuwa na alama kubwa zaidi kwa ajili ya kutukuzwa kwa jina lake Baba kuliko hilo la kupata kuwa Baba kwa ajili ya watoto wengi. Hivyo Yesu aliuliza kukamilisha huo upendo wa kukomboa kwa njia ya kuzaliwa kwa watoto wengi ndani ya Roho na ukweli kwa ajili ya kutukuza hilo jina la ki-baba.

Mwana alitwaa tena dai lake tukufu kwamba, Baba alikuwa amemkabidhi enzi yote juu ya hao wote waliozaliwa na wanawake. Kristo ndiye Mungu wa kweli, Mwumbaji na Mwokozi . Yeye ndiye Bwana wetu, Mfalme na Mhukumu. Sisi tu wake na yeye ni tumaini letu la kweli. Yeye alipokea hiyo mamlaka aliyokabidhiwa, si kwa hukumu na uharibifu, bali kwa ajili ya kuokoa na kuongoza. Shabaha ya kuja kwake Kristo ni kwamba, wamwaminio waweze kujaliwa uzima wa milele. Mauti haiwezi kupata kutawala juu yao. Msalabani Yesu alisamehe dhambi za binadamu wote. Ingawa ni wachache wanaoitikia kwa toleo lake la wokovu, waumini ndiyo kama taifa teule, wanaoamini ndani ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu na kudumu ndani ya utukufu wa Kristo unaookoa. Ndani yao Roho tukufu inaendelea kudumu. Hali yao mpya ndiyo mwujiza wa nyakati zetu, wakitukuza jina la Baba.

YOHANA 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Roho Mtakatifu anathibitisha yale ambayo Yesu alisema juu ya Mungu. Kwamba Yeye ni Baba wa Kristo na wa kwetu. Yeyote atambuaye siri hiyo tukufu na kuamini ndani yake, anayo uzima wa milele.Hakuna ufunguo nyingine wa kupata kumfahamu Mungu ila ndani ya nafsi ya Yesu Kristo tu. Yeye aonaye ndani ya Mwana ule ubaba wa Mungu, na akitegemea ndani yake, anakuwa amebadilishwa ndani ya hali takatifu ya kuwa mtoto wa Mungu. Ufahamu wa kustaajabu ndani ya tamko la Kristo sio ya ki-sayansi, lakini ni kuwa na hali ya kiroho na kupata kuendelea kuwa hali hiyo. Mungu hurudisha sura yake ndani ya kila mwumini. Ni nini hilo la ajabu katika sura hiyo tukufu? Jibu ni upendo, kweli na uaminifu, ambazo Roho Mtakatifu anazijenga ndani ya watoto wa Mungu. Pamoja na hayo ni kumtukuza Baba, na hivyo kutaja na kuthibitisha sifa zake.

Kristo alitumwa na Mungu ulimwenguni, ili watu waweze kutambua kwa mwenendo wake kwamba, mbali na yeye aliyezaliwa na Roho, aliyesulibiwa na kufufuka, hawataweza kamwe kumfahamu Mungu. Mwana ndiye Mtume tukufu, aliyejumlisha enzi yote nafsini mwake pamoja na upendo na utakatifu. Wewe ukipenda kumfahamu Mungu wa kweli, chunguza maisha ya Yesu ambaye ndiye sura ya Uungu, aliyetiwa mafuta na Roho. Akiwa Masihi, yeye naye ni Mfalme wa Wafalme, pia na Kuhani Mkuu, pia na nabii kamili na Neno la Mungu aliyeingia mwilini.

YOHANA 17:4-5
“Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.”

Wakati wa matembezi yake duniani, wakati wowote Yesu alitafakari habari ya Baba, akamshuhudia na kuendeleza kazi zake hadi mwisho. Alijikana mwenyewe ili kumtukuza Baba. Yote aliyoyasikia kwa Baba akaipitisha hadi kwetu. Maisha yake yote yakamtukuza Baba, akitegemea kabisa kwamba maombi yake yatajibiwa. Akakamilisha shabaha ya ukombozi pale msalabani. Hata hivyo, kwake jambo hilo halikuwa la kujitokeza kwa kiburi, maana Baba yake alikuwa amemkabidhi huo utume, ili aukamilishe. Alithibitisha kwamba Baba alikuwa amekamilisha mambo yote. Tangu Yesu alipojimwaga kabisa, wala hakuchukua sifa yoyote kwa ajili yake mwenyewe, anastahili kwamba utukufu wa milele ungemrudia yeye. Hivyo alishuhudia kwamba alikuwa na utukufu tangu milele, Mungu kutoka kwa Mungu, nuru kutoka kwa nuru, kufayika wala sio kuumbwa. Baada ya kukamilisha makusudi yake alitamani sana kurudi kwake Baba. Alipofikia mbinguni, malaika na wenye uhai wengine wakamtukuza wakisema, “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uwezo na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.” (Ufunuo 5:12)

SALA: Baba wa mbinguni, jina lako litukuzwe. Mwana wako alikutukuza kwa namna alivyoishi kwetu, maombi yake na sadaka yake. Hatustahili kuinua macho yetu kuelekea kwako. Tunakushukuru kwa kuwa radhi nasi kwa kuvunja amri zako, kwa sababu Kristo alitufia; umetufanya tuwe watoto wako. Nakushukuru kwa kunihamisha ndani ya maisha ya milele kwa njia ya kumwaga Roho wako Mtakatifu ndani ya moyo wangu. Utusaidie kukutukuza daima, bila kujaribu kunyofoa sifa kwa ajili yetu sisi wenyewe, bali kutii agizo la Mwanawe kupendana sisi kwa sisi, hata wengine waweze kuona ndani ya matendo yetu mema ule ubaba wako, wakutukuze na kutamani na wao kuwa wako.

SWALI:

  1. Wazo kuu katika sehemu ya kwanza ya maombezi ya Yesu ni lipi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:57 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)