Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 099 (Christ's peace in us defeats the world's afflictions)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

6. Amani ya Kristo ndani yetu inashinda taabu za dunia (Yohana 16:25-33)


YOHANA 16:25-26a
„Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. Na siku ile mtaomba kwa jina langu; ...

Yesu alifunua ukweli juu ya mambo ya mbinguni kwa njia ya mithali na mifano, ambazo zilificha siri hizo mbele za watu wa kawaida ya dunia hii, ila kwa wale waliokuwa na njaa ya kuelewa yaliyo ya haki na unyofu, walipata kufahamu. Kwa wanafunzi wake Yesu alitamani wapate kumwelewa waziwazi, na alingojea kwa hamu siku ile kuu ambapo atafufuka kutoka kwa wafu, na ndipo kupaa mbinguni na kuketi mkononi mwa kulia kwa Mungu, ndipo kutuma Roho wake tukufu kwao. Alieleza mambo hayo makuu yote ya kuokoa kwamba, yatatokea kwa siku moja. Roho akijia mioyo ya wafuasi wake, mifano na mithali hizo zitakoma; maana Roho huyu wa Kristo ataumba mwangaza mioyoni mwa waumini wake na kukomesha wakati wa mifano kwao. Mungu ndiye Baba na Kristo ni Mwana wake. Bila kuwa na Roho Mtakatifu hakuna mtu awezaye kumfahamu Mungu, lakini Roho wa Mwana hutuvuta ndani ya familia ya Mungu. - Je, unayo baba hapo ulimwenguni? Unazungumza naye? Anakushughulikia? Hayo ni maswali ya mara moja. - Kwenye hali ya juu zaidi, maneno ya Yesu na faraja ya Roho yake yanatuhakikishia kwamba, Mungu ni mwenye enzi zote, Mtakatifu, na hata hivyo Mungu wetu wa binafsi na moyoni atupendaye sana. Sisi tu watoto wake wapendwa, iwapo wote bado tu wenye dhambi; lakini kwa ajili ya damu yake Kristo tumepata kuwa watakatifu mbele zake. Roho Mtakatifu atufugulia midomo yetu tuweze kutamka sala za kweli, kwa sababu Roho huyu ni ya Kristo. Katika sala za kiroho Kristo anasema kwa kupitia kwetu. Omba yale ambayo Roho anayaomba, tena kwa tumaini la Baba na ushirikiano na Mwana. Sala zako zitakuwa ni mazungumzo kati ya Roho aliye ndani yako na Baba yako wa mbinguni, ambaye ni mmoja na Mwana.

YOHANA 16:26b-28
“... wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda, kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; nakwenda kwa Baba.”

Baba fulani ambaye hawapendi watoto wake, yeye si baba. Kwa njia ya kufunua jina la Mungu, Yesu alitupatia mamna iliyo rahisi kabisa kwa kutambua kwamba, upendo wa Mungu ni wenye enzi kuu. Kutoa umaarufu kwa jina la Baba ndiyo kiini cha shabaha ya Kristo. Yule anayemfahamu Baba anamfahamu na Mungu, naye amebadilishwa kuwa mtoto wa Mungu, akidumu ndani ya upendo wake. Ndani ya jina hilo tunakuta Injili kamili na tumaini la uzima wa milele. Kristo hututangazia, kwamba tangu sasa hakuna haja ya uombezi kwa kupitia mwingine, maana Baba mwenyewe anakupenda, tena amejaa upendo na rehema. Tangu Kristo amekufa pale msalabani, hakuna kabisa kizuizi kati yetu na Baba. Imani ndani ya Mwana, aliye Kondoo wa Mungu, inamwezesha Baba kumwaga upendo wake juu ya wale wanaompenda Kristo. Anayetambua uungu wa Kristo, kutoka kwake kwa Baba na kuishi kwake ndani yake, basi huyu amekaribia kuelewa Utatu Utakatifu. Huyu anadumu ndani ya uhai wa Mungu, naye amejaa na rehema ya Baba, akifurahi daima rohoni.

Katika sentenso moja Kristo anafafaanua mwujiza wa ukombozi kwa wanafunzi wake. Alishuka kutoka kwa uungu wa juu kabisa, akaja na kutembelea dunia, iliokuwa imechekechwa na chuki na upotovu; lakini alipokamilisha haki msalabani kwa ajili ya binadamu, aliacha tena dunia na kurudi haraka kwa Babaye, aliye asili ya uhai wote.

YOHANA 16:29-30
“Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala husemi mithali yoyote. Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu.”

Wanafunzi walianza kutambua ukuu wa upendo wa Mungu na kuwepo kwake Yesu tangu milele. Yesu ndiye Mungu wa kweli, mwenye kujua yote, takatifu na wa milele. Lakini walishindwa kukumbuka kwamba yeye naye ni upendo ulioingia mwilini, naye hakumwita Mungu “Baba” kila mara, ingawa Yesu alikariri kweli hizo tena na tena. Wao walikubali mambo hayo kiakili, lakini walishindwa kuelewa asili ya kweli ya nafsi yake.

YOHANA 16:31-32
“Yesu akawajibu, Je, mnasadiki sasa? Tazama saa yaja, maam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.”

Kwa kukunja uso Yesu aliuliza, “Je, mnaelewa hayo kiakili tu na kutambua hali ya nafsi yangu? Na kujua hayo ni sawa na imani ya kweli? Kupima hayo kunataka kuja sasa, na itaonyesha kwamba imani yenu bado inapungua upendo. Mnashindwa kumwelewa Mungu zaida, kwa sababu hamwamini katika ubaba wake. Mtatoroka wote na kuniacha kama kunitupa. Imani yenu itajionyesha kwamba haijatulia.”

“Hata kifoni mimi si peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.” Je, hayo yanagongana na mlio wa Yesu msalabani, “Mungu wangu, mbona umeniacha?” La, kwa sababu Mungu Mtakatifu alificha uso wake kwa Mwana, lakini Kristo aliendelea kuamini kwepo kwake Mungu karibu naye. Mlio wake ulionyesha tu kwamba, Mungu anadumu bila kubadilika; “Sitakuacha, hata wakati nisipokuona. Mkononi mwako naitoa roho yangu,” akamalizia Yesu. Imani yake Kristo ndani ya ubaba wa Mungu ilishinda juu ya hukumu iliyomwangukia kwa ajili yetu sisi. Upendo wa Mwana kwa ajili ya Baba yake ulizimisha moto wa ghadhabu ya Mungu iliyoinuka kwa ajili ya deni kuu iliyotokana na dhambi zetu. Tumaini lake ambalo halikutisika ilitufungulia mlango tuweze kumwona Baba. Kwa sababu ya kufa kwake kwa uamuzi wa Baba sisi sasa twaweza kusema kila mmojawetu, “Mimi si peke yangu, kwa sababu Baba yu pamoja nami.”

YOHANA 16:33
“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”

Yesu alijumlisha hotuba yake ya kuwaaga kwa tamko la faraja kwa waumini wake wote, “Nimeishi kwa muda pamoja nanyi, nikiwafundisha kwamba amani tukufu ijae mioyo yenu. Wasioamini hawawezi kuwa na amani. Mimi Mwana, nimesamehe kabisa mioyo yenu, na kusafisha utu wenu wa ndani. Mimi nimemweka Roho yangu wa amani ndani yenu. Sasa mkadumu ndani ya maneno yangu. Mimi binafsi ndiye mwenye kuwapigania. Ninyi hamwezi kuwa na ulinzi nje ya mimi. Upatanisho wenu na Mungu ndiyo msingi wa amani hiyo. Hamwezi kuwa na dhamiri safi mbali na msamaha wa dhambi zenu ndani ya damu yangu. Mimi nimewaokoa na Roho yangu imo ndani yenu. Amani yangu sio njozi au ndoto lakini ni jambo la kweli. Mimi nawajia, ili kuwapatia amani; mwe mkiikubali tu na kuamini ndani yangu.”

“Msifikiri kwamba mwaweza kutazamia amani ndani ya ulimwengu huu. Hapana! Ila hatari nyingi zinajificha hapo na pale: Mateso, magonjwa, udanganyifu, hofu na kifo. Watu wa sheria watawakataza, wenye kutaghafali watawachokoza. Maelfu ya maongo na mawazo ya watu yatajaribu imani yenu. Kiburi nayo itakuwa karibu daima. Msipende pesa; utajiri haitawaweka katika hali ya usalama.”

“Kumbukeni upendo wangu na kuiga unyenyekevu wangu, mkadumu ndani ya mfano wangu wa kujitoa na kujikinahi. Mimi nimeushinda ulimwengu. Sikutaka chochote kwa ajili yangu binafsi. Mimi katika asili yangu ni Mtakatifu wa Mungu. Ndani yangu amri zote za Mungu zilitimizwa; “Uwe takatifu, kwa vili mimi ni takatifu”. Mimi ndimi ukamilisho la upendo; ndani yangu mtamwona Baba.”

Je, umefaulu kushika umuhimu wa hotuba ya kuaga ya Yesu? Yeye amekuweka ndani ya ushirikiano na Baba, ili na moyo wako ukubaliane na amani ya Kristo. Amani hiyo ndiyo ukweli muhimu kuliko mengine yoyote ndani ya maisha ya mwumini. Ulimwengu utaendelea kuwa ovu na wa kukusumbua. Lakini amani yako ndani ya Mshindi juu ya kifo na Shetani atakuweka huru na moto wa ghadhabu ya Mungu na mateso ya milele. Yeye aaminiye ndani ya Kristo atapokea rehema ya Mungu. Je, ujumbe huo kutoka kwake Yesu umekujaa? Roho Mtakatifu yu ndani yako akisema, “Baba ni wa kwangu, Mwana ni Mwokozi wangu, na Roho hutawala ndani yangu”? Mungu mmoja yu ndani yetu. Mimi nadumu ndani ya neema yake.

SALA: Bwana Yesu Kristo, wewe umeshinda moyo wangu, umeninunua kwa ajili yako. Umenitunza ndani ya ulinzi wako kutoka kwa mitego ya shetani, na umeniweka huru na kifungo cha maongo yake. Umenijalia uhai wa milele. Sina hofu tena ya kifo, kwa sababu nakungojea wewe. Nitunze ndani ya mapenzi yako na kunijalia nguvu zako, ili nipate kukutukuza pamoja na watakatifu wote na kumhimidi Baba. Unisaidie kuwapenda ndugu, nikiwasamehe, na niwe mwenye kuleta amani kwa kuongozwa na wewe. Nakutegemea, wewe ndiwe Mshindi.

SWALI:

  1. Kwa nini na jinsi gani Mungu Baba anatupenda?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:56 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)