Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 098 (Christ predicts the joy of the disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

5. Kristo alitoa habari mbele kuhusu furaha ya wanafunzi kwenye sikukuu ya ufufuo (Yohana 16:16-24)


YOHANA 16:16-19
“Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo. Yesu alifahamu ya kwamba, wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?”

Wakati wa jioni ile Yesu alisema mara tatu habari ya kuondoka kwake.Hilo la kurudia kusema iliwashitusha wanafunzi wake; walishindwa kushika kusudi lake. Lakini pamoja na hayo aliwaahidia kurudi kwake, akimaanisha kwanza habari ya kufufuka kwake kutoka kaburini, lililotokea sikukuu ya Pasaka, mapema baada ya hapo. Ndipo aliwatokea wanafunzi wake akipita kati ya kuta za chumba (au kuingia chumbani walimokuwa bila kufungua mlango). Hili lilikuwa la kuwaambia “kwa heri” njiani kwenda kwake kwa Baba.

Yesu alipofanya utabiri huo wakati wakipanda jioni ile kwenye mlima wa mizeituni, basi walishindwa kumfahamu. Ingawa hata kabla ya hapo alikuwa amewaelezea mpango wa kuondoka kwake. Na sasa akawaambia habari ya kwamba kutengana naye ilikuwa usoni. Walikiri kwamba mpango huo na makusudi yake bado ilikuwa kama fumbo kwao. Walifadhaishwa na kuchanganywa, tena walihuzunishwa kwa ajili ya kurudi nyumbani kwake mbinguni.

YOHANA 16:20-23
“Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. Mwanamke azaapo yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.”

Yesu alisoma mawazo ya wanafunzi wake, tena alielewa yale waliyosemezana, iwapo hakuwa karibu kasi cha kuwasikiliza. Katika kuwajibu mashaka yao, hakutuliza tu hofu zao au kumulikia mashaka yao, lakini alikaza kwamba, maumivu mengi, machozi na kuhuzunika yatashika maisha yao hivi karibuni. Ilikuwa kama kifo cha mfalme mwema; watu walihangaika na kutupa matumaini mbali. Wakati wanafunzi watakapohuzunika, maadui zao watakuwa wanashangilia. Kwa neno la “maadui” Yesu alimaanisha ulimwengu kwa jumla, wala si viongozi wa wayahudi tu. Yote yaliyo nje ya Kanisa la Kristo wako upande wa dunia inayopotea, mbali na Mungu, tena waasi dhidi ya Roho Mtakatifu.

Na zaidi, Yesu aliwaahidi wanafunzi wake kwamba, watapata kuona furaha kuu. Saa za machozi na kuhuzunika zitakuwa fupi tu, kama vile maumivu ya ghafula ya kuzaa kwa mwanamke. Wakina mama huhesabu maumivu hayo kwamba yanabebeka kwa tazamio la furaha ya kushika mzaliwa mpya mikononi mwao.

Wakati wa ufufuo maswali yote upande wa wanafunzi yatatulizwa na kuwa kimya. Hasa jambo kuu la hatia yao itakuwa imetengenezwa kwa ajili yao, hata shida ya mauti itakuwa imeshindwa; utawala wa Shetani itakuwa imebomolewa, na ghadhabu ya Mungu haitawatisha tena kama ajali ya kuwapata. Ukani wao, hofu na kutokuamini kwao hautakataza kurudi kwake Kristo wala msamaha wake. Wayahudi hawataweza kuwashika, maana Bwana atawatunza. Hivyo maswali yao yote na kufadhaika kwao zilizowasumbua zitakuwa zimepata jibu na kupona siku ya ufufuo ndani ya nafsi ya huyu Mfufuka.

YOHANA 16:24
“Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.”

Mwanzoni mwa maneno yake ya kuwaaga , Yesu aliwataka wanafunzi wake wamwulize lolote wanalohitaji, akiongeza kwamba watapewa; na hivyo Baba yake angetukuzwa (Yoh.14:13). Maombi hayo yangehusika na kukua kwa Kanisa na kazi za uinjilisti, maana Yesu anatamani wengi wapate kuingia katika ushirikiano wa upendo wa Utatu. Hivyo alitusihi, “Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, ndipo na mengine yote mtaongezewa nayo”. Yesu anaahidi kwamba Mungu anajibu maombi ya watu yahusuyo mambo ya mbinguni hata ya duniani; hata hivyo, ya mbinguni yatatangulizwa mbele ya mambo mengine ya dunia.

Je, yapi ni maswali yako au mahitaji ya moyoni mwako? Unahitaji fedha, afya na kufaulu kikazi? Unaomba uweze kupata uhusiano njema kati yako na wengine? Au kuna mashaka kuhusu kuwepo kwa Mungu na kuhusu rehema zake kwako yanayokusumbua? Unajisikia tupu kwa sababu ya kukosa kuwa na nguvu ya Roho maishani mwako? Unasikia mzigo wa hatia maishani mwako na unateseka kutokana na majaribu, uharibifu fulani au kudhulumiwa? Je, unatetemeka kwa sababu ya roho za ubaya zikikusumbua? - Unangojea kurudi kwake Kristo na kuanzia kwa utawala wake wa amani? - Maswali gani yanayosumbua roho yako, akili yako na hata mwili? Je, wewe ni mtu wa haraka haraka au mwenye bidii sana? Ni wa kutazamia yote mema au mwenye tabia ya kuona yote kwenda vibaya? Unasikia kuumizwa haraka? Au je,unaweza kumwuliza Bwana wako akujalie kujazwa na Roho Mtakatifu?

Basi fanya tatizo lolote la kwako kuwa jambo la kuombea. Fungua moyo wako kuelekea kwa Baba yako ya mbinguni. Lakini usipayuke katika sala zako, bali tafakari vizuri juu ya yale unayohitaji kuomba. Kumbuka kwanza vipawa na uwezo ambayo Yesu alikwisha kukujalia ukimshukuru kwa yote hayo. Shukrani inastahili sana kila wakati. Ndipo ukiri makosa yako, kwa sababu ya upungufu wa imani, upendo uliopoa na tumaini la wasiwasi tu ni mambo yasiofaa mbele za Mungu. Omba msamaha kwa ajili ya dhambi ulizokiri , na umwombe akuonyeshe yale anayoyahitaji kwako, ili usije ukaomba mambo yasiyokufaa. Uhitaji neema yake na umtumaini kwamba atakusikia. Usisahau kabisa kwamba Mungu ni upendo, na anapenda kubariki wengine nao. Ufanye maombezi kwa ajili ya rafiki zako, pia na kwa ajili ya adui, ili Mungu awaguse na kuwabariki na neema sawa na wewe. Wewe siye mtu wa pekee wa kuhangaika na mwenye mahitaji. Watu wote hushiriki katika hali halisi hiyo ya matatizo. Toa mahitaji yako kwa uthabiti, kikamilifu, tena moja kwa moja kwake Kristo ukisuke na kuvisha shada la maua ya shukrani kwa unyenyekevu kwa shida zako zote. Na usisahau maombi kwa ajili ya wengine. Ndipo utapata kujifunza siri za sala za kweli katika jina lake Yesu.

Sala hasa ni kuongea na Mungu kuhusu mahitaji, shukrani na kumtukuza. Usikaze sana katika mazungumzo hayo kwa kutumia maneno ya makelele. Sema tu yale unayoyawaza katika maneno rahisi, kana kwamba unaongea na mzazi wako. Yule mtoza ushuru pale hekaluni alihesabiwa haki aliponong’ona tu, “Bwana, nihurumie mimi mwenye dhambi.” Baba wa mbinguni alimfufua Lazaro toka kifoni, Kristo alipoomba kwa urahisi kwamba, amfufue Lazaro. Ni imani inayojaliwa wokovu, au mafanikio. Usisite kumwomba Mungu kwa neema, ushujaa na shukrani. Unaitwa mtoto wake, hivyo tamka kwa furaha kama mtoto, wala usifiche lolote mbele zake.

Kristo anatamani kukujalia furaha yake; si kwanza kwa ajili ya itiko kwa sala zako, bali kwa ajili ya mapendeleo uliyopata kuhudhuria mbele za Mungu na Mwana wake katika sala za kuwahimidi. Jambo gani kwako ni muhimu zaidi je, zawadi au mtoa zawadi? Bwana hukupatia ya ukamilifu, upate kukumbuka kwamba yeye nafsini mwake ni mkamilifu. Yesu ahitaji furaha yetu iwe imekamilika. Basi, furaha iliongezeka ndani yetu, tulipotambua kwamba Yesu alijibu sala zetu sisi tulio wenye upungufu wakati wowote. Tena aliwabariki wengine na kuwaokoa kwa sababu ya sala zetu. Ndipo furaha yetu itaweza kuwa shangwe kuu tutakapomwona Yesu akirudi katika mawingu ya mbinguni. Ndipo basi furaha yetu itakuwa kuu, ng’ambo ya uwezo wa kutamka. Je, kurudi kwake Yesu kwa utukufu itakuwa ni jambo kuu kuliko yote kwako, hata katika sala zako?

SALA: Baba wa mbinguni, twakushukuru kutoka kwa kiini cha mioyo yetu, kwa sababu ulimtuma Mwana wako kwetu kuwa Mwokozi wetu. Tusamehe mahangaiko yetu ya kidunia, na utusaidie kutambua umuhimu wa msalaba wako. Utuweke huru kuweza kuomba kwa namna ya kuweza kusikilizwa na kujibiwa. Tuseme nawe kama watoto kwa wazazi wao katika urahisi na wazi kabisa. Waokoe pia na adui zetu, maana ni wenye shida na chini ya mizigo ya dhambi zao, wakiumizwa vibaya katika mioyo inayojaa upuzi na chuki. Waweke huru na mapingu yao, ili wao nao wapate kushiriki furaha ya kuwepo kwako maishani mwetu.

SWALI:

  1. Jinsi gani Mungu Baba anajibu sala zetu katika jina lake Yesu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)