Previous Lesson -- Next Lesson
4. Roho Mtakatifu hufunua maendeleo ya ajabu kabisa katika historia (Yohana 16:4-15)
YOHANA 16:12-13
“Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.”
Kristo ndiye mjua-yote, akipenda kuwajulisha wapendwa wanafunzi wake habari za siri za mbinguni na za wakati ujao; lakini uwezo wa roho na akili zao hazikuweza kushika kweli hizo kwa ukamilifu. Basi, hata sisi hatuwezi kutambua kiakili, kwamba Kristo sasa ameketi upande wa kulia kwake Mungu mbinguni, na hata huku kwa wakati uo huo kuishi ndani ya mioyo yetu; tusipojulishwa na nuru ya Roho ndani yetu na kumulikiwa naye. Vilevile, hatuwezi kwa kawaida yetu kutambua kwamba Mungu ni mmoja ndani ya nafsi tatu. Jambo hilo ubongo wa binadamu haiwezi kutambua, lakini Roho atusaidia katika kutokuweza kwetu na kumulika akili zetu. Yeye aweza kufunua siri za wakati ujao kwetu, pia na mawazo yaliyofichika mioyoni mwa watu, maana anaelewa yote ya ndani kabisa ya Roho Mtakatifu.
Kristo alitabiri habari ya Roho wa kweli atakayekuja na kwamba atawaongoza katika kila ukweli. Ukweli ni nini? Yesu hakutumia neno la ukweli kama ni kweli za aina mbalimbali, kana kwamba anaeleza mambo ya kidunia, lakini alisema habari ya ukweli moja tu alipotamka, “Mimi ndimi ukweli”. Ufunuo kuhusu kuja kwa Roho ina maanisha kwamba atatuongoza katika ukamilifu wa Kristo katika utendaji wake na asili yake. Hivyo, Yesu siye mwanadamu wa kawaida tu, bali Baba yu ndani yake, pia na yeye ndani ya Baba. Na kwa hiyo kuongozwa katika kila ukweli inamaanisha ufahamu juu ya Baba na kudumu kwetu ndani ya upendo wake na kuishi kwetu milele. Neno la “Ukweli” ndani ya injili haimaanishi kweli ya kisheria au kukubalika kiakili kuwa ni jambo la kweli, wala si hali ya kweli katika maana ya maadili tu; lakini maana yake ni pana zaidi na kufunika mambo yote kwa jumla na pia jambo moja moja.. Hivyo Roho hutuongoza kutambua ukweli wa mbinguni, ili tumfahamu Mungu katika Utatu na kuelewa enzi zake za ajabu.
Kwa mambo hayo yote Roho Mtakatifu ni nafsi anayejitegemea, akisema, akisikiliza, mwenye mapenzi ya huru, lakini wakati uo huo hatendi lolote lisilopatana na mapenzi ya Baba. Hatokei na mawazo ya kipekee, lakini anatujulisha yale ambayo Baba aliyasema. Ndani ya Utatu Utakatifu hakuna lolote ila utii wao kwa wao ndani ya uhuru wa upendo. Yeye ni mwaminifu katika ushuhuda wake anayotuletea kutoka kwa Mwana wa Mungu. Kwa namna hiyo anapenda kukuza Kanisa kwa jumla kama mwili wa Kristo; ili liwe kamilifu wakati wa kuja kwake Kristo, ambaye ni Bwana Arusi wake.
YOHANA 16:14-15
“Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba, atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.”
Shabaha iliyo nyuma ya kazi ya Roho Mtakatifu ni utukufu wa Kristo. Jinsi Yesu alivyojikana mwenyewe na kupitisha heshima yote kwa Baba yake tu, ndivyo pia na Roho Mtakatifu hatajiheshimu mwenyewwe, bali anamtukuza Yesu katika utendaji wake wote. Jambo hilo latufundisha sisi kuwa kimya juu ya yale tunayogundua, ushindi wetu na matendo yetu, ili tumtukuze Yesu Mwokozi pekee. Siyo jambo la kuokoka kwetu lililo na umuhimu wa kwanza, lakini kuoshwa kwa dhambi zetu ndani ya damu ya thamani ya Kristo. Shughuli zote za Roho, nguvu na makusudi zake zina shabaha moja tu, ni kumtukuza Yesu, aliyetununua kwa ajili yake. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia ya ushuhuda za mitume wa Kristo na kufaulu vema, wanapommwonyesha Kristo kwa wasikilizaji kuwa ndiye aliyesulibiwa na kufufuka.
Roho Mtakatifu haendelezi kazi fulani yeye peke yake, lakini anakamilisha yale ambayo Yesu aliyaanzisha katika maneno na matendo. Yeye huwakumbusha wanafunzi wa Yesu maneno ya Yesu na kutimiza maisha yake tukufu ndani yao. Anawasukumiza wazishike amri na maagizo yake, akiwasaidia wapate mizizi ndani ya Mwokozi wao. Hata toka mbali tunaona ushirikiano wao kwa wao inayoendelea kuwepo ndani ya Utatu Utakatifu. Nafsi moja hauchukui heshima kwa ajili yake mwenyewe, bali anaheshimu na kukuza wale wengine daima.
Wakati wa huduma yake hapo duniani, Yesu alitamka katika unyenyekevu wote; “Baba ni mkubwa kuliko mimi,” lakini katika hotuba yake ya kuaga alisema, “Enzi yote imekabidhiwa kwangu mbinguni na duniani”, maana Yesu aliumba yote katika ushirikiano na Baba. Baba ni yake (au yeye) mwenyewe akijitegemea; hata hivyo yu jisi alivyo kila baba na watoto wake, na wao kuwa wake Baba.
SALA: Bwana Yesu Kristo, ulitukomboa pale msalabani, ulipotuondolea mizigo ya dhambi zetu. Tunakushukuru kwa upendo wako unaozidi jambo lolote. Utujaze na Roho wako Mtakatifu, ili na maisha yetu yote yapate kutukuza sadaka yako na kufufuka kwako. Utuweke huru na uvivu, unafiki na kiburi, ili tuishi katika hali ya kweli ya maadili yako.
SWALI:
- Jinsi gani Roho Mtakatifu hufanya kazi katika maendeleo ya ulimwengu?