Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 094 (The world hates Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

3. Ulimwengu humchukia Kristo na wanafunzi wake (Yohana 15:18 - 16:3)


YOHANA 15:26-27
„Lakini ajapo huyu Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yeye atanishuhudia. Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.“

Lipi lilikuwa ni jibu la Utatu Utakatifu juu ya chuki ya ulimwengu na hatua yao ya kumsulibisha Mwana wa Mungu? Lilikuwa ni kumtuma Roho Mtakatifu duniani. Kuja kwa Roho ni mwujiza hata leo hii. Kuja kwake inadokeza kuja kwa Mungu ndani ya ulimwengu, maana anatokana na Baba, naye yuko na ushirikiano na Mungu katika hali yake na thibitisho lake. Anatamani ukombozi wa ulimwengu, akishiriki katika uumbaji. Roho huwa anahukumu uovu duniani, na kutuvuta kukaribia utakatifu wa Mungu, kwa vile anafunua machafu ya kila aina. Kuwepo kwake ndani ya wanafunzi inakuwa kitu cha kuchokoza unyenyekevu na kujikinahi, wakati dunia inaposongwa na kiburi, ushupavu na udanganyifu. Kwanza kabisa yeye ni roho wa ukweli, akikemea walimwengu kwa ajili ya udhalimu wao.

Pamoja na hayo huwafariji wanafunzi wake, akiwahakikishia kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu, anayekamilisha wokovu wao. Roho wa faraja huyu hupatia roho zetu ushuhuda juu ya Yesu, ili sisi tuone ndani ya upendo wa Mwana hali ya Baba mwenyewe. Bila huyu Roho Mtakatifu hatuwezi kutambua imani ya kweli. Pamoja na waumini wote tunakubaliana kwamba, hatuwezi kumtegemea Yesu Kristo Bwana wetu kwa bidii zetu sisi wenyewe au kwa welekevu wetu, wala hatuwezi kumfikia, isipokuwa kwa Roho yake, aliyetuita kwa kupitia Injili na kutumulikia na vipawa vyake pamoja na kututakasa kwa njia ya Imani ya kweli. Anawaita wakristo wote, akiwakusanya, kuwamulikia na kuwafanya wawe watakatifu ndani ya Kristo. Anawalinda ndani ya tumaini, iliyo kanuni ya imani ya kweli. Roho Mtakatifu huumba hali ya nguvu ndani ya ushuhuda wetu. Usitegemee ufahamu wako tu au uzoefu wako unapotaka kumwonyesha Kristo kwa wengine. Ujikabidhi kabisa kwake huyu Roho wa Hekima. Sikiliza maneno yake ili upate kujifunza namna ya kumkuza Yesu. Kusikiliza sauti ya Roho kwa moyo hivyo wakati ukishuhudia na kuzungumza na mtu, basi hayo yatakufanya uwe mtume wa kufaa wa Bwana Yesu.

Kristo aliwaita wanafunzi wake kumi na mmoja kwamba ni mashahidi wake, ambayo ni haki halisi kwao. Hao wanafunzi walikuwa ni mashahidi wa macho juu ya Yesu na kazi zake hapo duniani. Wao walikuwa wakishuhudia mambo ambayo waliyaona, kusikia na kuyagusa. Maneno yao yangethibitisha hoja ya kuwepo kwa Mungu hapo duniani. Imani yetu inatulia juu ya ushuhuda huo. Yesu hakuandika kitabu, wala barua, bali alikabidhi ujumbe wake wa kuokoa kwa ushuhuda wa Roho Mtakatifu na juu ya maneno ya wanafunzi wake na juu ya mwenendo wao. Huyu Roho wa kweli hawezi kusema uwongo, lakini kuithibitishia ulimwengu uliyo ngonjwa, habari ya nguvu ya upendo wa Kristo kwa njia ya midomo ya wanafunzi wake. Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake „Mtapokea nguvu, akiisha kuwajalia juu yenu Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu.“

SALA: Tunakuabudu, ewe Mwana wa Mungu, uliye Mtakatifu, wewe ni mmoja na Baba na Roho Mtakatifu, nawe hukutuacha yatima, lakini ulitutumia Roho yako ya kweli kwa ajili ya ushuhuda. Tuwe tumetakaswa kwa njia ya kuja kwako. Utufundishe namna ya kukushuhudia, ili na wengi wapate kukuamini.

SWALI:

  1. Jinsi gani Mungu anakabili ulimwengu, ambayo ulimsulibisha Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:49 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)