Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 093 (The world hates Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

3. Ulimwengu humchukia Kristo na wanafunzi wake (Yohana 15:18 - 16:3)


YOHANA 15:18-20
“Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake; ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.”

Baada ya Yesu kuwathibitishia umoja wake kamili na Mungu, na kutabiri kuja kwa Roho Mfariji, aliwatayarisha waweze kuvumilia chuki ya ulimwengu kwao.

Ulimwengu daima ni kinyume cha ushirikiano wa kikristo. Chuki inatawala dunia, lakini upendo unaongoza ushirikiano wa kikristo. Yesu hawaondoi wanafunzi wake kutoka kwa dunia la bahati mbaya na kuwapeleka kwenye kisiwa cha raha, hapana. Anawatuma ndani ya mazingira maovu, ili upendo wake upate kushinda kila chuki kali. Ujumbe huo sio matembezi ya raha, lakini ni mashambulio ya kiroho. Wao wanaotetea upendo watakutana na hali ya kukataliwa, chuki na kukemewa wakati wa kuhudumu, na sio kwa ajili ya makosa fulani, lakini kutokana na ushindano unaochochewa na roho mbaya zilizo kinyume cha neno la Yesu. Bwana wao aliyekuwa kamili katika upendo na hekima alikutana na chuki hiyo hadi mautini. Lakini mbali na hayo mateso makali, yeye hakutoroka kutoka kwa uwanda wa mapigano au kuondoka katika ulimwengu, bali alikufa hali akiwapenda wale waliomchukia.

Hakuna kati yetu aliye kama malaika; kutoka katika mioyo yetu kuna mawazo mabaya. Lakini kwa rehema ya Kristo roho nyingine mpya imetujia. Kuungama maana yake ni kubadilisha mwelekeo wa nia zetu. Yule aliyezaliwa na Roho siye wa dunia hii tena, bali ni wa Bwana. Yeye ametuchagua kutoka katika dunia hii. Neno la “Kanisa” kwa kiyunani inamaanisha kuwa ni mkutano wa waliochaguliwa na walioitwa kutoka kwa dunia hii, ili wapate kubeba madaraka. Kwa hiyo dunia inaangalia Kanisa kuwa ni mzaha. Tengano hilo linafanya nyufa za ajabu na usumbufu mkubwa hata katika familia, jinsi hata Yesu alivyoonja (Yohana 7:2-9). Katika hali hiyo yule anayedumu ndani ya Kristo anahitaji kuongezewa hekima na unyenyekevu aweze kuvumilia kuchokozwa na hata kupata mateso. Na wewe ukijikuta katika mazingira kama hayo, basi usisahau kwamba Yesu alipita katika hayo bila sababu. Kwa sababu aliwapenda na kuwaponya, hata hivyo bado walimsulibisha kama mhalifu.

Yesu anayo ahadi kuu kwa ajili yako kwamba, ingawa watu wanakutesa na kukugombeza, wachache baadhi yao watasikiliza kwa ushuhuda wako, jinsi walivyosikiliza ya kwake Yesu. Jinsi watu wa dunia hii waliojaliwa na Roho wakatokeza imani na upendo kuchanuka ndani ya wasikilizaji, ndivyo hata ushuhuda wako utaumba uhai wa milele ndani ya wachache wanaokusikiliza. Kila Mkristo ni mjumbe au mpelekwa wa Kristo ndani ya ulimwengu huu wa uadui. Basi, uhakikishe wito wako wa kimbinguni!

YOHANA 15:21-23
„Lakini haya yote watawatendea kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka. Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao. Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.“

Yesu aliwajulisha wanafunzi wake mapema kwamba, baada ya kupaa kwake mbinguni mateso makali yatawashambulia kwa ajili ya jina lake. Wayahudi hawakumtazamia Masihi aliye mnyenyekevu kama mwana kondoo, bali jitu mwenye siasa ya kuwaokoa kutoka kwa nira ya kikoloni ya Warumi. Maono hayo ya uongo kuhusu tumaini la wokovu ya kisiasa yalitokana na ujinga wao kuhusu enzi ya kweli ya Mungu. Walishindwa kutofautisha kati ya díni na serikali; walikuwa na Mungu wa kijeshi. Hawakumjua Baba wa Bwana wetu Yesu, ambaye ni Mungu wa starehe yote na amani. Ndiyo, anaruhusu mashambulio ya kivita - kama malipo ya kuadhibiwa, lakini vita hizo na ruhusa zake hazijengi Ufalme wa Mungu. Ni Roho yake tu anayeijenga katika kweli na usafi.

Kristo alikuja adhihirishe taratibu za Babaye waziwazi, lakini wayahudi walimkataa yule Roho wa upendo na upatanisho. Walifuatia ujeuri na vita. Mataifa yote yasiyomkubali Kristo aliye Mfanya Amani, basi huingia katika dhambi ile ile sawa na Wayahudi. - Dhambi yetu sio ile inayofanana na makosa ya adabu, bali ni uadui dhidi ya Mungu na hali yetu ya kukataa Roho yake ya Amani.

Kwa kawaida sababu za watu kumkataa Yesu, ufalme na amani yake ni hali yao ya kusadiki kuwa hakuna Mungu wa kweli. Watu hutambua miungu yao kutokana na mawazo yao wenyewe. Lakini Yesu alimfunua Mungu wa upendo kwetu. Basi yeye akataaye huo upendo, hufuatia njia ya ugomvi na uchafu, na amkataaye Kristo amkataa na Mungu wa kweli.

YOHANA 15:24-25
„Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.“

Yesu alitetea kwamba tangazo lake kuhusu ubaba wa Mungu itakuwa ni sababu ya hukumu kwa wale wanaojizuia kukubali sauti ya Roho, pamoja na miujiza yake mingi. Hakuna duniani aliyeweza au anayeweza kuponya kama Yesu, pamoja na kutoa roho za shetani, au kutuliza dhoruba baharini, au kulisha maelfu ya watu , au hata kufufua wafu. Mungu alikuwa kazini ndani yake kwa ishara hizo na thibitisho la uumbaji mpya kutokana na ufufuo wake. Wayahu hawakuona kitu cha ajabu ndani ya ishara hizo, kwa vile hazikuleta mabadiliko ya kisiasa au ubora wa kibiashara ndani yake kwa ajili ya taifa lao. Lakini walipotambua enzi ya upendo wa Yesu, matendo yake yote yakawa kama kikwazo kwao, kwa sababu walikataa kumwamini Baba. Jinsi Wayahudi walivyofunga roho zao dhidi ya mvuto wa Roho Mtakatifu, ndivyo hata leo mamilioni huishi ndani ya gereza la roho inayomkataa Mungu.Wale wasiokiri kwamba Kristo ndiye Mwana wa Mungu basi wanawachukia na wafuasi wake, wala hawamjui Mungu kwa kweli, wakidumu ndani ya dhambi zao, wakitukana na Utatu Utakatifu. Hata hivyo, Yesu hakuwahukumu moja kwa moja, lakini aliendeleza kazi zake za upendo kwa njia ya watumishi wake hadi leo. - Ndugu, jitayarishe kwa ajili ya mvutano huo wa kiroho, ukimwuliza Bwana wako akupatie nguvu na uvumilivu wa kudumu, pamoja na subira na utayari hata kupata mateso.

SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa ajili ya kukamilisha mipango yako mbali na chuki za watu. Tufundishe kuwapenda hata adui zetu, ili ikiwezekana wapate kuokoka. Fungua mioyo ya wote waliochaguliwa nawe wasikie sauti yako na kutenda mapenzi yako, wakikubali faraja ya Roho wako. Utuongoze na kutujalia nguvu zaidi na uvumilivu.

SWALI:

  1. Kwa nini ulimwengu unamchukia Kristo na wapendwa wake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:48 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)